GE2025 Polisi: Polepole afike Ofisi ya Mpelelezi wa Makosa ya Jinai ili kuthibitisha Tuhuma anazozitoa

GE2025 Polisi: Polepole afike Ofisi ya Mpelelezi wa Makosa ya Jinai ili kuthibitisha Tuhuma anazozitoa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mkuu umeisikiliza hiyo clip lakini?
Hajaambiwa ajisalimishe bali ameambiwa afike ili kutoa ushahidi na maelezo zaidi,

Hivyo ndivyo mimi nilivyoielewa hiyo clip.
walisu waliwezaje kuupata kwenye mtandao na wakamfungulia kesi.Yani hapo polisi uwa ni kazi ya laana .Maelezo gani wanayotaka au IT wa polisi ni wale wale wanaotumika
 
Njaa ni mbaya sana, wameshapoke kifurushi kuhakikisha wanamlaza haraka sana chadomodomo, Watanzania SPEAKER yenu inakwenda na maji...
 
Atoe ushahidi dhidi ya nani aliyefunguliwa mashtaka? Waanze kuwakamata kina Rostam ndipo Polepole aje mahakamani kutoa ushahidi.

Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA, Sura 20 R.E 2019) inawapa Polisi mamlaka ya kuchunguza tuhuma mara zinapotolewa. Wanaposema “tunamuita Polepole aje atoe ushahidi”, inamaanisha wanategemea mtoa tuhuma pekee badala ya wao wenyewe kufanya uchunguzi.

Polisi kama wanakimbia majukumu yao ya kifanya uchunguzi Kwa watuhumiwa
Hapo wanamtaka Polepole awe mtuhumiwa badala ya kuwa mtoa taarifa
 
Huyo akiingia mikononi mwa hao majambazi wanaovaa uniform watamuua siku hiyo hiyo na kwenda kumtupa mto Rufiji aliwe na mamba.
 
walisu waliwezaje kuupata kwenye mtandao na wakamfungulia kesi.Yani hapo polisi uwa ni kazi ya laana .Maelezo gani wanayotaka au IT wa polisi ni wale wale wanaotumika
Sawa kabisa. Polisi walimfikisha Lissu mahakamani kwa ushahidi wa kutoka mtandaoni. Hapo ndipo wakaanza kuwatafuta mashahidi wakati tayari wanamshikilia. Wafanye hivyo hivyo na kwa Polepole. Wawashike watuhumiwa na ndipo wamuite Polepole mahakamani kutoa ushahidi kesi ikianza. Aidha, mwanzoni mwa kesi ya Lissu, polisi walikuwa wakipigania kesi iendeshswe kwa mtandao. Vivyo hivyo kwa PolePole, wamhoji kwa mtandao atoe maelezo zaidi ya hayo aliyokwisha kuyasema kama kuna ya ziada wanayoyahitaji.
 
Hahaha bwaibwai tu..
 
​

Jeshi la Polisi limemwelekeza aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole afike katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) atoe maelezo na ushahidi kuhusiana na tuhuma ambazo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii. Jeshi hilo limesema mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo na vielelezo vitakavyothibitisha tuhuma hizo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

=================

Leo Septemba 15, 2025 Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa lilifungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma mbalimbali ambazo amekuwa akitoa Humphrey Herson Polepole toka Julai 2025.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Jeshi limesema Polepole amekuwa akitoa tuhuma hizo Tuhuma hizo kupitia mitandao ya Kijamii. Baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo/ushahidi na vilelezo vitakavyo thibitisha tuhuma hizo ili kuwezesha hatua zingine za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na ndivyo utaratibu wa kisheria ulivyo.​
​

HAHA HAH.... WATANZANIA SI WAJINGA KIASI HICHO. LABDA POLE POLE AWE MGENI NA POLICE WA NCHI HII.
 
Back
Top Bottom