Polisi: Msamaha wa kutoshtakiwa kwa wamiliki wa silaha kinyume cha sheria walioanza kusalimisha silaha kuanzia Sept 1 - Okt 31

Polisi: Msamaha wa kutoshtakiwa kwa wamiliki wa silaha kinyume cha sheria walioanza kusalimisha silaha kuanzia Sept 1 - Okt 31

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa taarifa rasmi kuhusu operesheni mbalimbali zilizofanyika katika kipindi cha hivi karibuni. Taarifa hiyo inatoa muhtasari wa hatua zilizochukuliwa na jeshi hilo katika kudhibiti uhalifu na kuhakikisha usalama wa raia.

Katika taarifa hiyo, Jeshi la Polisi limeeleza kwamba operesheni hizo zimepelekea kukamatwa kwa wahalifu wengi, pamoja na silaha na vitu mbalimbali vya uhalifu vilivyokuwa vikitumika katika shughuli haramu. Polisi pia imethibitisha kwamba kuna ushirikiano mzuri kati ya wananchi na jeshi hilo, huku raia wakihamasishwa kutoa taarifa kuhusu shughuli zinazoshukiwa kuwa za uhalifu katika jamii zao.
Screenshot_20241004-142049_1.jpg
Screenshot_20241004-142100_1.jpg
 
Utani kwani sio watekaji?
Acha kulichafua Jesi letu ambalo linaendelea kufanya kazi nzuri sana katika ulinzi wa Raia na mali zao. Kumbuka unalala salama na kuamka salama wewe na mali zako kwa sababu kuna askari wanaokesha usiku kucha wakikulinda wewe na mali zako na kupambana na wahalifu wa kila aina.
 
Niwachafue kwani ni wasafi? Hawanilindi kama hisani, ni wajibu wao maana maana wanalipwa mshahara kutokana na kodi yangu. Kama huamini waambie waache kulinda uone watakula wapi. Ww mwanaccm ndio unapaswa kuwasifia polisk kwakuwa huwa wanawasaidia kukaa madarakani kwa shuruti kupitia wizi wa kura.
 
Polisi pia imethibitisha kwamba kuna ushirikiano mzuri kati ya wananchi na jeshi hilo, huku raia wakihamasishwa kutoa taarifa kuhusu shughuli zinazoshukiwa kuwa za uhalifu katika jamii zao.
Mmeanza kuogopa? Sasa tunasema haturudishi silaha ng'o! Nyie mkija kututeka mjue ama zenu ama zetu. Njooni tutoane jasho, mmezoea za kunyonga nyie, njoo mkabili za kuchinja muone kazi hapa!
 
Back
Top Bottom