Polisi: Tumemkamata mfanyabiashara Niffer kwa kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu

Polisi: Tumemkamata mfanyabiashara Niffer kwa kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Baada ya kusambaa mitandaoni kwa taarifa za Mfanyabiashara Niffer kutekwa na Watu wasiojulikana leo Dukani kwake maeneo ya Sinza Kumekucha Jijini Dar es salaam, Ayo Tv imelitafuta Jeshi la Polisi ili kupata uthibitisho wa taarifa hizo zilizosambaa mitandaoni.

Soma Pia: Faiza Ally: Niffer amepigwa sana na amechukuliwa na watu wasiojulikana

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro ameithibitishia Ayo Tv kuwa Jeshi la Polisi ndilo lililohusika kumkamata Mfanyabiashara huyo huku akisisitiza yafuatayo ———> “Polisi wamemkamata wala sio Watu, sema Polisi wamemkamata mi ndio nakwambia” < ——— amesisitiza Kamanda Muliro.
=================
“Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tarehe 27,10.2025 majira ya saa 9 mchana eneo la Sinza Kumekucha limemkamata na linamuhoji Jenifer Bilikwiza Jovin miaka 26 mkazi Masaki Peninsula Kinondoni kwa tuhuma za kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu katika maeneo mbalimbali jijini hasa siku za kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025”, imesomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Polisi wamesema kuwa hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuzingatiwa dhidi ya mtuhumiwa huyo wakati uchunguzi ukiendelea.
Screenshot_20251027-190930.png

Chanzo: Ayo Tv
Screenshot 2025-10-27 201420.png
 
Siku moja kabla nilimpa onyo post yake ingeathir biashara yake mimi mwenye napost kwa machale nisije kuambiwa leta dawa sehem wanidake


Nataman nipost vikos vya wananch vilivyoandaliwa lakin naogopa maana kuna kikos cha mawe kikos cha mishale kikos cha mabomu ya petroli kikos cha misumali na mbao barabrani
 
Niffer arudishe pesa Za watu alizowatapeli mtandaoni na kile kibwana chake!! Wamewalipisha watu iPhone na simu mbalimbali hadi Leo hawakupokea chochote!! Polisi shikilieni hapo hapo atapike hela Za watu.
Mbona taarifa ya polisi haisemi UTAPELI, WIZI WA KUAMINIKA, wala nini zaidi ya kuvuruga amani?
 
Huyu niffer ndiye aliyechangisha pesa wakati wa ajali ya ghorofa la Kariakoo au?
 
Huyu Mafwele ni Binadamu kweli?
Huyu jamaa ataishia kubaya sana.Kuna watu hawajifunzi kutokana na historia, wakina Idd Amini na ubabe wao, waliishia kufia uhamishoni kwa aibu.Halafu et wanasema ni mzee wa kanisa, haya makanisa yanajielewa kweli - tuhuma dhidi yake ni nyingi na nzito.Kama yasemwayo juu yake yana ukweli...huyu ni motoni tu...hata atubu vipi hamna kitu hapo - Lucifer atakuwa anamsubiri kwa hamu
 
Sasa hivi hawagopi wala hawajifichi...imekuwa wazi sasa kwamba the unknown ndio wao.
Anasisitiza kabisa sema Polisi maana kashajua wameshajulikana kua wao ndio wanaofanya maana ni yeye aliesema "hakuna anaekufa mara mbili"
 
Back
Top Bottom