Polisi ni janga la kitaifa

Polisi ni janga la kitaifa

Wengi huwa mnalaumu tu polisi lakini shida sio polisi, tatizo ni sheria zetu zimekaa kikoloni sana, sheria ni kali kiasi kwamba polisi wakisizimamia inaonekana wakuda ila akizipotezea kwa kupewa 2000 ndio tunalalamika. Sheria zipunguzwe makali uone kama kuna askari atapewa rushwa.
Kakaaa, barabara imewekwa taa za kuongoza magari, polisi wa nini tena kwenye taa? kwanini usiweke camera pale na kifaa cha kuandika kosa cheyewe palepale? Mtoto wangu mdogo aliyefundishwa shuleni kwako juu ya matumizi ya taa za barabarani alishangaa sana polisi kuruhusu magari yapite kwenye taa nyekundu!!! Tunawachanganya watoto wetu kile wanachofundishwa na walimu wao.
 
Ukweli askari polisi ni kero kubwa kwa wananchi. Ni kero kubwa kwa wakulima, wafugaji, wasafirishaji, wafanyabiashara na hata madereva barabarani. Kila jambo na kila kitendo wanachokifanya ni kwaajili ya kupata hela kwa njia ya rushwa au unyang'anyi kunakosababisha Wananchi wanakata tamaa ndani ya nchi yao wenyewe. Hizi mashine za kutozea watu faini wanazotembea nazo ndio silaha kubwa wanayoitumia kusumbua watu kuwabambikiza makosa watu kwa lengo la kuwafanya watu wavutike kulipa hela punguvu kuliko sh. 30,000 zinazotozwa kwakutumia vifaa hivyo vya mkononi, ni kero.

Naomba kwa kuanzia polisi wanyang'anywe hizi mashine za mkononi ambazo wanazitumia vibaya. Wanaigombanisha serikali na wananchi wake. Barabarani hawaachi pesa, wanapokea kuanzia sh. 2000 ili kusamehe tsh 30,000 za kubambikia au kosa la kweli.

Kwa wakulima na wafugaji, polisi wanashirikiliana na wakulima/wafugaji kujipatia fedha kwa makosa ya kubambikia. Huku vijijini kero ni kubwa sana kiasi cha watu kukata tamaa kwa vitendo vya polisi kwa "michongo" ya polisi kwa ushirikiano na baadhi ya wanavijiji.

Wasafirishaji wa mizigo na abiria wako hoi, vijana wanaosafirisha mizigo kwa kutumia pikipiki za magurudumu 3 wana shida sana barabarani, wanawindwa kama swala na jeshi la polisi.

Ukweli jeshi hili livunjwe ili lipangwe upya.
Sababu kuu kuliko zote ni hizi:-
Binadamu wengi kwa asili ni Wahalifu namna moja au nyingine hivyo anapokuwepo anayesimamia sheria ya kutokufanya Uhalifu kamwe hawezi Pendwa maana anakuwa amedhibiti Uhalifu.
Sasa ili kumuondoa Msimamizi wa Sheria inabidi atengenezewe tuhuma za kutosha ili naye aonekane ni Mhalifu na akiondolewa pale ansposimamia sheria Jamii ya Wahalifu hupata shangwe kweli kweli .Shida huja hapa Uhalifu unapokosa Mtu wa kuudhibiti Jamii inaanza kujidhuru yenyewe hivyo vifo,vilema na Umaskini hutamalaki.

Mfano Dar es salaam waendesha Pikipiki hawavai kofia ngumu wala abiria wao na Wanaendesha mwendo hatari na wasimamizi wa sheria hiyo wakikaza kidogo tu tuhuma zitawarudia wasimamizi wa sheria hiyo lakini ukiangalia MOI wagonjwa wengi wamesababishwa na Pikipiki.

