Polisi wa Tanzania ni wazuri sana! Elezea kwa mifano

Polisi wa Tanzania ni wazuri sana! Elezea kwa mifano

Pole sana mkuu!

Lakini nikiomba tuyaeleze mazuri yao tu. Madhaifu yanafahamika, lakini ni wachache wanaomfahamu mazuri ya hao makamanda
Wako wengi wanaofanya kazi nzuri sana. Tusiache kutambua jitihada zao kwa sababu ya wachache wao.

Polisi mmoja kufanya uovu si Polisi wote wamefanya hivyo. Usilitupe tenga zima la samaki kwa sababu ya samaki mmoja aliyeoza.
Mmoja akioza wote wameoza hawafai hata kidogo hao watu hawana ubinadam.
Mimi sioni jema hata moja kwa hao viumbe.
 
Ni pale aliponiambia" My friend,you are not my friend" pale nilipotaka tuyamalize nje ya kituo.

Nikajua polisi waaminifu wapo bado.
 
Kama 20% ni waungwana; akikukuta na kosa ana kuelimisha na Kukushauri cha kufanya. Ukikutana na mtu wa hivi lazima ujitahidi asikukamate na hilo kosa tena
 
Comment ya 52 na bado hakuja ushuhuda wa mazuri ya polisi
 
Ukijiona wewe ni nunda ,msomi,mjuaji na mwenye dharau utakutana na wenye kukuzidi ulichonacho..
Kwa ufupi hata ushirikina hauna nafasi.....
 
Ni wakamilifu? Sijasema hivyo.

Isitoshe, hakuna taasisi ya kibinadamu iliyo kamilifu!

Pamoja na madhaifu yao, wana mengi sana mazuri. Shrikisha🙏

Usiandike madhaifu, bali mema tu. Elezea matukio yaliyowahi kufanywa na Polisi wa Tanzania, iwe ulishuhudia au umesimuliwa na mtu mwingine, ambayo ni mojawapo ya kazi za Jeshi la Poklisi. Cha msingi, uwe umejieridhisha kuwa ni "ushuhuda" wa kweli.

Naamini humu JF kuna maofisa wa Jeshi la Polisi.

Karibu kwa michango itakayowatia moyo🙏
A good Police Officer is ONLY the dead Police Officer!
 
Back
Top Bottom