Polisi na NEC waanza kuhofia barua za Amsterdam & Partners LLP?

Polisi na NEC waanza kuhofia barua za Amsterdam & Partners LLP?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa barua kutoka kampuni binafsi ya Amsterdam & Partners LLP, walioingia mkataba na mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu kumsaidia masuala yake ya kisheria, kiusalama na ulinzi wa haki zake.

Moja ya sehemu ya barua yao waliyoliandikia Jeshi la polisi inasema,

"By this letter, we notify you (Tanzania Police) our intention to hold accountable all public servant of the government of Tanzania individually... " Robert Amsterdam.

Vile vile waliiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kuwa,

“It is our intent to hold the members of the NEC personally accountable”, Robert Amsterdam.

Jana Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amewataka makamanda wa jeshi hilo kuja na majibu ya nguvu kwa mikoa iliyo anza kufanya vurugu kwenye misafara ya wanasiasa ikiwemo kurusha mawe na wale waliohusika kuchoma ofisi za vyama vya siasa.

"...mtu yeyote wa ovyo ovyo atakaejihusisha na uchomaji wa ofisi au kujihusisha na vurugu tutamshughulikia vizuri" IGP Sirro.

Je, hizi zinaweza kuwa dalili kwa jeshi la polisi kuanza kubadilika au ni kwa sababu ya vitisho vya barua za Robert Amsterdam?
 
Polisi na tume kama wangeamua kutenda HAKI na kuheshimu maamuzi ya Watanzania kila kona Nchini kuhusu nani anayestahili kuwa Mbunge wa Jimbo na nani anastahili kuwa Rais wa Nchi hii barua kutoka Amsterdam Partners & LLP isingekuwa tishio kwao, lakini kwa kuwa wanajua dhambi zao tangu 1995 sasa wanaweweseka.
 
Polisi wakiongozwa na IGP na NEC wafanye kazi zao kwa usawa na haki vinginevyo wakifanya kazi ili wamfurahishe mtu mmoja nawaambia lolote baya litakalo tokea mwaka huu wao ndio watajibu na sio huyo mtu mmoja wanae taka kumfurahisha. Wanasemaga akili za kuambiwa... Kazi kwenu
 
Mnachekesha, sisi ni nchi huru, tunajiamlia mambo yetu. Wazungu wajanja hapo hiyo gharama imeahidiwa kulipwa kwa mikataba minono ya upendeleo atakayo itoa lisu pindi akiwa rais (kitu ambacho hawezi kuwa rais maana watamuua akishindwa urais).
Kuwa nchi huru hakukupi haki ya kuwafanyia vurugu wengine, huu ni utetezi wa kishamba.
 
Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa barua kutoka kampuni binafsi ya Amsterdam & Partners LLP, walioingia mkataba na mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu kumsaidia masuala yake ya kisheria, kiusalama na ulinzi wa haki zake.

Moja ya sehemu ya barua yao waliyoliandikia Jeshi la polisi inasema.

Mkuu ebu kuwa serious kidogo basi

Angalau make your sons and daughters be proud kwa sababu yako

Unaamini kabisa kwa akili zako timamu dola na nchi huru inaweza kutikisika kwa barua ya private firm? Wana nini zaidi ya kuandika tu?

Na kabisa ulichoandika hapa maadui wa Liss hawawezi kulibeba hili kisiasa? Kuwa katumwa na wazungu?

Hivi huwa mnafikiria kabla ya ku post au uhalisia ndio kweli kabisa uwezo wa fikra ulipoishia?

You are better than this
 
Huu no mtego kwa Chadema maana ndio walioigizackurushiana mawe na kuchoma polisu
Waropokaji kama wewe ndiyo mnatakiwa kukamatwa na kulisaidia jeshi la polisi kutoa ushahidi wa jinsi Chadema wanavyochoma ofisi zao.

Ifike mahali huu upumbavu wenu wa kuteka, kuua, kuharibu mali za wapinzani hasa Chadema kisha muwasingizie wao kuwa wanafanya hivyo ili kupata umaarufu maana hata viongozi wenu nao wameingia kwenye huu upumbavu.
 
Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa barua kutoka kampuni binafsi ya Amsterdam & Partners LLP, walioingia mkataba na mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu kumsaidia masuala yake ya kisheria, kiusalama na ulinzi wa haki zake.
halafu pia wamesema wata lobby US & UK kuhakikisha Tanzania inawekewa vikwazo kama Zimbabwe (huu mfano wa Zimbabwe ni wangu!)

Naiomba mamlaka na vyombo vyake vya dola isipuuze hili tishio maana mambo ya kubeba lumbesa zilizojaa noti mtu anapokwenda kununua kilo ya unga hatuko tayari kufika huko!
 
Kuwa nchi huru hakukupi haki ya kuwafanyia vurugu wengine, huu ni utetezi wa kishamba.
Tunachotaka tushindane kwa hoja za kuleta maendeleo, hatutaki kudharauliana, hata huyo Lisu anapowadhihaki polisi na TISS na jesho hivi kuna kati ya hao anaweza kukubali kuwa chini ya amri jeshi anayewadharau?

Kwa ufupi piga chinja garagaza lisu na wapinzani waliopo hakuna aliyejiweka katika nafasi ya kutawala, na unafiki huo umekuja kuonekana baada ya rais Magufuli kushika nchi kwa sababu kila ambacho hata sisi tuliona kilipaswa kufanyika Dr Magufuli kafanya ila leo wapinzani wanapinga na kuzusha uongo, wanaungana wa wezi wazungu ili kuyumbisha nchi yetu, wanakaa meza moja kupanga mbinu za kumuua rais wetu leo hii uwape nchi?

Lisu na genge lake wanajulikana kwa hizo mbinu, ndiyo maana ameachwa tu ili wammalize hao hao wazungu kwa kumtwanga risasi tena.
 
Mnachekesha, sisi ni nchi huru, tunajiamlia mambo yetu. Wazungu wajanja hapo hiyo gharama imeahidiwa kulipwa kwa mikataba minono ya upendeleo atakayo itoa lisu pindi akiwa rais (kitu ambacho hawezi kuwa rais maana watamuua akishindwa urais).
mbona hata Libya na Iraq zilikuwa zinasema hivi hivi zilipokuwa chini ya marais madikteta?

kikubwa ni haki itamalaki miongoni mwetu ili haya masahibu yasitupate.
 
Back
Top Bottom