Vijijini Waendesha Pikipiki nikiwemo na Mimi Pikipiki hazina bima , tunabeba mizigo kwa mitindo ya hatari
Hatuna leseni ,Pikipiki zetu ni Mbovu hatuzirekebishi kwa viwango vya kuwepo barabarani lakini tukikamatwa tunalalamika sana kama tumeonewa kumbe yule msimamizi wa Sheria katekeleza jukumu lake. Kuhusu rushwa siku zote tokea nianze kuona Traffic na Mapolisi wengine Sisi ndiyo tunaomba wapokee rushwa ili tusipate adhabu tunayostahili na akishakubali kupokea hiyo rushwa ili kukusaidia wewe yeye anakuwa katenda kosa la kupokea rushwa .Shida ipo kwenye kwenye Sheria Kutoa na kupokea rushwa ni kosa kisheria hivyo anayetoa na kupokea wote ni Wahalifu.kicheko ni hapa aliyetoa rushwa anaanza kulalamika kuonewa kama yeye hakutenda kosa.

Kuhusu Makosa ya Barabarani ukiona hujaridhika na fine Mwambie Officer akupeleke court ili mkabishane kwa hoja za kisheria Mahakamani.
Kitu kinachekesha ni hiki Mtu amekuandikia fine wewe ukalipe kwa kosa ambalo umetenda kakupa risiti mbaya zaidi hata ukilipa yeye hapati chochote zaidi ya Mshara wake wa kila mwezi sasa hapo yeye kakukomoa nini.

KWA UFUPI KAZI YA USIMAMIZI WA SHERIA NI NGUMU SANA HASA KWA JAMII AMBAYO HAIJASTARABIKA NA MASKINI. GARI BOVU ,HUNA LESENI ,HUJAFUNGA MKANDA ,HUJALIPA FINE ULIZOPIGWA SIKU ZA NYUMA HAYO NI MAKOSA MAARUFU BARABARANI YAANI NIMEKAMATWA MARA NYINGI SANA KWA HAYO MAKOSA NA NI KWELI NI MAKOSA NINAYOISHI NAYO KILA SIKU .
 
hiyo sio kweli, polisi wanakusimamisha saa 1 asubuhi wakati wasafirishaji, wasafiri na madereva binafsi wanawahi kazini, wanasimamisha magari 10 halafu anapitia gari mojamoja kuhoji hili na lile asuhi ile. Lakini ukimpa 2000 kosa linayeyuka. Je, sh. 5000 inayeyusha makosa ya dereva au gari? Yaani dhamira haikuwa kupunguza ajali bali kujipatia fedha binafsi. Kule kijijini mfugaji au mkulima anawekwa mahabuhusu makusudi kwa tuhuma ambayo wana uhakika kuwa ni mchongo.
Kwanini utoe hela kama hauna kosa??
 
Ndio maana wamekuja na hoja ya watu wapeleke vyeti ili kuwatambua madereva ingawaje mbinu yao ni mbovu ila wewe sio Dereva bhana...
Mimi ni dereva, nimeendesha safari fupi na ndefu, Dar- Mbeya, Dar - Dodoma, Dar - Arusha.

Kusimamishwa na jambo la kawaida na ni wajibu wa polisi kukusimamisha na kukukagua, hata kaka hauna kosa.

Wewe ukikimbilia kutoa hela ni uoga wako ndio unakuponza, kama sio hivyo basi ni kweli unamakosa na hautaki wafike mbali na maswali yao.
 
Sababu kuu kuliko zote ni hizi:-
Binadamu wengi kwa asili ni Wahalifu namna moja au nyingine hivyo anapokuwepo anayesimamia sheria ya kutokufanya Uhalifu kamwe hawezi Pendwa maana anakuwa amedhibiti Uhalifu.
Sasa ili kumuondoa Msimamizi wa Sheria inabidi atengenezewe tuhuma za kutosha ili naye aonekane ni Mhalifu na akiondolewa pale ansposimamia sheria Jamii ya Wahalifu hupata shangwe kweli kweli .Shida huja hapa Uhalifu unapokosa Mtu wa kuudhibiti Jamii inaanza kujidhuru yenyewe hivyo vifo,vilema na Umaskini hutamalaki.

Mfano Dar es salaam waendesha Pikipiki hawavai kofia ngumu wala abiria wao na Wanaendesha mwendo hatari na wasimamizi wa sheria hiyo wakikaza kidogo tu tuhuma zitawarudia wasimamizi wa sheria hiyo lakini ukiangalia MOI wagonjwa wengi wamesababishwa na Pikipiki.

