mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 901
- 1,742
Aliyefukuzwa TRC apekuliwa na polisi
Summary
- Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanya upekuzi nyumbani kwa aliyekuwa Meneja
Upekuzi huo umefanyika baada ya jeshi hilo kudaiwa kumkamata juzi akiwa nyumbani kwake Goba, jijini Dar es Salaam.
Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache zimepita tangu Bodi ya Wakurugenzi ya TRC kumwandikia barua Afumwisye ya kumfukuza kazi akituhumiwa kufanya makosa kadhaa, ikiwemo kupinga tozo za miamala ya simu kwenye makundi ya kijamii.
Hata hivyo, tangu juzi Mwananchi imekuwa inawatafuta Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam bila mafanikio, kwani kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro alisema yupo nje ya ofisi.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu juzi jioni, Peter Kibatala, wakili anayemtetea Afumwisye alisema: “Wanamfanyia upekuzi nyumbani kwake Goba kisha atarudishwa Central kwa taratibu nyingine, ikiwemo kuandika maelezo.”
Kibatala alisema, kama ambavyo wamejitolea kumtetea katika rufaa yake ya kufukuzwa kazi, atafanya hivyo kwa jambo lolote litakalokuwa linamkabili mtumishi huyo wa zamani wa TRC.
Alisema juzi walikamilisha rufaa dhidi ya uamuzi wa kinidhamu wa ndani wa TRC uliosababisha mteja wake kufukuzwa kazi. Alisema licha ya muda wa kukata rufaa kuwa siku 45 tangu alipopokea barua, wamekata mapema na kumpelekea nakala mkurugenzi mkuu wa TRC ambaye ndiye alisaini ile barua ya kumfukuza kazi.”
Wakati Kibatala akieleza hayo, jana Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kupitia taarifa yake kwa umma kilibainisha kuwa kinafuatilia kwa ukaribu taarifa za kukamatwa kwa Afumwisye.
View attachment 2338099