Polisi: Mzee Philip Mangula amekutwa na sumu mwilini, ni baada ya kufanyiwa uchunguzi

Polisi: Mzee Philip Mangula amekutwa na sumu mwilini, ni baada ya kufanyiwa uchunguzi

Duuh...sasa kweli naamini fisi wanakula fisi...
Aisee, mzee wa watu, aache siasa sasa lasivyo, sasa hivi tutamuwish, apumzike kwa amani...

Everyday is Saturday..................... 😎
 
Eti wanasema Sumu waliopang kumpa
Jasusi Mbobezi kwenye Mahojiano na Kamat ndogo ya Fisiemu Dodoma Ndio Kala Mangalu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jasusi alisema "Sikiliza nina watu wangu serikalini,nina watu ndani ya chama na nina watu ndani ya usalama".Jasusi mbobezi anahitaji akili sana kummaliza,anajua mno mbinu na uwezo wa wanaomsumbua.
 
Kuna mtu mmoja hivi wanampangia mkakati wa kumkamata ili asichukue FORM YA URAIS, wampe kesi ya jinai ya KUSUDIO LA KUUA, maana wameona ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha raia tumezizoea kuona wanaompinga jiwe kusukumiwa nazo.

Aliowashauri anawapotosha, wsijaribu hilo wanalotaka kufanya kwa huyo mtu, maana raia wanaweza kuingia mtaani.
Tatizo kwenye vikao vyao vya sumu wala hakuwemo!
 
Hayamambo yanahitaji subira jamani so yakukimbilia kutoa maoni
 
M/Mwenyekiti wa CCM, Mzee Philipo Mangula akurwa na dalili za sumu. Sio mwili!. Neno mwili linatumika kwa the deceased!.
P

Hakika kabisa, kauli ya ofisa ngazi ya juu kusema na kutumia maneno hayo hata IGP itamtatiza leo, kama ile siku IGP alivyotoa karipio la mavazi ya Mambosasa kuchanganya / kuvaa jungle uniform na kuitisha press conference zinazozidi kuchanganya umma au kuharibu uchunguzi kwa wanaoshukiwa kuwa na tuhuma.
 
Kuna mtu mmoja hivi wanampangia mkakati wa kumkamata ili asichukue FORM YA URAIS, wampe kesi ya jinai ya KUSUDIO LA KUUA, maana wameona ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha raia tumezizoea kuona wanaompinga jiwe kusukumiwa nazo.

Aliowashauri anawapotosha, wsijaribu hilo wanalotaka kufanya kwa huyo mtu, maana raia wanaweza kuingia mtaani.
Very Possible idea
inawezekana kabisa
 
a9c2c648-b26e-4fe3-8d8c-4e04a7160cda.jpg



Bwana Mambosasa amesema mwili wa Mangula umekutwa na sumu. Hapohapo akaeleza kwamba uchunguzi wa "tuhuma" za sumu hiyo unaendelea. Pigia mstari neno *TUHUMA.*

Sasa tuendelee;

1⃣; Mambosasa hajaeleza chanzo cha sumu kwenye mwili wa Mangula. Je alilishwa sumu, alinusa, aligusa, au alijilisha mwenyewe kwa kula vyakula vilivyo contaminated na sumu?
_
2⃣; Anaposema wanafanya uchunguzi wa TUHUMA wakati bado hajui chanzo cha sumu hiyo, je anachunguza nini? Ni lazima kwanza madaktari waeleze chanzo ndipo polisi waanze kutuhumu watu. Huwezi kukimbilia kutuhumu bila kwanza kujua chanzo. Hivi ripoti ya madaktari ikionesha kuwa chanzo cha sumu ni Mangula mwenyewe mtampiga pingu kwa jaribio la kutaka kujiua?

3⃣; Kabla Mambosasa hajajitokeza kwenye camera angewaacha kwanza madaktari wafanye kazi yao. Mambo ya kitaalamu yanahitaji kutolewa maelezo na wataalamu, for this case medical personnels, sio Askari polisi aliyesoma miezi sita CCP Moshi, anayevaa "jungle" na staff shoes.

4⃣; Mambosasa anasema wanafanya uchunguzi wa tuhuma za sumu. Unaposema tuhuma (allegations) means kuna mtu unamtuhumu (alleged). Je wanamtuhumu nani? Na kwanini wakimbilie kutuhumu watu wakati chanzo cha sumu hiyo hakijajulikana? Kukimbilia kutuhumu watu kabla ya kujua chanzo, inaweza kutafsiriwa kuwa Polisi wamejiandaa kumuangushia mtu "jumba bovu".
_
5⃣; Mambosasa ametoa taarifa kwa umma ambayo inaleta mkanganyiko. Anasema wanafanya uchunguzi kujua sumu hiyo iliingiaje mwilini mwa Mangula. Lakini hapohapo anasema aliyehusika kumlisha Mangula sumu atasakwa usiku na mchana. Hapa ni kama Mambosasa ameshacoclude kuwa Mangula amelishwa sumu lakini hapohapo anasema hawajui sumu iliingiaje mwilini. Contradiction. Kama hawajui sumu iliingiaje mwilini huyo wanayemsaka usiku na mchana ni nani? Mambosasa ajifunze kufanya kazi kwa weledi badala ya kupenda sana camera.!
*Anaandika fundi Malisa GJ!*
 
Vizee hivi kwa kupenda kulakula bana. Usikute alidokoa Ubwabwa ulioandaliwa kwa ajili ya Kachero mbobezi.

Na ni huyu huyu alikuwa kwenye kamati ya maadili ya kumkata Laigwan na kuropokaropoka hatutaki rais atakaye kuwa mgonjwa


-NGUSERO-
 
Haijawahi tokea mtu aliekweye system katika nafasi ya Juu Ya uongozi akalishwa Sumu na mtu ambae hayuko kwenye system, duniani kote Sumu za aina hiyo humilikiwa na watu wakubwa kimamlaka na kifedha, sumu inayoanza kufanya Kazi baada ya Siku kadhaa ni sumu inayonunuliwa toka nje nchi na watu wazito,

na mara nyingi sumu za aina hiyo hutumiwa na kitengo maaalum cha nchi Au wafanyabiashara wakubwa wenye Sauti ndani ya utawala, na sumu za aina hiyo hutegewa watu wazito au watu walioziandaa kukosea step Wakati Wa implementation kwa Kukosea hesabu na kujikuta kapewa mtu ambae hakuwa kusudio, yani

Mfano, kwa kuweka kwenye Maji ya chupa halafu Wakati mnagawa Maji mnajikuta Maji yanaenda kwa mtu ambae hakuwa mlengwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vizee hivi kwa kupenda kulakula bana. Usikute alidokoa Ubwabwa ulioandaliwa kwa ajili ya Kachero mbobezi.

Na ni huyu huyu alikuwa kwenye kamati ya maadili ya kumkata Laigwan na kuropokaropoka hatutaki rais atakaye kuwa mgonjwa


-NGUSERO-
Kwahiyo alionja kama imekolea
 
Back
Top Bottom