Polisi: Mzee Philip Mangula amekutwa na sumu mwilini, ni baada ya kufanyiwa uchunguzi

Polisi: Mzee Philip Mangula amekutwa na sumu mwilini, ni baada ya kufanyiwa uchunguzi

CCM mmeanza kumalizana wenyewe...
Kwani ndio wakwanza huyu? Mbona hata yule aliyekimbizwa india rafiki yake ambae ni marehemu kwasasa alikiri wazi kabisa kuwa rafiki yake kapewa sumu
 
Ee Baba nusuru chama makini Leo hii tunapoingia majaribu ya kifunga watu wasiohusika, watie akili uweledi wasimamizi Wa sheria watende haki, achana kabisa na chama twawala waendelee kuana na kulana kama kuku Wa mayai. Wanyonyoane had I wabaki vipara moto kama kuku kishingo.
 
Jpm!"niliwahi kuwekewa sumu !nikaomba kujiuzulu wakanikatalia"!Leo Mangula ana sumu mwilini baada ya kumfukuza membe Chamani!!!Naendelea kuunganisha data!kwa mbaaaali na nusa ugoro!!!ACHA NIPIGE CHAFYA NTARUDI BAADAE!!!
Kabla hakuwa na hiyo sumu?
 
Bwana Mambosasa amesema mwili wa Mangula umekutwa na sumu. Hapohapo akaeleza kwamba uchunguzi wa "tuhuma" za sumu hiyo unaendelea. Pigia mstari neno TUHUMA

Sasa tuendelee;

1⃣; Mambosasa hajaeleza chanzo cha sumu kwenye mwili wa Mangula. Je alilishwa sumu, alinusa, aligusa, au alijilisha mwenyewe kwa kula vyakula vilivyo contaminated na sumu?
_
2⃣; Anaposema wanafanya uchunguzi wa TUHUMA wakati bado hajui chanzo cha sumu hiyo, je anachunguza nini? Ni lazima kwanza madaktari waeleze chanzo ndipo polisi waanze kutuhumu watu. Huwezi kukimbilia kutuhumu bila kwanza kujua chanzo. Hivi ripoti ya madaktari ikionesha kuwa chanzo cha sumu ni Mangula mwenyewe mtampiga pingu kwa jaribio la kutaka kujiua?

3⃣; Kabla Mambosasa hajajitokeza kwenye camera angewaacha kwanza madaktari wafanye kazi yao. Mambo ya kitaalamu yanahitaji kutolewa maelezo na wataalamu, for this case medical personnels, sio Askari polisi aliyesoma miezi sita CCP Moshi, anayevaa "jungle" na staff shoes.

4⃣; Mambosasa anasema wanafanya uchunguzi wa tuhuma za sumu. Unaposema tuhuma (allegations) means kuna mtu unamtuhumu (alleged). Je wanamtuhumu nani? Na kwanini wakimbilie kutuhumu watu wakati chanzo cha sumu hiyo hakijajulikana? Kukimbilia kutuhumu watu kabla ya kujua chanzo, inaweza kutafsiriwa kuwa Polisi wamejiandaa kumuangushia mtu "jumba bovu".
_
5⃣; Mambosasa ametoa taarifa kwa umma ambayo inaleta mkanganyiko. Anasema wanafanya uchunguzi kujua sumu hiyo iliingiaje mwilini mwa Mangula. Lakini hapohapo anasema aliyehusika kumlisha Mangula sumu atasakwa usiku na mchana. Hapa ni kama Mambosasa ameshacoclude kuwa Mangula amelishwa sumu lakini hapohapo anasema hawajui sumu iliingiaje mwilini. Contradiction. Kama hawajui sumu iliingiaje mwilini huyo wanayemsaka usiku na mchana ni nani? Mambosasa ajifunze kufanya kazi kwa weledi badala ya kupenda sana camera.!
*Anaandika fundi Malisa GJ!*
 
Sio kila kitu polisi waseme. Hilo suala la kidaktari ilishindikana nini daktari akaongelea hilo tena huwenda angekuja na maelezo ya kitaalamu zaidi.

