Polisi na NEC waanza kuhofia barua za Amsterdam & Partners LLP?

Polisi na NEC waanza kuhofia barua za Amsterdam & Partners LLP?

mbona hata Libya na Iraq zilikuwa zinasema hivi hivi zilipokuwa chini ya marais madikteta?

kikubwa ni haki itamalaki miongoni mwetu ili haya masahibu yasitupate.
Libya na Iraq mkuu ni tofauti na Tanzania. Hizo nchi ni waislamu na unajua wenzetu na dini yao. Sisi rais anasisitiza umoja, upendo na kuchapa kazi. Lisu na wapinzani wanasisitiza vita, wazungu na kuchukiana.
 
Mnachekesha, sisi ni nchi huru, tunajiamlia mambo yetu. Wazungu wajanja hapo hiyo gharama imeahidiwa kulipwa kwa mikataba minono ya upendeleo atakayo itoa lisu pindi akiwa rais (kitu ambacho hawezi kuwa rais maana watamuua akishindwa urais).
Watu wa propaganda lumumba mnakwama wapi?Mnadhani mnawaandikia wajinga humu jf?idiot
 
Quinine,

Amsterdam hatanii mwaka huu. Mitambo yote iko Tanzania. Lolote wanalofanya watu wanachukua ushahidi na kwenda mbele.

Nilisema humu na nasema tena humu. Huu ndo mwaka sahihi wa kuitoa madarakani CCM .?Hakuna kipindi rahisi kama mwaka huu na sababu kuu ni kwamba mwaka huu CCM lazima wataiba kura, na kama Lissu alivyosema kamwe hatokubali kuibiwa ivyo watu wataingia mtaani. Nina uhakika watu wakiingia mtaani polisi lazima watatumia nguvu na hapo ndo Amsterdam atapata ushahidi wake wote kupeleka ICC.

Chadema, ushauri wangu kwenu ni kuwa komaeni hivi hivi. Hawa CCM mwaka huu lazima watoke.
 
Uhuru wa kufanya utakalo /pumbavu
Mnachekesha, sisi ni nchi huru, tunajiamlia mambo yetu. Wazungu wajanja hapo hiyo gharama imeahidiwa kulipwa kwa mikataba minono ya upendeleo atakayo itoa lisu pindi akiwa rais (kitu ambacho hawezi kuwa rais maana watamuua akishindwa urais).
 
Libya na Iraq mkuu ni tofauti na Tanzania. Hizo nchi ni waislamu na unajua wenzetu na dini yao. Sisi rais anasisitiza umoja, upendo na kuchapa kazi. Lisu na wapinzani wanasisitiza vita, wazungu na kuchukiana.
Wapi Lissu amesisitiza vita? Kawadanganye wajinga wenzio.
 
Bila shaka kuna soft power fulani imetumika kwanza kuwezesha Lissu kurudi bila kukamatwa wala kubughudhiwa.

Hata Makonda kushindwa ubunge na hatimaye kuwekwa pembeni kwenye uongozi naamini ilikuwa ni janja ya kumuweka pembeni huku wakubwa wakisitiri sura zao. Makonda hakuwa mtu wa kuumbuliwa na wajumbe.

Tutaendelea kuona mengi ila itahitaji jicho la tatu.

Reagan aliwahi kusema, speak softly but carry a big stick.
 
Quinine,

Yaani hao amtardam wanaweza kupangia nchi mambo yao?

Nakushangaa sana hao amstardam wana mahusiano gani na Tanzania mpaka watupangie, yaani bavicha akiri zenu ni sifuli tu.
Hao wana mkataba na Lisu na sio mchi ya tanzania. Na hawana uwezo wowote wa kutupangia mabo yetu ila wanaweza kumpangia Lisu kwani ni kibaraka wao.
 
Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa barua kutoka kampuni binafsi ya Amsterdam & Partners LLP, walioingia mkataba na mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu kumsaidia masuala yake ya kisheria, kiusalama na ulinzi wa haki zake.

Moja ya sehemu ya barua yao waliyoliandikia Jeshi la polisi inasema,

"By this letter, we notify you (Tanzania Police) our intention to hold accountable all public servant of the government of Tanzania individually..... " Robert Amsterdam.

Vile vile waliiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kuwa,

“It is our intent to hold the members of the NEC personally accountable”, Robert Amsterdam.

Jana Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amewataka makamanda wa jeshi hilo kuja na majibu ya nguvu kwa mikoa iliyo anza kufanya vurugu kwenye misafara ya wanasiasa ikiwemo kurusha mawe na wale waliohusika kuchoma ofisi za vyama vya siasa.