Vijijini Waendesha Pikipiki nikiwemo na Mimi Pikipiki hazina bima , tunabeba mizigo kwa mitindo ya hatari
Hatuna leseni ,Pikipiki zetu ni Mbovu hatuzirekebishi kwa viwango vya kuwepo barabarani lakini tukikamatwa tunalalamika sana kama tumeonewa kumbe yule msimamizi wa Sheria katekeleza jukumu lake. Kuhusu rushwa siku zote tokea nianze kuona Traffic na Mapolisi wengine Sisi ndiyo tunaomba wapokee rushwa ili tusipate adhabu tunayostahili na akishakubali kupokea hiyo rushwa ili kukusaidia wewe yeye anakuwa katenda kosa la kupokea rushwa .Shida ipo kwenye kwenye Sheria Kutoa na kupokea rushwa ni kosa kisheria hivyo anayetoa na kupokea wote ni Wahalifu.kicheko ni hapa aliyetoa rushwa anaanza kulalamika kuonewa kama yeye hakutenda kosa.

Kuhusu Makosa ya Barabarani ukiona hujaridhika na fine Mwambie Officer akupeleke court ili mkabishane kwa hoja za kisheria Mahakamani.
Kitu kinachekesha ni hiki Mtu amekuandikia fine wewe ukalipe kwa kosa ambalo umetenda kakupa risiti mbaya zaidi hata ukilipa yeye hapati chochote zaidi ya Mshara wake wa kila mwezi sasa hapo yeye kakukomoa nini.

KWA UFUPI KAZI YA USIMAMIZI WA SHERIA NI NGUMU SANA HASA KWA JAMII AMBAYO HAIJASTARABIKA NA MASKINI. GARI BOVU ,HUNA LESENI ,HUJAFUNGA MKANDA ,HUJALIPA FINE ULIZOPIGWA SIKU ZA NYUMA HAYO NI MAKOSA MAARUFU BARABARANI YAANI NIMEKAMATWA MARA NYINGI SANA KWA HAYO MAKOSA NA NI KWELI NI MAKOSA NINAYOISHI NAYO KILA SIKU .
Kila fatiki/program ni lango la rushwa kwa Polisi. Ukisema hii ni wiki ya usalama barabarani tayari umefungua lango la rushwa, ukisema sijui Sasa tuwasake panya road tayari umeshatoa uchochoro wa kuhangaisha wananchi wema. Hebu niambie Polisi anachukua leseni yako halafu anakwenda nayo ukiwa unasubiri ahangaike na magari mengine kwanza huo ni uungwana? Kama Nina kosa SI uandike kosa na kuniachia niende zangu kuwahi kuwahudumia watanzania wengine?
 
Kwanini utoe hela kama hauna kosa??
Siku moja alisema Kwanini gari Lina vumbi sana. Hapo ni baada ya kukosa makosa . Siku moja pale tazara alimsababishia ajali mbaya mwenye pikipiki ambae hakuvaa viatu vya kuvunika, aligonga gari na pikipiki yake kuharibika na yeye kuvunja mkono. Utadhani serikali ya makaburu.
 
Trafic anakukamata harafu anakuuliza kiongozi mbona huna fine ngoja nikuandikie na wewe uchamgie kidogo. Harafu hizi rushwa za 5000 zilichagizwa nakauli za magufuli Magufuli. eti 5000 hera ya polish.
 
Kila fatiki/program ni lango la rushwa kwa Polisi. Ukisema hii ni wiki ya usalama barabarani tayari umefungua lango la rushwa, ukisema sijui Sasa tuwasake panya road tayari umeshatoa uchochoro wa kuhangaisha wananchi wema. Hebu niambie Polisi anachukua leseni yako halafu anakwenda nayo ukiwa unasubiri ahangaike na magari mengine kwanza huo ni uungwana? Kama Nina kosa SI uandike kosa na kuniachia niende zangu kuwahi kuwahudumia watanzania wengine?
Unakuwa na mashaka gani juu ya leseni wakati wao ndiyo waliokupitisha uipate?

