Polisi na NEC waanza kuhofia barua za Amsterdam & Partners LLP?

Nimekuwa nikijiuliza kuwa hivi hiki kizazi ndio cha kupeleka nchi mbele

Mtu anaanini kuwa nchi fulani au private fulani inaweza kuitisha nchi huru nyingine?

Yaani mtu ana akli timamu ana post eti barua imetumwa kwa jeshi la polisi, si bora iliyotumwa officially na nchi , yaani mfano Mkono advocate Company iitishie Trinidad and Tobago? Tuwe serious hii ni aina ya akina chief Mangungo wa Msowero kwa aina tofauti

Ni mpumbavu tu ndio atanunua wazo la post hii.
Msitufadhaishe kuwa upinzani umesheheni Malimbukeni wakati kuna wasomi wazuri au kuna wasomi wa makaratasi wamegoma kutumia akili zao zote
 
Libya na Iraq mkuu ni tofauti na Tanzania. Hizo nchi ni waislamu na unajua wenzetu na dini yao. Sisi rais anasisitiza umoja, upendo na kuchapa kazi. Lisu na wapinzani wanasisitiza vita, wazungu na kuchukiana.
kwani Waislamu wana matatizo gani comrade?
kama wana matatizo mbona mwenyekiti wetu (Mkatoliki mwenzangu) anawajengea nyumba ya ibada hapo Kinondoni?

hiyo mosi.

pili, Lissu kupigwa risasi 16 ndiyo upendo wa chama chetu unaoringia?
 
Wale vijana walitumwa na Ole sabaya, mbona hawamkamati?
Kule wilaya ya Hai DC na OCD wapo kwenye List ya watu watakaopelekwa kwenye mahakama ya uhalifu wa kimataifa The Hague
 
Libya na Iraq mkuu ni tofauti na Tanzania. Hizo nchi ni waislamu na unajua wenzetu na dini yao. Sisi rais anasisitiza umoja, upendo na kuchapa kazi. Lisu na wapinzani wanasisitiza vita, wazungu na kuchukiana.
Vita inasisitizwa na CCM kwa kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani hata DC wa hai anasisitiza vita kwa kuwatuma vijana kuwarushia mawe chadema, CCM ndiyo inaivuruga Aman ya Tanzania
 
Mnachekesha, sisi ni nchi huru, tunajiamlia mambo yetu. Wazungu wajanja hapo hiyo gharama imeahidiwa kulipwa kwa mikataba minono ya upendeleo atakayo itoa lisu pindi akiwa rais (kitu ambacho hawezi kuwa rais maana watamuua akishindwa urais).

Kwani hiyo mikataba minono ya kuchimba madini sasa hivi nani ananufaika nayo na analipia fadhira gani hivi. Hao mabeberu ndo mmewasainisha mikataba minono ya kuchimba madini sehemu zote lakini sasa mnahofia Lissu mnadhania nayeye ana roho ya ufisadi kama huo wabkwenu
 

Nimecheka kwa sauti hilo dongo la mwishoni umeuwa kabisa Mkuu
 
Big respect kwako. Mwenye akili atakuelewa ila mburula wanaotaka uteuzi shauri zao. Kuna mfano mzuri wa IGP wa zamani wa Uganda Kale Kayihura, rafiki wa zamani wa Museveni ambaye yuko kizuizini kwa sasa.

Ameshtakiwa kwenye court martial ya Uganda mwaka 2018 kwa makosa ya ukatili dhidi ya wakimbizi wa Rwanda. Museveni ameamua kumshtaki kwa sheria za kijeshi kama kumsaidia baada ya ICC ya The Hague kutoa waraka wa kumtaka akakabiliane na mashtaka.

Soma zaidi hapa:
Museveni speaks out on Kayihura USA sanctions

Kwa hiyo watendaji wakumbuke kuwa hata kama Rais anakutuma ukafanye udhalimu, itakapofika wakati wa kuwajibika ni wewe ndiyo utapanda kizimbani.
 