"Polisi wameelezea namna mkazi wa Buza alivyoshinda Jackpot"
Tukisema ianzishwe Bureau ya Investigation ambayo ina watu wenye professional zao wengi wanapinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda itakuwa kuteka na kuua.
"....litachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakaye bainika kupanga,......." napata shida kuelewa hii "statement" kwani zaidi ya kukamata, kuchunguza na kumpeleka mtuhumiwa mahakamani hatua kali zinazongunzwaga na Jeshi letu ni zipi kwa mujibu wa Katiba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaweza kuwa Corona, wana CCM bado wanasalimiana kwa mikono.
 
Bwana Mambosasa amesema mwili wa Mangula umekutwa na sumu.
Uandishi wa namna hii siyo mzuri hata kidogo....Jana nilishtuka sana....! Hivi hata Moderators hawajaona tatizo kwenye uandishi wa maneno ".............Mwili wa Mzee Philip Magula umekutwa na sumu....." ? Hivi ilishinidikana vipi kuandika kuwa ".....Mzee Mangula agundulika kuwa na sumu mwilini..."
====
Nikirudi kwenye mada.
Awali wakati Mheshimiwa Rais alipomtembelea Mzee Mangula hospitalini, kuna wafuasi maarufu wa chama fulani cha siasa hapa Jamvini, yaliwaoka maneno ya ajabu sana. Wakajivika na utaalamu wa saikolojia na usomaji wa lugha za mwili. Wakahusisha, "kuugua ghafla kwa Mzee Mangula" eti na kutokukubaliana na baadhi ya mambo ya wawili hao kwenye maamuzi yaliyofanywa na chama wiki kadhaa zilizopita.

Picha na video zilizopigwa hospitalini zikatumika eti kama ushahidi wa maneno yaliyowatoka 'wafuasi hao maarufu wa chama fulani'. Kiko wapi sasa...! Ukweli unaanza kudhihirika. Acheni 'kuropoka' na kuhisi vitu visivyo na msaada huku mkipalilia nia zenu ovu dhidi ya nchi hii.
 
Huyo atakuwa alikula kilaji kilichokusudiwa kupewa mtu mwingne bhana!! Duniani kote wanaomiliki sumu za kuwapa vigogo ni kitengo maalum cha nchi ila walijichanganya Wakati Wa kugawa ndio wakajikuta Ngoma inaenda kwa Mwenyekiti si mnajua Tz bado hatuna wasomi wa hali ya Juu Ya ubobezi? Wote wababaishaji tu walimtega mwingne wakajikuta wananinasa wenyewe kutokana na umakini hafifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
IMG-20191216-WA0001.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Wamekamatwa wahudumu wa vyakula na kikaoni wangapi?
  • Wamekamatwa Wana-Kamati wenzake wangapi?
  • Wamekamatwa wahojiwa wangapi?
  • Wamekamatwa maafisa wa CCM Lumumba wangapi?
  • Wamekamatwa maafisa wanaoshughulika na usalama wa CCM na viongozi wake wangapi?
  • Wamekamatwa wanafamilia wake wangapi?
  • Wamekamatwa walio Serikalini au nje ya Serikali wangapi?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Uandishi wa namna hii siyo mzuri hata kidogo....Jana nilishtuka sana....! Hivi hata Moderators hawajaona tatizo kwenye uandishi wa maneno ".............Mwili wa Mzee Philip Magula umekutwa na sumu....." ? Hivi ilishinidikana vipi kuandika kuwa ".....Mzee Mangula agundulika kuwa na sumu mwilini..."

Vipi ikiwa uandishi na uwasilishaji haujakosewa, wanaposema “mwili wa Mzee”..... kwanini usiwaze kuwa huenda tayari RIP..?
 
Back
Top Bottom