Msitafute mchawi hana tishio lolote huyo mzee! Kila mtanzania hasa wabongo Darisalama wana sumu mwilini mwao, inayozalishwa kwa ajili ya kukaa kwenye Mazingira mabaya, hatari, na machafu, yasiyo salama, kama keko Magurumbasi, karibu tu na hapo lumumba, Jiji gani linakuwa na cholera mwaka mzima? tena wilaya iliyoko Ikulu?
Viongozi wanajidanganya wakidhani kuwa wao wako salama sana, na majanga! kumbe dhambi ya uzembe inawatafuna angalia sasa! wanavoadhirika huyu kafakamia samaki (Sato) wa Mwanza waliowekewa Formalin nyingi kupita kiasi,kwenye kikao! akashushia na maziwa ya kutoka gongo la mboto!
Bongo yenu, ni hivi; chakula kibaya, kisicho zingatia ubora wa kanuni za afya, km Ngano mbovu, Vibudu vya ng'ombe wanaojifia Pugu mnadani, nyama za kuku mfu kutoka Pollo Amadori, samaki waliopuliziwa dawa za kutunzia mahiti (Fomalin) ili wasiharike haraka wakati wanasafirishwa!
Maziwa ya ng'ombe waliodungwa Sindano muda huo huo, kikawaida inatakiwa ichukue siku 4-7, ndo ukamue, matumizi ya maji ya visima vifupi, vinyesi vitupu, hasa kwa Aziz ally, Kipawa, Mbagalla, Temeke wailles,Salasala nk, wakati water table iko juu juu ya kiwango kisichotakikana kitaalamu!
Uoga wa ukosefu wa hela na mafanikio binafsi, vibaka, kuvamiwa, kupoteza madaraka, majanga km haya kwa binadamu huzalisha kemikali mbaya sana mwillini aina ya Adrenalin , hii huwa sumu baada ya muda. unaweza pata magonjwa kama, Renal failure, BP, IDDM, Sudden death, Herpes zoster nk.
Sumu ya kweli asingebaki salama aombe hata maji? muangaliege!
Mnaishi na kuwa hai kwa kudra za mwenyezi Mungu, na Hospitali zenu mbovu hizo zenye magonjwa tele., hajakimbizwa South?