Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Unaposema huku kuna mashetani nashindwa kujua kama upo sahihi. Hivi chanzo cha hayo maandamano na machafuko ni nini kama sio huohuo ushetani wa hao polisi unaotaka kuwasifia? Halafu kumbuka hao polisi wa Marekani hawajafanya tukio moja tu la wiki iliyopita, wamefanya matukio mengi sana yanayowaumiza watu weusi. Unaweza pia kurejea kauli za Rais Trump kwenye vifo vya Corona jinsi zinavyoonyesha ubaguzi waziwazi.
Hayo yaliyofanywa na hao polisi huko US hata huku yanafanywa sana na polisi wa huku. Utofauti uliopo kati ya polisi wa huko na hawa wa huku, ni uungwana wa kuomba msamaha.