Sheria inasema nini juu ya leseni?
wakati gani leseni itashikwa na Afisa wa Polisi na dhumuni gani ?
Ni nani mwenye Mamlaka ya kukifungia leseni ya Udereva.

Jibu la mwisho ni lile lile Jamii kubwa ni Wahalifu na kama ni wahalifu hawawezi penda mdhibiti uhalifu watakachofanya ni Kumshawishi mdhibiti Uhalifu apokee rushwa ili Wahalalishe Uhalifu wao kisha wanaanza kumlaumu Mpokea rushwa na kusahau Mtoa rushwa na Mpokea rushwa wote Wahalifu.

Usitoe rushwa mwambie huyo Polisi akupeleke Mahakamani ili upate haki yako kama amekuonea .
 
Hivi tuna waziri wa mambo ya ndani kweli? Sijawazi kusikia akiwakemea polisi. Au kuongelea utendaji wao.
 
Mimi ni dereva, nimeendesha safari fupi na ndefu, Dar- Mbeya, Dar - Dodoma, Dar - Arusha.

Kusimamishwa na jambo la kawaida na ni wajibu wa polisi kukusimamisha na kukukagua, hata kaka hauna kosa.

Wewe ukikimbilia kutoa hela ni uoga wako ndio unakuponza, kama sio hivyo basi ni kweli unamakosa na hautaki wafike mbali na maswali yao.
Sio dereva mkuu narudia tena polisi wanakera sana ndio maana wengi wanapenda kusafiri usiku mimi sio mtoa rushwa na gari nazotumia karibu vitu vyao vipo na siwaogopi Polisi...
 
Ni nadra sana kubambikia kosa barabarani. Madereva wengi wanafanya makosa na ushahidi unakuwepo.

Kama kweli umefanya kosa nakusihi kuwa mzalendo lipa hiyo 30k.

Kama hauna kosa acha aandike lakini unao uwezo wa kwenda kuipinga hiyo faini.

Utakuwa unaendesha Punda na sio gari, Dar to Morogoro - Day time, utatozwa fine or rushwa pasipo haki 100%.
 
Kuna mmoja kidogo nimlambe makofi
😂😁😅😄😃😆😀Hivi Yule Aliyemtishia Adam Malima Wa SMG Kule Masaki Yupo Wapi Sasa Hivi?
Police Wa Nape Tunasikia Ndiyo Alikuwa Anatuhumiwa Kukatisha Uhai Wa Mtu Mtwara
 
Unakuwa na mashaka gani juu ya leseni wakati wao ndiyo waliokupitisha uipate?

Sheria inasema nini juu ya leseni?
wakati gani leseni itashikwa na Afisa wa Polisi na dhumuni gani ?
Ni nani mwenye Mamlaka ya kukifungia leseni ya Udereva.

Jibu la mwisho ni lile lile Jamii kubwa ni Wahalifu na kama ni wahalifu hawawezi penda mdhibiti uhalifu watakachofanya ni Kumshawishi mdhibiti Uhalifu apokee rushwa ili Wahalalishe Uhalifu wao kisha wanaanza kumlaumu Mpokea rushwa na kusahau Mtoa rushwa na Mpokea rushwa wote Wahalifu.

Usitoe rushwa mwambie huyo Polisi akupeleke Mahakamani ili upate haki yako kama amekuonea .
Hakuna nchi ya hivyo watu kujazana mahakamani, makosa yote yanafahamika na adhabu zake. Kama amefanya kosa na adhabu IPO kwanini usiandike adhabu badala yake unaruhusu majadiliano na mkosaji? Kwanini uchukue leseni au ufunguo wa gari/pikipiki na kuondoka nao ili akufuate pembeni?

Jeshi la Polisi livunjwe ili lisukwe upya, la Sasa limekusanya askari ambao hawana wito Wala passion ya kuwa Polisi, ni watoto wa ndugu, najirani na michongo TU walioingizwa jeshi la Polisi. Na Mimi nawaambia chunguza zaidi uone trend na pattern ya askari Polisi wa usalama barabarani utagundua kitu ambacho ni common na association fulani.
 
