Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro ameeleza kuwa wameanza ukaguzi wa kushtukiza kwa madereva wa magari wenye dalili za kutaka kusababisha ajali.
Pia ameeleza kuwa wamejipanga kushirikiana na nyumba za ibada ibada ili kutanzua uhalifu kabla, wakati na baada ya ibada mbalimbali kuelekea msimu wa sikukuu
===
TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama pia wananchi linaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuzuia vitendo vya kihalifu kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji. Hali ya usalama kwa ujumla ni nzuri na wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Pamoja na mambo mengine mwezi Octoba hadi Novemba 2025 Jeshi la Polisi kwenye sehemu ya mashauri yaliyofikishwa ofisi ya Mashitaka na baadae Mahakamani kumekuwa na mafanikio yaliyowezesha baadhi ya watuhumiwa kupatikana na hatia hasa wenye makosa yanayohusiana na ukatili kwa wanawake na watoto. Baadhi ya watuhumiwa waliopatikana na hatia ni 1.Abubakari Memba Abuu Mkazi wa Mbagala alihukumiwa kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa kosa la kulawiti 2.Julius Jasto Mbwambo mkazi wa Ukonga alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti 3. Paul Elisha mkazi wa Kawe alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya Kinondoni kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka 4. Erick Muhagama Mkazi wa Kimara alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya Ubungo kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti. 5. Khalifani Ramadhani Mkazi wa Kiponza Chamazi alihukumiwa na Mahakama ya Temeka kifungo cha Miaka 30 jela
kwa kosa la Unyang'anyi wa kutumia silaha, 6. Jackson Tumwesige na Abrahamani Hassani Mkwawa wakazi wa Ukonga walihukumiwa na Mhakama ya Wilaya ya Ilala kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali.
Katika kueleka sherehe za Krismas na mwaka mpya, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam litaendelea kushirikiana na umma katika kubaini, kuzuia na kutanzua mambo ya uhalifu na kushirikiana na nyumba za ibada ili kuhakikisha usalama unaimarika kabla, wakati na baada ya ibada mbalimbali.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu kwa watoto wakati wa matembezi na mikusanyiko mbalimbali, pia nyumba na makazi yasiachwe bila uangalizi kipindi chote. Suala la Usalama barabarani ukaguzi wa kushitukiza na kuwapima madereva wa vyombo vya moto umeanza. Polisi inatoa wito kwa watumiaji wengine wa barabara kuzingatia sheria ili kuepusha ajali. Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali na za haraka za kisheria kwa wote watakao bainika kutenda makosa.
Polisi inawaonya na kutao tahadhari kwa watu wenye tabia ya kupiga baruti au fataki bila vibali vya kisheria na kusababisha usumbufu na hofu kwa umma. Polisi haitasita kuchuka hatua kwa mtu yeyote atakaye kiuka sheria Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inawatakia maandalizi mema na kusherehekea kwa amani siku kuu hizo.
Imetolewa na;
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam