Bwana Mambosasa amesema mwili wa Mangula umekutwa na sumu. Hapohapo akaeleza kwamba uchunguzi wa "tuhuma" za sumu hiyo unaendelea. Pigia mstari neno TUHUMA
Sasa tuendelee;
1⃣; Mambosasa hajaeleza chanzo cha sumu kwenye mwili wa Mangula. Je alilishwa sumu, alinusa, aligusa, au alijilisha mwenyewe kwa kula vyakula vilivyo contaminated na sumu?
_
2⃣; Anaposema wanafanya uchunguzi wa TUHUMA wakati bado hajui chanzo cha sumu hiyo, je anachunguza nini? Ni lazima kwanza madaktari waeleze chanzo ndipo polisi waanze kutuhumu watu. Huwezi kukimbilia kutuhumu bila kwanza kujua chanzo. Hivi ripoti ya madaktari ikionesha kuwa chanzo cha sumu ni Mangula mwenyewe mtampiga pingu kwa jaribio la kutaka kujiua?
3⃣; Kabla Mambosasa hajajitokeza kwenye camera angewaacha kwanza madaktari wafanye kazi yao. Mambo ya kitaalamu yanahitaji kutolewa maelezo na wataalamu, for this case medical personnels, sio Askari polisi aliyesoma miezi sita CCP Moshi, anayevaa "jungle" na staff shoes.
4⃣; Mambosasa anasema wanafanya uchunguzi wa tuhuma za sumu. Unaposema tuhuma (allegations) means kuna mtu unamtuhumu (alleged). Je wanamtuhumu nani? Na kwanini wakimbilie kutuhumu watu wakati chanzo cha sumu hiyo hakijajulikana? Kukimbilia kutuhumu watu kabla ya kujua chanzo, inaweza kutafsiriwa kuwa Polisi wamejiandaa kumuangushia mtu "jumba bovu".
_
5⃣; Mambosasa ametoa taarifa kwa umma ambayo inaleta mkanganyiko. Anasema wanafanya uchunguzi kujua sumu hiyo iliingiaje mwilini mwa Mangula. Lakini hapohapo anasema aliyehusika kumlisha Mangula sumu atasakwa usiku na mchana. Hapa ni kama Mambosasa ameshacoclude kuwa Mangula amelishwa sumu lakini hapohapo anasema hawajui sumu iliingiaje mwilini. Contradiction. Kama hawajui sumu iliingiaje mwilini huyo wanayemsaka usiku na mchana ni nani? Mambosasa ajifunze kufanya kazi kwa weledi badala ya kupenda sana camera.!
*Anaandika fundi Malisa GJ!*