Ukweli askari polisi ni kero kubwa kwa wananchi. Ni kero kubwa kwa wakulima, wafugaji, wasafirishaji, wafanyabiashara na hata madereva barabarani. Kila jambo na kila kitendo wanachokifanya ni kwaajili ya kupata hela kwa njia ya rushwa au unyang'anyi kunakosababisha Wananchi wanakata tamaa ndani ya nchi yao wenyewe. Hizi mashine za kutozea watu faini wanazotembea nazo ndio silaha kubwa wanayoitumia kusumbua watu kuwabambikiza makosa watu kwa lengo la kuwafanya watu wavutike kulipa hela punguvu kuliko sh. 30,000 zinazotozwa kwakutumia vifaa hivyo vya mkononi, ni kero.
Naomba kwa kuanzia polisi wanyang'anywe hizi mashine za mkononi ambazo wanazitumia vibaya. Wanaigombanisha serikali na wananchi wake. Barabarani hawaachi pesa, wanapokea kuanzia sh. 2000 ili kusamehe tsh 30,000 za kubambikia au kosa la kweli.
Kwa wakulima na wafugaji, polisi wanashirikiliana na wakulima/wafugaji kujipatia fedha kwa makosa ya kubambikia. Huku vijijini kero ni kubwa sana kiasi cha watu kukata tamaa kwa vitendo vya polisi kwa "michongo" ya polisi kwa ushirikiano na baadhi ya wanavijiji.
Wasafirishaji wa mizigo na abiria wako hoi, vijana wanaosafirisha mizigo kwa kutumia pikipiki za magurudumu 3 wana shida sana barabarani, wanawindwa kama swala na jeshi la polisi.
Ukweli jeshi hili livunjwe ili lipangwe upya.
Sababu kuu kuliko zote ni hizi:-
Binadamu wengi kwa asili ni Wahalifu namna moja au nyingine hivyo anapokuwepo anayesimamia sheria ya kutokufanya Uhalifu kamwe hawezi Pendwa maana anakuwa amedhibiti Uhalifu.
Sasa ili kumuondoa Msimamizi wa Sheria inabidi atengenezewe tuhuma za kutosha ili naye aonekane ni Mhalifu na akiondolewa pale ansposimamia sheria Jamii ya Wahalifu hupata shangwe kweli kweli .Shida huja hapa Uhalifu unapokosa Mtu wa kuudhibiti Jamii inaanza kujidhuru yenyewe hivyo vifo,vilema na Umaskini hutamalaki.
Mfano Dar es salaam waendesha Pikipiki hawavai kofia ngumu wala abiria wao na Wanaendesha mwendo hatari na wasimamizi wa sheria hiyo wakikaza kidogo tu tuhuma zitawarudia wasimamizi wa sheria hiyo lakini ukiangalia MOI wagonjwa wengi wamesababishwa na Pikipiki.
Vijijini Waendesha Pikipiki nikiwemo na Mimi Pikipiki hazina bima , tunabeba mizigo kwa mitindo ya hatari
Hatuna leseni ,Pikipiki zetu ni Mbovu hatuzirekebishi kwa viwango vya kuwepo barabarani lakini tukikamatwa tunalalamika sana kama tumeonewa kumbe yule msimamizi wa Sheria katekeleza jukumu lake. Kuhusu rushwa siku zote tokea nianze kuona Traffic na Mapolisi wengine Sisi ndiyo tunaomba wapokee rushwa ili tusipate adhabu tunayostahili na akishakubali kupokea hiyo rushwa ili kukusaidia wewe yeye anakuwa katenda kosa la kupokea rushwa .Shida ipo kwenye kwenye Sheria Kutoa na kupokea rushwa ni kosa kisheria hivyo anayetoa na kupokea wote ni Wahalifu.kicheko ni hapa aliyetoa rushwa anaanza kulalamika kuonewa kama yeye hakutenda kosa.
Kuhusu Makosa ya Barabarani ukiona hujaridhika na fine Mwambie Officer akupeleke court ili mkabishane kwa hoja za kisheria Mahakamani.
Kitu kinachekesha ni hiki Mtu amekuandikia fine wewe ukalipe kwa kosa ambalo umetenda kakupa risiti mbaya zaidi hata ukilipa yeye hapati chochote zaidi ya Mshara wake wa kila mwezi sasa hapo yeye kakukomoa nini.
KWA UFUPI KAZI YA USIMAMIZI WA SHERIA NI NGUMU SANA HASA KWA JAMII AMBAYO HAIJASTARABIKA NA MASKINI. GARI BOVU ,HUNA LESENI ,HUJAFUNGA MKANDA ,HUJALIPA FINE ULIZOPIGWA SIKU ZA NYUMA HAYO NI MAKOSA MAARUFU BARABARANI YAANI NIMEKAMATWA MARA NYINGI SANA KWA HAYO MAKOSA NA NI KWELI NI MAKOSA NINAYOISHI NAYO KILA SIKU .