Polisi wabadili gia angani, Wanadai hawajui alipo Mfanyakazi wa LHRC Tito Magoti

Ukiona manyoya...Duuh naomba isiwe kweli Jah mlinde Titto na wenzake!
 

Chuki inazidi kukolezwa na wao wenyewe wenye Mamlaka. Kwani kama ana tuhuma au makosa si wangemkamata kwa kufuata utaratibu tu!? Taifa linaendekeza chuki!
 
Na mimi nahisi hivyo, aidha ndio bai bai au amepigwa sana wanashindwa kumtoa
 
Hata suala na Ben Saanane inaweza ikawa hivyo hivyo. Wakishakutesa wakaona umetepa au unaweza kuwafia wanakupoteza kabisa.
 
Na makanisani msiwe mnaenda. Chagua kuishi kama mashetani. Tunawaona mtangaza Upendo ,Amani,Mshikamano. Huyo Mungu mnayemwomba alete Amani ndo huyu wa Yakobo Isaka na Ibrahimu ?.Sasa tulipigania uhuru kwa ajili gani kama kama watu wanachukuliwa na kuahawa kila siku?. Tabia hii italipeleka taifa pabaya .Taifa litapasuka kwa tabia hii Tunakemea na kulaani kila siku juu ya tabia hii nyie mnaendelea na vichwa vyenu vigumu.
 
Hivi hawa watu wafanyao hivi wanafanya kwa niaba ya nani? Jee huyo anayewatuma SIO ADUI WA TAIFA HUYO?
Tuvumilie hiki kitu hadi lini? Hata hawa wenzetu tulio nao hapa JF wanao unga mkono utekaji na mateso kwa nini na sisi tusiwashukie kama mwewe hata kama ni kupigwa ban potelea mbali au tuwaweke wote kwenye ignore list?
Moyo wangu ni mzito sana nikiwaza yakuwa pengine Tito kateswa na kafa au yuko hoi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…