Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

Polisi wa Tanzania nini mabaya na mazuri yao? Kuna umuhimu wa kuwa na Polisi binafsi?

Polisi ni wazuri sana. Wanafanya kazi kubwa ya kuenforce law. Bila polisi hizi sheria tulizonazo ni takataka. Na polisi wanatakiwa kuwa wakali, watu wasio na mchezomchezo.

Wabaya wapo kama ambavyo kuna wabaya kila kona kuanzia marais, wabunge, madaktari, madereva nk.
 
Dah! Inatisha, sasa hivi kuna mtu kanambia kuna matatizo makubwa mawili yamejipenyea kwenye jeshi la polisi, yasipodhibitiwa hayo, tutateseka sana.

Kamari ya betting na Ulevi. Sasa hivi ni tatizo kubwa jeshini humo.

Sasa ikiwa polisi ni walevi kupindukia na wachea kamari kupindukia, hivi maadili ya vijana wetu hawa tutayasimamia vipi?

Hawa Masheikh na Maaskofu wawe wanapitia vituo vya polisi kuwapa darsa, wasikae misikitini na makanisani tu, kungoja wateja wao wawafate huko. Wawe na malengo.
 
Kuna wale watuhumiwa walioiba benki billions zile wale Kuna askari walichukua pesà nyingi sana
Kuna mpelelezi wa Ile kesi Sasa anashirikiana na wake za watuhumiwa kuficha Baadhi ya nyumba alizonnua mmoja wa watuhumiwa wa Ile kesi
Kuna nyumba Mmoja wa wale watuhumiwa namjua vzr sana wameagana na askari mpelelezi kua kesi ikiisha aachiwe nyumba Moja ,nyingine wachukue wao
Sio uongo ni Kweli kabisa na kama wanasoma hapa wajue kabisa watu tunajua na wanajitapa kabisa wanakula na askari
Weka details kamili hapa. Kwa utulivu.
 
Nipo mikononi mwa polisi maisha yangu bado ni mikosi afande - Sugu.

Wimbo huu maalamu kwa marehemu Michael Sikupya.
 
Kweli kabisa, natamani polisi wawe na nidhamu na sifa za polisi waliopo duniani.

Huko ulipopataja Polisi wanakuwa ni kimbilio la jamii na ni washauri wakuu wa jamii inapokosea. Hapa kwetu ni kinyume chake, jamii, inaiogopa polisi. Kwanini?

endelea kutamani tu.

polisi wenu wa bongo hapa hata mishahara ya maana mmeshindwa kuwalipa mnaota polisi wenye maadili!!!

polisi anastaafu baada ya maiak 30 ya kazi yenye masimango analipwa milioni 17 kiinua mgongo 2023[emoji28][emoji28][emoji28],
rais nayeye anashangaa hajui tatizo nini.
waziri wa mambo ya ndani naye hajui tatizo nini.
Igp katoa macho haelewi shida iko wapi.

unafikiri ni polisi gani atazubaa kutochukua rushwa kwa asante hii ya kifedhuli kutoka serikalini!!!???
ukizingatia rushwa yenyewe haombi anapewa kwa ushawishi.
juzi kwenye kamati ya haki jinai,mzee mmoja anasema polisi wanalipwa laki 9 na posho zao zinafika 1.6ml kwa mwezi[emoji28][emoji28],huyu katumwa na rais ampelekee majibu ya changamoto katika utoaji haki ngazi zote,hicho ndicho anachokijua kuhusu maslahi ya polisi.
IMG_2403.jpg
 
endelea kutamani tu.

polisi wenu wa bongo hapa hata mishahara ya maana mmeshindwa kuwalipa mnaota polisi wenye maadili!!!

polisi anastaafu baada ya maiak 30 ya kazi yenye masimango analipwa milioni 17 kiinua mgongo 2023[emoji28][emoji28][emoji28],
rais nayeye anashangaa hajui tatizo nini.
waziri wa mambo ya ndani naye hajui tatizo nini.
Igp katoa macho haelewi shida iko wapi.

unafikiri ni polisi gani atazubaa kutochukua rushwa kwa asante hii ya kifedhuli kutoka serikalini!!!???
ukizingatia rushwa yenyewe haombi anapewa kwa ushawishi.
View attachment 2701488
Hayo ndiyo matatizo ya kuzungumzwa bila ushabiki.

Duniani huko kuna nchi zimeanza kuweka Polisi binafsi (Private Police), ni muhimu na Tanzania tukaanza huo mpango.

Ni kitu kinachowezekana kikipangwa vizuri.
 
Hayo ndiyo matatizo ya kuzungumzwa bila ushabiki.

Duniani huko kuna nchi zimeanza kuweka Polisi binafsi (Private Police), ni muhimu na Tanzania tukaanza huo mpango.

Ni kitu kinachowezekana kikipangwa vizuri.
Mfano Railway, inatakiwa iwe na polisi wake binafsi, wanalipwa na Railwa na wanafundishwa sheriaa na nidhamu zote za Kipolisi.

Bandari.