"......mtu yeyote wa ovyo ovyo atakaejihusisha na uchomaji wa ofisi au kujihusisha na vurugu tutamshughulikia vizuri" IGP Sirro.

Je, hizi zinaweza kuwa dalili kwa jeshi la polisi kuanza kubadilika au ni kwa sababu ya vitisho vya barua za Robert Amsterdam?
Kabla ya barua ya Amsterdam, Sirro na Magufuli walikuwa wamemnyima Lissu ulinzi...baada ya pale siku ya pili yake wakampa Ulinzi na akawa habughudhiwi kwenye mikutano yake
 
Yaani hao amtardam wanaweza kupangia nchi mambo yao?

Nakushangaa sana hao amstardam wana mahusiano gani na tanzania mpaka watupangie, yaani bavicha akiri zenu ni sifuli tu.

Hao wana mkataba na Lisu na sio mchi ya tanzania. Na hawana uwezo wowote wa kutupangia mabo yetu ila wanaweza kumpangia Lisu kwani ni kibaraka wao.
Mbona wewe Akili yako ni zero tena wewe ni juha zuzu kabsa, hawana uwezo wa kukupangia mbona kutwa CCM mnaenda kuomba misaada ulaya na shirika la fedha IFM huwapangia mashariti? CCM ikienda kupiga magoti kuomba omba misaada ulaya huwaita wazungu wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa ujinga wenu wa CCM mnakimbilia kuwaita wanaume wenzenu mabeberu utazani nyinyi CCM ni mbuzi jike.
 
Quinine,

Mtanzania ni mtu wa ajabu na uhovyo mwingi Sana

Mtu akitaka kufanya kazi yake, utasikia ameogopa, akitaka kubinya kidogo, amenunuliwa, anamfanyia mfalme n.k

Sasa tuwaeleweje!!!
 
Mtanzania ni mtu wa ajabu na uhovyo mwingi Sana

Mtu akitaka kufanya kazi yake, utasikia ameogopa, akitaka kubinya kidogo, amenunuliwa, anamfanyia mfalme n.k

Sasa tuwaeleweje!!!
CCM waache kuwabambikia kesi kuwapiga risasi kuwapora ushindi wapinzani
 
Mkuu ebu kuwa serious kidogo basi

Angalau make your sons and daughters be proud kwa sababu yako

Unaamini kabisa kwa akili zako timamu dola na nchi huru inaweza kutikisika kwa barua ya private firm? Wana nini zaidi ya kuandika tu?

Na kabisa ulichoandika hapa maadui wa Liss hawawezi kulibeba hili kisiasa? Kuwa katumwa na wazungu?

Hivi huwa mnafikiria kabla ya ku post au uhalisia ndio kweli kabisa uwezo wa fikra ulipoishia?

You are better than this
Amsterdam & Partners LLP – International Law Firm | London | Washington DC

Amsterdam & Partners LLP

Experienced partners to navigate both crisis and opportunity. Amsterdam & Partners LLP is a trusted advisor to clients experiencing complex challenges.

Our Practices

Arbitration & Litigation
Anti-Corruption
Extractive Industries
Frontier Markets
Human Rights
Crisis Management
 
Libya na Iraq mkuu ni tofauti na Tanzania. Hizo nchi ni waislamu na unajua wenzetu na dini yao. Sisi rais anasisitiza umoja, upendo na kuchapa kazi. Lisu na wapinzani wanasisitiza vita, wazungu na kuchukiana.
Lissu anawahadaa wazungu na hasa umati aliopata katika ziara zake za utalii unampa kichwa, umati kama ule haujaanzia kwaLissu, Mrema alipata sana tu, akaja Lipumba na Ngangali akapata umati wa kutosha na wao walifikia hata kutangaza balaza la mawazi kabla ya kupiga kura, akaja Dr. Slaa naye alipata sana tu, wakamalizia na Lowasa ambaye hadi barabara zilidekiwa na kina mama kutandika khanga barabarani.

Amsterdam anatakiwa ajue kuwa kujaza umati siyo kushinda uchaguzi, kuwa wajumbe wanaofanya maamuzi, Tundu lissu anataka kuvuta pesa tu hana jipya. Historia ya nyomi kwa atanzania iko wazi.

Baada ya october Lissu hatataka hata kuongea na waandishi wa habari kwa aibu
 
Kabla ya barua ya Amsterdam, Sirro na Magufuli walikuwa wamemnyima Lissu ulinzi...baada ya pale siku ya pili yake wakampa Ulinzi na akawa habughudhiwi kwenye mikutano yake
IGP ile video yake ya vitisho aliyoitoa juzi imefika The Hague wanaanza vikao vya kumjadili ikiwezekana aunganishwe kwenye kesi
 
Back
Top Bottom