GE2025 Polisi: Polepole afike Ofisi ya Mpelelezi wa Makosa ya Jinai ili kuthibitisha Tuhuma anazozitoa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mkuu haya unayoandika hapa wao hawayajui kabisa, kumbuka tuna jeshe la polisu lililojaza mambulula ambao wao wapo kwa ajili ya kupokea order kutoka kwa viongozi wao wa kisiasa tu basi.

Hao mbululas suala la kuua mtu asiyekuwa na hatia kisa tu wamepewa amri na kiongozi wa kisiasa ni kawaida kabisa.
 
Kwa hiyo kama wameshindwa kumkamata ndo itawezekana kujipeleka mwenyewe kweli..!
 
Ndio maana Lissu anapigania mabadiliko
 
Sale za jeshi la polisi ! Badala wao kuangalia hiyo zabuni na kuangalia kama kesi ilifikishwa kwa DPP ya tuhuma za angela kizigha kuhusu sale za polisi wao wanataka polepole aende hii ni maajabu mengine
 
Kudhani kwamba Watanzania wengine hawana akili ila nini huo ni umama.
 


Waanze na waliompiga risasi Lissu , mwenyewe wanaye gerezani
 
Mbona sijaskia sehemu waliyosema ajisalimishe, kaambiwa afike kutoa maelezo na ushahidi hajaambiwa ajisalimishe, kujisalmisha maana yake ni tofauti

Kwa sababu hana tuhuma ya kujibu...

Kilichotolewa ni wito tu nadhani, wanahitaji akawape madini "ushahidi"...
 

Kwamba?

"Baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo/ushahidi na vilelezo vitakavyo thibitisha tuhuma hizo ili kuwezesha hatua zingine za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na ndivyo utaratibu wa kisheria ulivyo."

Wonders shall never end!
 
Si walisema huwa hawafanyii kazi taarifa za kwenye mtandao?

Lile zuio alilotoa Msigwa jana ilikuwa ni mkwara na maandalizi ya kumpa wito.

Mimi naona kabla hawajasema aende waeleze pia kwanini siku ya kwanza alipojouzulu na kuitisha press walivamia makazi ya dada yake na kumpiga.

Pia waliotuhumiwa wote watuthubitishie wameenda kuandika maelezo kwa DCI kuanzia Abdul na wenzake.

Baada ya kumfuatilia kimya kimya kwa njia za panya sasa wamegonga mwamba ndio wameona wamuite katika njia zilizo rasmi.

No reforms no election.

Free Lissu.
 
Badala ya kumtafuta kwa kosa la kimtandao kwa kuzusha mambo na kuleta taharuki, mnatoa wito wa kuja kwamba atoe ushahidi. Mbona wengine mnawakamata na kuwashtaki huyu mnataka atoe ushahidi wa jambo gani?
 
Kwa sababu hana tuhuma ya kujibu...

Kilichotolewa ni wito tu nadhani, wanahitaji akawape madini "ushahidi"...
Anaweza kuwatumia huo ushahidi kwa email, DM, live video conversation kupitia Facebook, YouTube, instagram na twitter.

Amesema atakuwa anaongea marambili kwa wiki. Wakibisha atawaletea ushahidi usio na shaka.

Jeshi la polisi, DPP, usalama, JWTZ watege sikio mara mbili kwa wiki mitandaoni kuchukua ushahidi. Wakihitaji taarifa, ufafanuzi zaidi wamtumie DM.
 
Wanaumwa ma.vi hawa. Nani ajisalimishe?
 
Sale za jeshi la polisi ! Badala wao kuangalia hiyo zabuni na kuangalia kama kesi ilifikishwa kwa DPP ya tuhuma za angela kizigha kuhusu sale za polisi wao wanataka polepole aende hii ni maajabu mengine
Kama Mkuu wao alikutwa na B kwenye akaunti, kuna jipya gani anaweza kusema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…