Polisi Tanzania wanadai Waandamanaji sasa Wanapanga kuua Viongozi, wameshaanza kuwakamata

Polisi Tanzania wanadai Waandamanaji sasa Wanapanga kuua Viongozi, wameshaanza kuwakamata

Sasa Waandamanaji wamegeuka wauaji hata kabla ya maandamano. Kwamba Jeshi limeshaanza kuwakamata Wanaofanya mipango hiyo ya kuua Viongozi wa Serikali.
Polisi wanatoa wazo na ushauri kwa waandamanaji - kwamba badala ya kuandamana na kupambana na sisi Polisi kwa amri toka juu ya kuwaua, kwanini msiwaue viongozi wanaoharibu nchi na kutuambia tuwaue?

NI wazo la kutafakari. Asanteni sana Polisi kwa uzalendo wenu
 
Kama mwaipopo na kundi lake hawamo kwenye hiyo list ya walio kamatwa, basi hiyo operation ya ukamataji ni batili.
 
Sasa Waandamanaji wamegeuka wauaji hata kabla ya maandamano. Kwamba Jeshi limeshaanza kuwakamata Wanaofanya mipango hiyo ya kuua Viongozi wa Serikali.

Jeshi la Polisi Tanzania limesema linaendelea kufuatilia kwa karibu viashiria vya baadhi ya watu wanaodaiwa kuhamasisha vurugu na kupanga kufanya maandamano yasiyofuata taratibu za kisheria na kiusalama.

Ili kukomesha suala hilo, tayari limekamata baadhi ya watu kwa ajili ya uchunguzi, bila kuweka bayana idadi yao.

Hayo yamesemwa leo, Jumapili, Julai 5, 2026, na Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime, alipozungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba, jijini Dar es Salaam.

======

View attachment 3623190View attachment 3623191
Jeshi la Polisi Tanzania limebaini viashiria vya ‘watu wachache’ wanaotaka kuvuruga amani kwa kisingizio cha kufanya maandamano yasiyofuata taratibu za kisheria na kiusalama huku baadhi ya watu wanaohusika na uhamasishaji wa vurugu wakikamatwa na uchunguzi ukiendelea ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Jumapili Julai 05, 2026, Msemaji wa Jeshi hilo, DCP David Misime amesema kuwa kupitia ufuatiliaji wa mitandao ya kijamii na klabu za majadiliano, polisi wamebaini mipango ya watu hao inayolenga kuua baadhi ya viongozi na wananchi, kuchoma moto shule ili kusababisha taharuki kwa wazazi na walezi, kufanya uharibifu na uporaji wa mali za umma na binafsi, na kushambulia askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa lengo la kupora silaha

Kutokana na hilo, Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa mtu au kikundi chochote kisidhubutu kushiriki katika uhalifu huo, likisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa sharia.

Polisi wamewahakikishia wananchi kuwa ulinzi umeimarishwa nchi nzima kuelekea tarehe 7 Julai ili kuruhusu sherehe za Saba Saba na Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa kufanyika kwa amani.
Shekhe mwaipopo?
Mbwa mwitu??
 
Kuna habari hapa ilitoka sijajua ni nani ila alitoa tahadhari kwa viongozi wa chadema na watu wenye mapenzi na nchi wawe makini wanaweza kuvamiwa na vikundi vyenye ofisi za polisi.
Ila ile mada inageuzwa kuwa wao ndio wameonaView attachment 3623563
Polisi wanaajiriwa kwa urefu wao? Na mbio siyo akili Wala weledi
 
Ila polisi saivi wanaishi kwa mashaka sana yaani yaani polisi hata akitembea usiku hajiamini anahisi muda wowote atashambuliwa
 
Back
Top Bottom