Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

Nashauri DP World waje kufundisha polisi wa bandarini, maana Polisi Dubai wanaenda na wakati:

CNN: Hakuna mahali pengine duniani unaweza kusifu gari la polisi na kupiga selfie na dereva. Hakuna mahali pengine duniani ni kwamba gari la polisi linaweza kuwa Bugatti Veyron, Ferrarri FF au Lamborghini Aventador.

Hii ni Dubai, ambapo jeshi la polisi limekabidhiwa cheti na Guinness World Records kwa kuwa na gari la polisi lenye kasi zaidi duniani - Bugatti Veyron -


View attachment 2701204


Kinara ya gari hizo ni Veyron, lina kasi ya juu ya 253 mph (407 km / h).

Watoto wa kitajiri walikuwa wanachezea sna polisi, Mfalme wao akasema upuuzi huu, wasicheze tena na polisi, akwashushia vitu vya uhakika, waekoma ubishi.

Siyo kwetu hapa, polisi ukiwapigia simu wanakuuliza pesa ya mafuta!

Chanzo: CNN
BILA YESU YOTE NI BURE!
 
Polisi..

Polisi wanatumiwa na wanasiasa viongozi.
Kama jana alipitisha jambo la mkubwa, leo haoni aibu kuchukua rushwa.
Kama jana alimsaidia mjumbe kushinda,leo hashindwi kumuangamiza mshindwa.
POLISI WAKIWA HURU BILA USHAWISHI WA KISIASA, WANAFANYA MAZURI SANA.
 
Kilichoharibu ni siasa, siasa ilipoingia huko basi mfumo mzima umekua kijanja kijanja.
Ukiwa na kesi huko basi uwe mjanja mjanja na kujuana na wenye vyeo la sivyo utapewa hata kesi ya kubaka.
 
Polisi wa Tanzania:

Mabaya yao:

Rushwa na ufisadi: Kama ilivyo katika nchi nyingine, polisi wa Tanzania wamekabiliwa na mashtaka ya rushwa na ufisadi. Hii imeathiri ufanisi wa jeshi hilo na kusababisha kupoteza imani kwa baadhi ya wananchi.

Matumizi mabaya ya nguvu: Kuna malalamiko ya mara kwa mara kuhusu matumizi mabaya ya nguvu na unyanyasaji kutoka kwa polisi. Kesi za ukatili wa polisi dhidi ya raia zimekuwa zikiripotiwa, na hii inaleta wasiwasi juu ya haki za binadamu na utawala wa sheria.

Uhaba wa rasilimali na mafunzo: Polisi wa Tanzania mara nyingi wanakabiliwa na changamoto za uhaba wa rasilimali na mafunzo ya kutosha, ambayo inaweza kuathiri utendaji wao katika kushughulikia uhalifu na kuwalinda wananchi.

Mazuri yao:

Ulinzi wa umma: Licha ya changamoto zinazokabiliwa na polisi wa Tanzania, wao bado wanafanya juhudi za kulinda umma na kudumisha usalama na amani ndani ya nchi.

Kukabiliana na uhalifu: Kuna maafisa wa polisi wanaojitahidi kikamilifu kukabiliana na uhalifu na kuhakikisha kuwa wahalifu wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ulinzi wa mipaka: Polisi wa Tanzania wanashiriki katika kudhibiti usalama wa mipaka ya nchi na kuzuia uingiaji wa wahalifu na vitisho kutoka nje.

Kuhusu polisi binafsi:

Kuwa na polisi binafsi kunaweza kuwa na faida na hasara, na inategemea muktadha wa nchi na mahitaji ya usalama. Hapa kuna faida na hasara kadhaa za kuwa na polisi binafsi:

Faida:

Kutoa huduma za usalama maalum: Polisi binafsi wanaweza kutoa huduma za usalama zilizobinafsishwa na za kipekee kwa makampuni, taasisi, au watu binafsi, ambazo hazipatikani kwa kawaida kutoka kwa polisi wa umma.