Vituo vya mabasi, ni sehemu nyingi sana zinaweza kuwa na Polisi binafsi. Ambao wanakuwa ni hawahawa polisi waliopitia vyuo vyote ila huku wanaongezewa mafunzo ya ufanisi na mishahara inakuwa ya binagfsi siyo ya serikali, mafao yanakuwa ya binafsi siyo ya sereikali.


Kuna njia nzuri zinazweza kufanyika, kuupunguzia mzigo serikali, na wale waserikalini wakajikuta wanalipwa vizuri pia.

mfano mwingine ni askari jela, jela zinatakiwa zizalishe, zinawezza kuajiri polisi binafsi wenye nidhamu na wataheshimu kazi kwa kuwa watalipwa vizuri.


Ni wakati tuanze kuwa positive.
 
Hayo ndiyo matatizo ya kuzungumzwa bila ushabiki.

Duniani huko kuna nchi zimeanza kuweka Polisi binafsi (Private Police), ni muhimu na Tanzania tukaanza huo mpango.

Ni kitu kinachowezekana kikipangwa vizuri.

kama walinzi mnao na kampuni tayari,fanyeni mchakato mpate taasisi binafsi za upelelezi sio polisi kamili.
 
Pamoja na changamoto wanazozipitia Wapiganaji wetu ila bado ni chombo makini sana tunawashukuru sana POLISI WETU.

Bila wao amani mitaani isingekuwepo.

Hongera kwao General Duty/Field Force Unit/CID's/Intelijensia kwa kazi nzuri.
 
Weka details kamili hapa. Kwa utulivu.
hili suala askari mmoja hivii Kule kitaa ,alisema hvi ndugu tu Hata nikisema niripoti ntajikuta nahamishwa kituo au wakubwa wanachukua wao hizoo nyumba au wasilifanyie Kazi,ila sana sana ni kua watachukua wao wakubwa baasi hvyo Bora kuacha tu
Hii bongo askari 99%are corrupt
 
Tueleze walikufanya nini?
Kuna diwani fulani wa kata fulani iliyopo KOROGWE ndugu yake alikamazwa na Mali ya wizi ya zahanati iliyopo kata hiyo (viatilifu) robota 2 na jamaa akafikishwa kituo cha polisi wilaya,huwezi amini alichokifanya diwani yule akishirikiana na polisi........
 
Polisi wa tanzania tumesoma na kusikia malalamiko mengi sana juu yao, mpaka inakuwa vigumu kuanza kutafuta mema yao.

Tunaona kuwa Polisi ndiyo wamekuwa chimbuko la rushwa, imefikia mpaka kuna msemo mitaani "kuingia kwa pesa, kutoka kwa pesa"

katika mema yao machache ni pale tunapoona kwenye vyombo vya habari wakijitangaza wao wenyewe kukamata majambazi na wezi, au, wameuwa jambazi fulani.

Nakumbuka sisi tulivyokuwa utotoni, miaka ya mwanzo 60s, tulibahatika kuliona jeshi la Polisi lililosheheni Wazungu, Wahindi, Waarabu na Waafrika. Na kila mtoto alitamani akikuwa awe polisi.

Polisi kilikuwa siyo chombo cha kutishia watoto, kila mtoto akipenda na kutamani awe polisi au kama polisi. Hivi sasa polisi imekuwa chombo cha kutishia watoto, ukimwambia mtoto "polisi huyo" basi mtoto anaweza kukulilia utafikiri kamuona ziraili mtowa roho za watu.

Tumefeli wapi na jeshi letu la Polisi?


Mtazamo wangu; Jeshi la polisi lilianza kufeli zamani sana, lilianza kufeli lilipoanza kutumiwa na wanasiasa kukandamiza wananchi wafanye watakavyo wao kwa nguvu au kwa hiyari. Chanzo nnachokikumbuka mimi ni vijiji vya ujamaa, watu walipoanzwa kuhamishwa makazi yao ya asili na kupelekwa vijiji vya ujamaa, jeshi la polisi likaanza kutumika kuwahamisha watu kwa nguvu na kuwapakia kwenye "makarandinga" kuwahamisha kutoka makazi yao ya asili na kwenda kuwatupa maporini waanzishe makazi mapya yaliyoitwa "vijiji vya ujamaa".

Kuanzia kipindi hicho serikali zote, mpaka leo hii, hazijaacha kuitumia polisi kama chombo chao cha kuhakikisha walitakalo wanasiasa ndilo wanalifanya polisi.

Tatizo liko wapi? Jee ni wakati siasa zikaachanishwa na kuendesha serikali? Serikali ibaki kama serikali na siasa zibaki kama siasa?

kinachotakiwa ni tafakuri ya kina, maji yakimwagika hayazoleki, lakini tunaweza kupiga deki na kuyakausha na kuchota mengine.

Wewe unaonaje? Umefikia wakati tuwe na Polisi binafsi?
Police Wajinga wapo na police wenye akili ya kujua majukumu yao pia wapo, kazi kwako kuwatafuta police wenye maadili mema kwenye kazi zao humo humo ndani ya Jesho la Police! Mfano mdogo,Mimi kuna mpelelezi aluzingua kwenye kesi yangu,lakini baada ya kulalamika,kuna police wengine walikuja rekebisha Jambo langi hadi Mahakama ikanipa haki yangu!
 
Back
Top Bottom