BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Tukio hilo lilitokea katika ukumbi wa disco ujulikanao kama ‘The Don’ uliopo Kata ya Ziwani katika Halmashauri ya Wilaya Mtwara June 30 mwaka huu baada ya kuzuka kwa ugomvi.
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amesema kuwa ugomvi ndiyo uliosababisha kifo cha Humbu mkazi wa Kijiji cha Majengo katika halmashauri hiyo.
Amesema kuwa kijana huyo alifariki njiani kabla ya kufikishwa hospitalini kufuatia jeraha ubavuni upande wa kushoto, lililotokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali. Anayedaiwa kufanya kitendo hicho ni Ally Salum maarufu kama Chepe.
“Inaoneka kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliozuka baina ya marehemu na mtuhumiwa Ally Salum ambapo baada ya tukio hilo alitokroka na hadi sasa jitihada za kumtafuta zinaendeleea ili sheria iweze kufuata mkondo wake,” amesema.
Katika tukio hilo watu wawili walikamatwa kwa mahojiano zaidi ambao ni Aziz Salum Mkumba (32) mkazi wa Kijiji cha Mkubiru pamoja na Shaibu Bakari Mpoyo (33) mlinzi wa ukumbi wa Ziwani kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.