Kupunguza mzigo kwa polisi wa umma: Kwa kuwa polisi binafsi wanasimamia usalama wa maeneo maalum, hii inaweza kusaidia kupunguza mzigo kwa polisi wa umma na kuwaruhusu kuzingatia majukumu muhimu zaidi.

Hasara:

Hatari ya utumiaji mbaya: Polisi binafsi wanaweza kutumiwa vibaya na watu au mashirika yenye maslahi maalum, ambayo inaweza kusababisha unyanyasaji wa haki za binadamu au matumizi mabaya ya nguvu.

Utoaji wa huduma zisizo sawa: Kuwa na polisi binafsi kunaweza kuongeza tofauti za kiuchumi na kijamii, kwani wale wenye uwezo wa kulipa huduma hizi watapata usalama bora kuliko wale wasioweza kumudu.

Upungufu wa udhibiti: Mara nyingi, polisi binafsi hawasimamiwi kwa ukali kama polisi wa umma, na hii inaweza kusababisha matumizi mabaya au kukiukwa kwa sheria na taratibu za kazi.

Kwa kuzingatia muktadha huu, kuna umuhimu wa kuwa na polisi binafsi katika maeneo maalum kama vile usalama wa kampuni au taasisi, lakini lazima kanuni na udhibiti thabiti ziwekwe ili kuzuia matumizi mabaya ya nguvu au ukiukwaji wa haki za binadamu. Polisi binafsi hawapaswi kamwe kuchukua nafasi ya polisi wa umma katika jukumu la kudumisha amani na utulivu wa kitaifa.
 
Nashauri DP World waje kufundisha polisi wa bandarini, maana Polisi Dubai wanaenda na wakati:

CNN: Hakuna mahali pengine duniani unaweza kusifu gari la polisi na kupiga selfie na dereva. Hakuna mahali pengine duniani ni kwamba gari la polisi linaweza kuwa Bugatti Veyron, Ferrarri FF au Lamborghini Aventador.

Hii ni Dubai, ambapo jeshi la polisi limekabidhiwa cheti na Guinness World Records kwa kuwa na gari la polisi lenye kasi zaidi duniani - Bugatti Veyron -


View attachment 2701204


Kinara ya gari hizo ni Veyron, lina kasi ya juu ya 253 mph (407 km / h).

Watoto wa kitajiri walikuwa wanachezea sna polisi, Mfalme wao akasema upuuzi huu, wasicheze tena na polisi, akwashushia vitu vya uhakika, waekoma ubishi.

Siyo kwetu hapa, polisi ukiwapigia simu wanakuuliza pesa ya mafuta!

Chanzo: CNN
Polisi huko dubai hawan njaa

Wanalipwa vizuri wana maisha mazuri pia...haya sasa wa,huku kwetu je

Ova
 
Polisi huko dubai hawan njaa

Wanalipwa vizuri wana maisha mazuri pia...haya sasa wa,huku kwetu je

Ova
Sio hivyo mkuu,its not about money ni DISPLINE, traffic officer's wa Botswana rushwa it's almost ni zero, ni kuwawekea msingi mzuri wa kufuata sheria, ndio maana kwangu ningelivunja jeshi hili la polisi na kuanza upya, above 40yrs fukuza wote, nitaajiri vijana under 30yrs walio graduates
 
Polisi Binafsi watafanya recruitment kutoka wapi ? Kama Kumeoza kwenye Bahari unategemea ukichota maji kwenye ndoo yatakuwa pure ?

Ulizia sehemu kama USA ambapo hadi Mahakama imebinafsishwa; ni mwendo wa kushika watu na kuwapeleka ndani ili wa-justify pesa wanazolipwa kwamba zimefanya kazi....

Yule mtu wa South Africa aliyetoroka that was a Private Security kwenye hilo Gereza...;

Nadhani watu hatujui why we even Privatize....
 
