Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

Polisi wa tanzania tumesoma na kusikia malalamiko mengi sana juu yao, mpaka inakuwa vigumu kuanza kutafuta mema yao.

Tunaona kuwa Polisi ndiyo wamekuwa chimbuko la rushwa, imefikia mpaka kuna msemo mitaani "kuingia kwa pesa, kutoka kwa pesa"

katika mema yao machache ni pale tunapoona kwenye vyombo vya habari wakijitangaza wao wenyewe kukamata majambazi na wezi, au, wameuwa jambazi fulani.

Nakumbuka sisi tulivyokuwa utotoni, miaka ya mwanzo 60s, tulibahatika kuliona jeshi la Polisi lililosheheni Wazungu, Wahindi, Waarabu na Waafrika. Na kila mtoto alitamani akikuwa awe polisi.

Polisi kilikuwa siyo chombo cha kutishia watoto, kila mtoto akipenda na kutamani awe polisi au kama polisi. Hivi sasa polisi imekuwa chombo cha kutishia watoto, ukimwambia mtoto "polisi huyo" basi mtoto anaweza kukulilia utafikiri kamuona ziraili mtowa roho za watu.

Tumefeli wapi na jeshi letu la Polisi?


Mtazamo wangu; Jeshi la polisi lilianza kufeli zamani sana, lilianza kufeli lilipoanza kutumiwa na wanasiasa kukandamiza wananchi wafanye watakavyo wao kwa nguvu au kwa hiyari. Chanzo nnachokikumbuka mimi ni vijiji vya ujamaa, watu walipoanzwa kuhamishwa makazi yao ya asili na kupelekwa vijiji vya ujamaa, jeshi la polisi likaanza kutumika kuwahamisha watu kwa nguvu na kuwapakia kwenye "makarandinga" kuwahamisha kutoka makazi yao ya asili na kwenda kuwatupa maporini waanzishe makazi mapya yaliyoitwa "vijiji vya ujamaa".

Kuanzia kipindi hicho serikali zote, mpaka leo hii, hazijaacha kuitumia polisi kama chombo chao cha kuhakikisha walitakalo wanasiasa ndilo wanalifanya polisi.

Tatizo liko wapi? Jee ni wakati siasa zikaachanishwa na kuendesha serikali? Serikali ibaki kama serikali na siasa zibaki kama siasa?

kinachotakiwa ni tafakuri ya kina, maji yakimwagika hayazoleki, lakini tunaweza kupiga deki na kuyakausha na kuchota mengine.

Wewe unaonaje? Umefikia wakati tuwe na Polisi binafsi?
Kongole dada FaizaFoxy kwa hoja mujarabu.

Hivi ndio vitu tunatakiwa tuvijadili (likiwemo la IGA kati ya nchi ya Tanzania na "nchi ya DP - World") kwa mustakabali mwema wa Tanzania yetu.

Kufeli kwa TanPol ni kutokana na kuchukua Watanzania ambao hawabebeki kwenye kada zingine za ajira za "staha".

Hawabebeki kwenye kada zingine kwa kuwa hawana vigezo vya ufaulu mzuri.

Kada za ajira zinazohitaji ufaulu mzuri zimetengenezewa maslahi mazuri.

TanPol ndiyo inayooneka kuwa ni "last option" kwa yule kijana aliyemaliza kidato cha nne au cha sita na kutopata ufaulu.

Serikali kudogosha na kudunisha hii kada pamoja na wanasiasa kuwatumikisha hawa TanPol kwa manufaa yao, ndio kunapopelekea changamoto za kuwa na polisi tulionao leo hii.

Tatizo la msingi ni serikali.
 
Si umeona jinsi traffic wanavyoendesha chombo
Chao cha Maputo wanayopata
Kutoka kwenye madalala
Hivi igp ashawahi kuzungumzia hiyo
Au wameshindwa wadhibiti!