Hivi tuna waziri wa mambo ya ndani kweli? Sijawazi kusikia akiwakemea polisi. Au kuongelea utendaji wao.
Issue ya uozo wa Polisi hata Rais Samia anafahamu kinagaubaga, alishawahi kuiongelea hadharani, kama hachukui hatua Sasa ni hiyo basi TU.
 
Utakuwa unaendesha Punda na sio gari, Dar to Morogoro - Day time, utatozwa fine or rushwa pasipo haki 100%.
Polisi hawazuii makosa bali wanatafuta makosa. Wanachukia kama hawaoni makosa. Makosa ndio mtaji wao mkuu.
 
Sababu kuu kuliko zote ni hizi:-
Binadamu wengi kwa asili ni Wahalifu namna moja au nyingine hivyo anapokuwepo anayesimamia sheria ya kutokufanya Uhalifu kamwe hawezi Pendwa maana anakuwa amedhibiti Uhalifu.
Sasa ili kumuondoa Msimamizi wa Sheria inabidi atengenezewe tuhuma za kutosha ili naye aonekane ni Mhalifu na akiondolewa pale ansposimamia sheria Jamii ya Wahalifu hupata shangwe kweli kweli .Shida huja hapa Uhalifu unapokosa Mtu wa kuudhibiti Jamii inaanza kujidhuru yenyewe hivyo vifo,vilema na Umaskini hutamalaki.

Mfano Dar es salaam waendesha Pikipiki hawavai kofia ngumu wala abiria wao na Wanaendesha mwendo hatari na wasimamizi wa sheria hiyo wakikaza kidogo tu tuhuma zitawarudia wasimamizi wa sheria hiyo lakini ukiangalia MOI wagonjwa wengi wamesababishwa na Pikipiki.

Vijijini Waendesha Pikipiki nikiwemo na Mimi Pikipiki hazina bima , tunabeba mizigo kwa mitindo ya hatari
Hatuna leseni ,Pikipiki zetu ni Mbovu hatuzirekebishi kwa viwango vya kuwepo barabarani lakini tukikamatwa tunalalamika sana kama tumeonewa kumbe yule msimamizi wa Sheria katekeleza jukumu lake. Kuhusu rushwa siku zote tokea nianze kuona Traffic na Mapolisi wengine Sisi ndiyo tunaomba wapokee rushwa ili tusipate adhabu tunayostahili na akishakubali kupokea hiyo rushwa ili kukusaidia wewe yeye anakuwa katenda kosa la kupokea rushwa .Shida ipo kwenye kwenye Sheria Kutoa na kupokea rushwa ni kosa kisheria hivyo anayetoa na kupokea wote ni Wahalifu.kicheko ni hapa aliyetoa rushwa anaanza kulalamika kuonewa kama yeye hakutenda kosa.

Kuhusu Makosa ya Barabarani ukiona hujaridhika na fine Mwambie Officer akupeleke court ili mkabishane kwa hoja za kisheria Mahakamani.
Kitu kinachekesha ni hiki Mtu amekuandikia fine wewe ukalipe kwa kosa ambalo umetenda kakupa risiti mbaya zaidi hata ukilipa yeye hapati chochote zaidi ya Mshara wake wa kila mwezi sasa hapo yeye kakukomoa nini.

KWA UFUPI KAZI YA USIMAMIZI WA SHERIA NI NGUMU SANA HASA KWA JAMII AMBAYO HAIJASTARABIKA NA MASKINI. GARI BOVU ,HUNA LESENI ,HUJAFUNGA MKANDA ,HUJALIPA FINE ULIZOPIGWA SIKU ZA NYUMA HAYO NI MAKOSA MAARUFU BARABARANI YAANI NIMEKAMATWA MARA NYINGI SANA KWA HAYO MAKOSA NA NI KWELI NI MAKOSA NINAYOISHI NAYO KILA SIKU .
Mifumo yote kwenye taifa moja ni lazima isomane, jeshi la polisi halisomani na mifumo mingine. Mfano, jeshi la polisi linaanza msako wa makosa ya magari asubuhi saa moja ili kukamata magari na madereva wenye makosa. Wanaweka camera yao barabarani ili kubaini magari ambayo hayakulipa faini zao siku zilizopita. Kwakufanya hivyo wanasababisha msongamano wa magari pale ambapo wamebinya upana wa barabara ili magari yote yapite ilipo kamera yao, lakini pia magari yatakayobainika kuwa yanadaiwa kodi yanasimamishwa yote muda huohuo hata kama yangekuwa 200 bila kujali kuwa magari hayo yamebeba abiria wangapi wanaokwenda wapi asubuhi ile. Mwisho wa siku walimu, wanafunzi, manesi, madaktari, wagonjwa, wafanyabiashara wanaowahi feri na sokoni ambao wote hawa wanachelewa kule wanakokwenda asubuhi ile. Hii ni akili ndogo sana na fupi ya utendaji ya kuchelewesha watu woooote hawa bila kuchukua tahadhali kuwa kuchelewa kwao kutazorotesha jambo huko waendako.
 
