Polisi Trafiki komesheni ajali za wakimbia kwa miguu barabarani

Polisi Trafiki komesheni ajali za wakimbia kwa miguu barabarani

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
24,523
Reaction score
30,084
Polisi Trafiki waelimisheni wanaokimbia au kutembea kwa miguu barabarani watumie upande wa kulia ambao wanatazamana na vyombo vya moto vinavyokuja upande wao.

Mara nyingi zimetokea ajali za watembea au wakimbia kwa miguu kugongwa na vyombo vya moto vinavyokuja nyuma yao kutokana na kutoviona.
 
Hii ni kweli kabisa ila ni vema nasi pia tuwe tunakumbushana
Na kama inawezekana basi jitahidi sana ufanye mazoezi uwanjani au gym ikishindikana basi kimbia kama mada inavyosema
Haya mazoezi ya Joging'i hufanywa na makundi makubwa yakiwemo yale ya kuchangia kitu fulani ambayo wakati mwingine husimamiwa na trafiki ambao sijui inakuwaje nao hawajui kanuni ya usalama kwa watembea kwa miguu barabarani! Kanuni huwataka watembea kwa miguu watumie upande wa kulia ambao huwawezesha kuviona vyombo vya moto vinavyokuja mbele yao.
Kwa kifupi inaelekea trafiki nao hawaujui utaratibu huu wa usalama barabarani, ni juzi tu huko Morogoro walijeruhiwa watu sita hivi kutokana na kukimbia barabarani wakiwa upande wa kushoto wa barabara.
 
Jamani kusema kweli mimi siwaelewi kabisa hawa watu wanaofanya mazoezi barabarani.
Kama mimi ninapoishi viwanja vipo ila unaweza ona mtu tena unamfahamu anakimbia barabarani.
Mimi kawaida yangu nakimbia uwanjani nasubiri madogo wamemaliza kucheza zao mpira napiga rounding zangu 10 nakuwa nipo fresh
Kukimbia barabarani hapana kwa kweli kwanza kuna moshi wa magari, unaweza kugongwa na magari hatari ni nyingi kwa kweli
 
Pamoja na kwamba ni kweli ILA nafikiri hili jukumu linatuhusu wote na sio kazi ya Polisi pekee.
Tungehimizana tu watu wajue upande sahihi wa kukimbilia; Sijui kama hilo nalo linahitaji watu wapelekwe vyuoni kusomea? Unajua tukijifanya kila kitu ni jukumu la watu flani hata yale yanayotaka watu watumie akili zao hatutafika...
 
Pamoja na kwamba ni kweli ILA nafikiri hili jukumu linatuhusu wote na sio kazi ya Polisi pekee.
Tungehimizana tu watu wajue upande sahihi wa kukimbilia; Sijui kama hilo nalo linahitaji watu wapelekwe vyuoni? Unajua tukijifanya kila kitu ni jukumu la watu flani hata yale yanayotaka watu watumie akili zao hatutafika...
Umesema point konki sana hii.

Kuna watu hupenda kufanyiwa kila kitu, hata wakirahisishiwa kwa kufanyiwa, hutaka watafuniwe kabisa.

na wakishatafuniwa hutaka pia wemezewe na wakishamezewa wao hupenda kushiba tu na wakishashiba na kama mfumo wa kimaumbile ungeliruhusu, basi hata kwenda kujisaidia wangeliwatuma watu wakawanyee!
 
Naona zile marasoni za kujiunga kutafuta mbususu zimepoteza mzuka siku hizi….
 
Jamani kusema kweli mimi siwaelewi kabisa hawa watu wanaofanya mazoezi barabarani.
Kama mimi ninapoishi viwanja vipo ila unaweza ona mtu tena unamfahamu anakimbia barabarani.
Mimi kawaida yangu nakimbia uwanjani nasubiri madogo wamemaliza kucheza zao mpira napiga rounding zangu 10 nakuwa nipo fresh
Kukimbia barabarani hapana kwa kweli kwanza kuna moshi wa magari, unaweza kugongwa na magari hatari ni nyingi kwa kweli
Kukimbia barabarani kuna raha yake,ni tofauti na kukimbia uwanjani ambapo unazunguka mahali hapohapo.Kuhimizana tu inatakiwa kukimbia upande magari yanapokujia kwani hata likizidi kuja kwako unaweza kukwepa.Pia ni vizuri kukimbia muda ambao magari sio mengi,mfano asubuhi sana,siku za sikukuu,jumamosi asubuhi n.k.
 
Nilisikitika kumuona mtu kavaa headphone kubwa huku akikimbia uelekeo sawa na magari yani hata akipigiwa honi hawezi sikia
 
Back
Top Bottom