Polisi Moro na mazoezi ya kufa mtu, ni yale Maandamano yetu?

Polisi Moro na mazoezi ya kufa mtu, ni yale Maandamano yetu?

Polisi Moro wakiwa na vifaa vyao timamu, yakiwamo yale magari pendwa yenye uwezo kamili wa kuzima moto bali yakitumika kama washawasha wamefanya mazoezi ya kufa mtu Moro:


View: https://m.youtube.com/watch?v=kKIzxrOI-V4

Ni wazi kuwa isingalikuwa taabu kuudhibiti moto ule na mapema asubuhi Kariakoo, laiti hata kama yangetumika kama yalivyo na machache yao tu. Wala si mengi.

Kama ilivyokuwa kwa wale wa zoezi la usafi enzi za operation ukuta, hawa wamejumuisha wakiviita pamoja na vyombo vile vingine vyote ..

"Bila shaka ni zile tishia nyau zetu kazini sasa."

Izingatiwe jemedali Mwabukusi amekuwa wazi:

"taratibu zote za kisheria zitafuatwa."

Ya kuwa 7 October kutakuwa na tamko rasmi.

Kasisitiza Mwabukusi watanzania siyo waoga. Ya kuwa mwenye kuwadhania vinginevyo na akaeleke jiwe.

Viva Mwabukusi.

Mlipo tupo!

Mazoezi hayatabadili kuzaliwa upya kwa Tanganyika
 
Hawa wapelekwe kwa alshabaab waache kudekadeka hapa kwa kubebwa na rais na mahakama. Hivi kweli unabeba RPG eti unaonesha uwezo wa kupambana na wahalifu?! Kwamba mhalifuni adui sio mkengeufu wa sheria anayestahili kupelekwa mahakamani isipokuwa auawe?
 
Back
Top Bottom