Polisi huko dubai hawan njaa

Wanalipwa vizuri wana maisha mazuri pia...haya sasa wa,huku kwetu je

Ova
Tulidhani TRA wakiongezewa pesa wataacha kula mlungula...; (lakini ni yaleyale) mwisho wa siku ni vema kila mtu apate ujira unaotosha..., lakini baada ya hapo ni Utamaduni.., Siku hizi wizi umekuwa sifa na kutoa bakshishi / takrima ni kama wajibu (Hayo mambo yalikuwa huko nchi za Asia) Zamani mzee wako akiiba serikalini aibu kwa ukoo mzima; siku hizi ndio ujanja..., In short tuna Utamaduni wa Kipuuzi sana siku hizi; Na hii sumu kutoka itachukua muda.....
 
Polisi wa tanzania tumesoma na kusikia malalamiko mengi sana juu yao, mpaka inakuwa vigumu kuanza kutafuta mema yao.

Tunaona kuwa Polisi ndiyo wamekuwa chimbuko la rushwa, imefikia mpaka kuna msemo mitaani "kuingia kwa pesa, kutoka kwa pesa"

katika mema yao machache ni pale tunapoona kwenye vyombo vya habari wakijitangaza wao wenyewe kukamata majambazi na wezi, au, wameuwa jambazi fulani.

Nakumbuka sisi tulivyokuwa utotoni, miaka ya mwanzo 60s, tulibahatika kuliona jeshi la Polisi lililosheheni Wazungu, Wahindi, Waarabu na Waafrika. Na kila mtoto alitamani akikuwa awe polisi.

Polisi kilikuwa siyo chombo cha kutishia watoto, kila mtoto akipenda na kutamani awe polisi au kama polisi. Hivi sasa polisi imekuwa chombo cha kutishia watoto, ukimwambia mtoto "polisi huyo" basi mtoto anaweza kukulilia utafikiri kamuona ziraili mtowa roho za watu.

Tumefeli wapi na jeshi letu la Polisi?


Mtazamo wangu; Jeshi la polisi lilianza kufeli zamani sana, lilianza kufeli lilipoanza kutumiwa na wanasiasa kukandamiza wananchi wafanye watakavyo wao kwa nguvu au kwa hiyari. Chanzo nnachokikumbuka mimi ni vijiji vya ujamaa, watu walipoanzwa kuhamishwa makazi yao ya asili na kupelekwa vijiji vya ujamaa, jeshi la polisi likaanza kutumika kuwahamisha watu kwa nguvu na kuwapakia kwenye "makarandinga" kuwahamisha kutoka makazi yao ya asili na kwenda kuwatupa maporini waanzishe makazi mapya yaliyoitwa "vijiji vya ujamaa".

Kuanzia kipindi hicho serikali zote, mpaka leo hii, hazijaacha kuitumia polisi kama chombo chao cha kuhakikisha walitakalo wanasiasa ndilo wanalifanya polisi.

Tatizo liko wapi? Jee ni wakati siasa zikaachanishwa na kuendesha serikali? Serikali ibaki kama serikali na siasa zibaki kama siasa?

kinachotakiwa ni tafakuri ya kina, maji yakimwagika hayazoleki, lakini tunaweza kupiga deki na kuyakausha na kuchota mengine.

Wewe unaonaje? Umefikia wakati tuwe na Polisi binafsi?

Uzi mzuri ila wewe kuwepo 1960’s uongo[mention]FaizaFoxy [/mention]
 
Uzuri wa polisi wananjaa sana sana, hii ni fursa kubwa kwa wale watu wa deal chafu kufanya shughuli zao bila shida.

Polisi akiona laki anatetemeka keshawaza konyagi kubwa.
Unategemea nini ukiwa na RPC kama MURILO? Unampelekea taarifa juu ya wahalifu badala ya kuchukua hatua kama kiongozi anakwambia nenda kwa OCD!!! Hapo kuna RPC kweli? Mtu anapompelekea taarifa RPC ujue huku chini yake hakuna ufanisi ndio maana wanakuja kwa mkubwa!!!
Hawa mapolisi wa design ya MURILO inafaa wapumzishwe.
 
Back
Top Bottom