Halafu ukasahau kuwa hizo pesa wanazodaiwa kuwa zimeshaingizwa kwenye bajeti ya serikali kuu ili zikanunue dawa,kujenga shule na kuwalipia mishahara hawo Madaktari .Kila kitu kina umuhimu wake ila Usalama wetu ni Muhimu zaidi
 
Hizi si ndio zile hela walizokuwa wanaziomba wazitumie kwenye mambo yao na Rais akawakatalia? KIla tozo kuna percent yao, na hii ndio inayowasumbua wananchi. wanatumia makosa kama kitega uchumi badala ya kuzuia makosa yasitokee. Kama ukisafiri mikoani utagundua kuwa polisi wanajificha porini ili madereva watende makosa wayatumie kuvuna hela. Anakwambia gari lako lina makosa lakini wanakuachia uendelee na safari baada ya kuwalipa, je, tozo zao zinatengeneza gari? zinarekebisha matairi ambayo ni vipara? yananunua fire fighters njiani mule? yanarekebisha magurudumu ambayo ni vipara mule safarini?. Kinachotakiwa ni tozo au niwe na fire extinguisher kwaajili ya usalama wangu na gari? Wanahitaji tozo au niwe na bima ya gari iliyohai? tozo inaisaidiaje kupata bima ya gari? Kama gari isiyokuwa na bima inaendelea na safari baada ya kulipa tozo/rushwa ni upuuzi sawa na upuuzi mwingine tu.
 
Polisi ni tatizo, wanafanya kazi kama maroboti yaliyotegeshwa. Hawana takwimu zinazoonyesha kuwa pikipiki zilizobeba watu watu ndio zainapata ajali zaidi kuliko zile zilizobeba watu 2 au 1. Hata aliyebeba aboria 2 akichatoa chochote anaachowa aendelee na safari yake vilevile kulekule aendako.
 
Nilimuuliza Polisi mmoja kwanini wanachukua hata sh.2000 kwa madereva tena waziwazi? Akaniambia hadi nikakubali wachukue kidogo kidogo.

Akasema, Polisi wengi ni watoto wa maskini vijijini, watoto wa matajiri hawawi polisi. Baada ya kuwa Polisi ukoo wote unahukuru kupata mtoto wao ambao Yuko kwenye mfumo rasmi wa serikali. Lakini, mshahara ni mdogo sana kuliko wategemezi na Polisi hawezi kuiba chochote hata muda wa kwaajili ili kufanya shughuli nyingine ya pembeni ya kujiingizia kipato kama wanavyofanya waajiliwa wengine.

Anasema mshahara jana ulitosha lakini unashangaa ghafla kesho hautoshi tena baada ya vitu kupanda bei kila siku kwa mshahara uleule wa miaka 3 iliyopita. "Hakuna namna nyingine utaweza kumsaidia dada yako gharama za matibabu yake kama hujajidhalilisha kwa kujiongeza" ndio nikajua kumbe hata wao wanajua kuwa wanajidhalilisha ili ni hali TU inawabana na kuwalazimu.

Key point hapo ni kwamba halii hii ya polisi wetu Iko hata kwa waajiliwa wa aina nyingine, ila tofauti ni kwamba wao kazi Yao inaonekana zaidi kwakuwa wako barabarani na kwamba hakuna kitu hata kimoja kinachoweza kuibiwa ukiwemo muda wa mwajili.
 
Back
Top Bottom