Polisi Tanzania nipeni 'Rukhsa' ya 'Kuwashikisha' Adabu Wanaume 'Dhaifu' na 'Wazembe' kama hawa kwani Wanatutia mno Aibu

Mkuuu...jamani mkiona mnashindwana Muachane kwa Amani... Mwanamke kuwa na mauzi mpaka ukamkata mkono...hayo mauzi yanaondoka na huo mkono?

Je wanaume Kufanya Kama hayo...nao wakatwe mikono...tuseme wanaume wana mauzi ?..

Hakuna hoja ya kutetea huu upuuzi
 

Umesema Ukweli mtupu Mkuu na hongera sana tu. Bado nawahusia 'Madume' wenzangu Dawa ya Kuachana na 'Wivu' ni kuwa na 'Mademu' kibao.
 
Kila Siku nawaambieni hapa 'tuigeni' Sisi wenye 'Mahawara' kila eneo huwezi kutukuta na 'Mawivu' haya ya 'Kipumbavu' kwani tumejitosheleza nao.
Mkuu, yote yale yale kuwa na wivu au mahawara vina nafasi sawa ya kuweza kusababisha ugomvi, majeraha na hata kifo. Hili unalosema limetokana na wivu lakini yapo mengi huko nyuma yaliyotokana na kuwa na mahawara, mfano mahawara kugombana wenyewe kwa wenyewe, n. k
 
Mapenzi ni upofu
 
Mkuu hatutetei maovu ila swala lakumdhuru mtu huwa linakuja automatically kutokana na malimbikizo ya chuki kwa muda mrefu. Ko unajikuta ushafanya tu afu ndo unaanza kujuta. Ukiwa mkubwa utanielewa zaidi. Usitukane mamba hujavuka mto..haya majumba yana mengi sana jaman
 
Sawa...Mkuu nikiwa mkuubwa sitaki kudhuru Watu Kisha kujutia. Mungu anijaalie Busara na hekima kwenye kuyaendea mambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…