Polisi, Uhamiaji na Wanausalama wengine Tizameni hili kwa jicho la Tai

Polisi, Uhamiaji na Wanausalama wengine Tizameni hili kwa jicho la Tai

Likitokea Shambulio la kigaidi kama la chuo kikuu cha Garisa(ten years ago)tutaacha mzaha
Nakumbuka lile shambulio lilivyotokea tulikuwa chuo,

Hahah ukaguzi uchwara ulianza, mara kuvaa I'd mara kuchekiwa gettini but havikudumu hata mwezi
 
Na kuongezea serikali inabidi imulike mpaka wa kenya na Tza kwa jicho la 3 kama inataka kutokomeza wimbi la wahamiaji haramu kutoka Ethiopia.
Hii ya mpaka wa Kenya ni biashara ya nani?
 
Watu wengi wanao jiita waha mkoa wa kigoma na wengine wametapakaa nchii nzima wengi wao ni warundi na wanyarwanda, wanaingia kama wafanyakazi mashambani wanafanya mipango wanapata vitambulisho vya kupigia kula na vitambulisho vya nida tayali waanza kujiita waha na wengine wanatoroka tuu kwenye kambi za wakimbizi

kibaya zaidi sio kwamba wenye mamlaka hawaoni wala kujua lakini wanaiweka nnchi hatarini kwa vihela vichache vya rushwa, Mkuu wa majeshi alionya tena mbele ya bibi chaudele lakini hakuna hatua yoyote iliyo chukuliwa kukomesha hilo, usione kagame anatuletea dharau ukamuona mjinga amesha otesha watu wake humu hatuko salama kabisa
 
Roho mbaya tu hizo kwani wakivuka huku utapungukiwa nini? Mbona waarabu wanashikilia bandari kuu ya Taifa na hujui hapo wanavusha nini, yani unamnyima mtu kutoka rwanda na burundi kuja kujitafutia? Hiyo ni chuki mbona wazanzibar wanashika utawala nchi nzima na hamuongei kijana acha unafiki warwanda na waburundi waachwe wajitafutie
 
Yule mwanamke mliyempa Idara ya UHAMIAJI siku akibadilishwa Nchi itakuwa siriaz kwenye kudhibiti uhamiaji haramu.
 
Roho mbaya tu hizo kwani wakivuka huku utapungukiwa nini? Mbona waarabu wanashikilia bandari kuu ya Taifa na hujui hapo wanavusha nini, yani unamnyima mtu kutoka rwanda na burundi kuja kujitafutia? Hiyo ni chuki mbona wazanzibar wanashika utawala nchi nzima na hamuongei kijana acha unafiki warwanda na waburundi waachwe wajitafutie
Acha bangi Wee mhutu. Zingatia paragraph ya mwisho la dokezo langu.
 
Mpaka Sasa Kigoma Ndiyo Maana Kuna Changamoto Zisizoisha Na Upande Wa Vitambulisho Wanazuiwa Kupatiwa NIDA Ukiwapa Unajikuta Burundi, Congo, Rwanda Umewapa Pia


Jiwe Alipokwenda Mishamo Aliwaambia Uraia Hamtapata, Silaha Mlizoficha Zisalimisheni Haraka, Vinginevyo Mwafaa
 
Mipaka ya kikoloni tu Rwanda na Burundi na watz ni watu wale wale
 
Unapoteza muda wako kwa serikali hii ya mama mitano tena? Hao ambao rushwa ukora na uzandiki ndo vipaumbele vyao?

Acha niishie hapo 😌😌
 
Mimi ni mtoa huduma kwa wakimbizi kutoka katika shirika la madakatari wasio na mipaka la MSF.

Mara nyingi nimeshuhudia wakimbizi wasio na vibali vya kutoka nje ya kambi wakisafiri kutoka kambi la Nduta kwenda Kasulu na baadaye Kigoma manispaa. Njiani Kuna vituo vya ukaguzi lakini wakati mwingine watu hao hufanikiwa kuvuka vizuizi na kufika mjini salama.

Nimefanikiwa kufuatilia na nikagundua

Wakimbizi kutoka kambi laNduta, Warundi na Wanyarwanda kutoka nchini kwao huingia katika manispaa ya Kigoma kupitia njia zisizo rasmi.


Katika usafiri wa treni ya Kigoma - Dar, uongozi hukagua vitambulisho kwa abiria.

Hapa watakagua kadi ya NIDA, mpigakura, Passport, Leseni ya Udereva na asiye na vitambulisho hivyo atapaswa kuonyesha BARUA YA UTAMBULISHO KUTOKA SERIKALI YA KIJIJI ALIKOTOKA.

Lakini,

Kuna Wenyeviti na watendaji wa vijiji wanaoshindwa kutofautisha Raia wa Tanzania na wa nchi za Kigeni. Pia Kuna Wenyeviti na watendaji wa vijiji wasio waaminifu ambao kwa kufahamu kabisa hupewa "Chai" na raia wa Kigeni ili kuwaandalia badua zenye mihuri ya vijiji husika ili kuwawezesha watu hao kusafiri kwa Treni hivyo watafanikiwa kufika mikoa mbalimbali nchini kwa madhumuni yasiyofahamika.

Ikumbukwe,

Nchi za Congo DR, Burundi Rwanda, Uganda na Kenya, kwa muda mrefu zimekuwa zikipambana na matishio ya ugaidi wa ADF, Al Shabaab na makundi mengine hatari.

Huwa najiuliza,

Itakuwaje kama wahamiaji hao ni Sehemu ya makundi hayo na ni mpango wao wa ku_infiltrate katika jamii za Watanzania ili baadaye waanze kutishia Usalama?
Watu wapo busy na uchawa hawawezi lifatilia hilo..
 
Back
Top Bottom