Nimekuwa nikijiuliza kuwa hivi hiki kizazi ndio cha kupeleka nchi mbele

Mtu anaanini kuwa nchi fulani au private fulani inaweza kuitisha nchi huru nyingine?...

Hakuna nchi iliyohuru bila kuheshimu misingi ya uhuru wa watu wake kuishi nchi ikishajiingiza kwenye kuuwa raia wake tu inakuwa imepoteza huo uhuru wake ndiyo maana kuna viongozi wa nchi wamepelekwa The Hague Kwani hizo nchi zao hazikuwa huru.

Uhuru siku zote una mipaka yake huwezi kuamuwa ukawa unauwa watu na kujificha kwenye kichaka cha uhuru wa nchi utashugulikiwa na wenzako wanaoongoza nchi kama wewe.
 
Yaani hao amtardam wanaweza kupangia nchi mambo yao? Nakushangaa sana hao amstardam wana mahusiano gani na tanzania mpaka watupangie, yaani bavicha akiri zenu ni sifuli tu.
Kweli mpambe ana nguvu yaani mabosi wako wanatoa ulinzi kama walivyotakiwa na kusisitiza kushughulikiwa kwa waliofanya vurungu...ww ndo unajifanya mbabe.
 
Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa barua kutoka kampuni binafsi ya Amsterdam & Partners LLP, walioingia mkataba na mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu kumsaidia masuala yake ya kisheria, kiusalama na ulinzi wa haki zake...
Hizi ni janja janja zao.... utaskia huko bdae kama hawajazitumia hizi kauli km reference..... "changanya na zako"
 
Wakipewa maagizo wafikirie na familia zao, wanaowapa maagizo wanaweza kiwa na kinga kidogo lakini wao hawana hiyo kinga, utashtakiwa utahukumiwa utaenda jela au adhaby nyinginezo kadri ya kosa huku ukiacha familia yako ikiteseka.
 
Mkuu ebu kuwa serious kidogo basi

Angalau make your sons and daughters be proud kwa sababu yako...
Ile barua haitishia nchi. Soma tena alichoquote hapo juu. Wanataka kudeal na individuals kama individuals.
 
Hata the Hague ina utaraibu wake.

Smith wa S.A hakuwahi kufikishwa the Hague, G. Bush wa Skull & Bones hajafikishwa, Israel leader wote hawajawahi. Why Afrikan pekee ndio wanapelekwa? Jiulize. Halafu jiulize fanya utafiti wako mdogo kwa gharama zako nenda kijijini kwenu na sehemu nyingine uone kama Tz kuna kiongozi anefikia huko?

Sio mpenzi wa mauaji ya waTz wenzetu wala kubambikiana kesi lkn ijulikane kuwa Tawala zote wengine wenzetu iwe ukweli au kusingiziwa wameteswa na mamlaka zilikuwepo aidha kwa Usalama wa Taifa au Kimakosa.

Uliza habari za Ntunte. Mauaji ya waganga wa jadi kanda ya ziwa. Leo wakimbizi wa comoro
Je Mwangosi na Dr?

Sometime ni kimakosa lkn sometime kunusuru taifa.
 
Ile barua haitishia nchi. Soma tena alichoquote hapo juu. Wanataka kudeal na individuals kama individuals.
Kwani si umesema NEC na Police hizi sio Taasisi za nchi? Huenda kumbe ni individual
 
Mnachekesha, sisi ni nchi huru, tunajiamlia mambo yetu. Wazungu wajanja hapo hiyo gharama imeahidiwa kulipwa kwa mikataba minono ya upendeleo atakayo itoa lisu pindi akiwa rais (kitu ambacho hawezi kuwa rais maana watamuua akishindwa urais).
Toka lini umejiamlia mambo yako mwenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…