Ova
Hao wakubwa ndo wanawatuma kukusanya pesa ukijifanya mjeuri unafukuzwa kazi au wanakutoa kitengo
 
Usingeandika kuhusu Dubai,ningekwambia uagize Pepsi kubwa hapo kwenye Mini - Supermarket ya mchaga njia panda ya kwenda kwako au pale Panone Supermarket.
 
Ulivo mjinga na uzee wako unatamani police wazungu sijui waarabu pumbavu ww.
Pita kule
Kweli kabisa, natamani polisi wawe na nidhamu na sifa za polisi waliopo duniani.

Huko ulipopataja Polisi wanakuwa ni kimbilio la jamii na ni washauri wakuu wa jamii inapokosea. Hapa kwetu ni kinyume chake, jamii, inaiogopa polisi. Kwanini?
 
Kweli kabisa, natamani polisi wawe na nidhamu na sifa za polisi waliopo duniani.

Huko ulipopataja Polisi wanakuwa ni kimbilio la jamii na ni washauri wakuu wa jamii inapokosea. Hapa kwetu ni kinyume chake, jamii, inaiogopa polisi. Kwanini?
Nenda kaishi huko huko walipo hao police malaika ,
Kwani hapa Tz kuna mtu kakulazimisha kuishi .
The choice is yours.
 
Ila police kwenye nchi nyingi ni corrupt...
Kwa sababu wana deal na wahalifu
Kuna police wengine wanakuwa upande wa wahalifu,wako kwenye payroll yao

Ova
 
Kituo Cha polisi Mbagala Kizuani au maturubai OCS na wenziwe wanafanya Mali ya baba Yao wale Watu Wana roho mbayaa Sanaaaa
Mule ndani Kuna wafungwa pale Kuna Watu mule wamefungwa kimya kimya,
Kuna mahabusu Yuko mule miezi miwili mitatu,mwingine sita Kwa kesi za ajabu ajabu mradi tu una pesa unahonga askari baasi umemaliza shughuli
 
Nkukasirikie nakujua atiii
Police wanazingua zingua sometimes.
Ila wewe pita kule Bibi.
Nipite wapi?

Hilo la kuzinguwa, ndilo tuliongelee na mazuri yao tuongelee. Kwenye mabaya tuishauri serikali ianye nini.
 
Kuna wale watuhumiwa walioiba benki billions zile wale Kuna askari walichukua pesà nyingi sana
Kuna mpelelezi wa Ile kesi Sasa anashirikiana na wake za watuhumiwa kuficha Baadhi ya nyumba alizonnua mmoja wa watuhumiwa wa Ile kesi
Kuna nyumba Mmoja wa wale watuhumiwa namjua vzr sana wameagana na askari mpelelezi kua kesi ikiisha aachiwe nyumba Moja ,nyingine wachukue wao
Sio uongo ni Kweli kabisa na kama wanasoma hapa wajue kabisa watu tunajua na wanajitapa kabisa wanakula na askari
 
Nipite wapi?

Hilo la kuzinguwa, ndilo tuliongelee na mazuri yao tuongelee. Kwenye mabaya tuishauri serikali ianye nini.
Pita kuzimu huko

Wew kama nani uishauri serikali
Nyie wanasiasa acheni vyombo vya ulinzi vifanye majukumu yake Kwa weledi
 
Kituo Cha polisi Mbagala Kizuani au maturubai OCS na wenziwe wanafanya Mali ya baba Yao wale Watu Wana roho mbayaa Sanaaaa
Mule ndani Kuna wafungwa pale Kuna Watu mule wamefungwa kimya kimya,
Kuna mahabusu Yuko mule miezi miwili mitatu,mwingine sita Kwa kesi za ajabu ajabu mradi tu una pesa unahonga askari baasi umemaliza shughuli
Inatisha, sasa mambo kama hayo ndiyo tuyaseme serikali watatusikia tu.

Tupe details tumwandikie Masauni na kopi tutapeleka Ikulu na kwa IGP. Tukikaa kimya na wao wanaona ni kawaida tu.


Polisi wanapofanya vyema tuwape maua yao, na wanapofanya mabaya tuwapakazie mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom