Msengapavi
JF-Expert Member
- Oct 23, 2008
- 8,819
- 7,638
Mambosasa keshasema Tito Magoti yuko kwenye mikono salama na ‘Habeas corpus’ case imeshaanzishwa LHRC ili kuhakikisha anafinguliwa mashtaka haraka. Kwa hiyo tuamini kuwa yuko hai na kwa haraka ataachiwa au atafiishwa mahakamani. Kinyume cha hayo patachimbika tu!Inawezekana wamesha katisha uhai wake, sasa wanajitoa kabisa, huenda asipatikane.
Mimi nadhani polisi hawakumkamata Tito Magoti badala yake alikamatwa na WATU WASIOJULIKANA ambao ni kikundi kinachopewa amri na mkuu wa rogue elements za ikulu au TISS. Baada ya makelele mengi kwenye social media waliomteka Magoti wameitaka polisi kufanya kile kinachoitwa DAMAGE CONTROL. Hiyo ndo maana RPC wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni hajui lolote kuhusu kukamatwa kwa Magoti nacwenzake watatu.Terror squad kazini. Wasiojulikana wanajulikana na kulindwa
ITAKUWA WALIMKAMATA TITAAAAA MAGOTI SIO TITOOKamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni asema hana taarifa za kukamatwa na kushikiliwa kwa mwanaharakati,Tito Magoti
Mussa Taibu amesema kuwa mpaka sasa hana taarifa ya kukamatwa kwa Ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu [LHRC] Tito Magoti, katika eneo la himaya yake na hata amejaribu kuwauliza wenzake lakini nao hawana taarifa hizo.
Awali Kamanda Lazaro Mambosasa aliuthibitisha Umma kwamba Magoti alikamatwa Mwenge wilayani Kinondoni
Taarifa za awali kuhusu kutekwa kwa Tito Magoti ni kuwa alikuwa katika bodaboda akielekea Mwenge kununua simu, alipofika katika kituo cha mafuta cha Puma watu 5 waliokuwa na gari aina ya Harrier walimchukua kwa mabavu kisha kuondoka kwa uelekeo wa Posta, Dar es Salaam.
Jana Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar, Lazaro Mambosasa amekaririwa akisema Polisi inamshikiliwa Magoti na wenzake watatu kwa uchunguzi wa tuhuma za makosa ya jinai inayowakabilia.
Hata hivyo, Mambosasa hajawahi kubainisha ni kituo gani ambacho Magoti anashikiliwa.
Zaidi, soma:
View attachment 1301209Mwanasheria Tito Magoti wa LHRC achukuliwa na watu wasiojulikana; Polisi wasema wanamhoji na wenzake 3
Tito ambaye ni Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) inadaiwa ametekwa maeneo ya Mwenge, Jijini Dar Yaelezwa amechukuliwa na watu 5 waliovalia kiraia ambao walimfunga pingu kabla ya kuondoka naye Watu hao walikuwa kwenye gari aina ya Harrier. Taarifa za awali kuhusu...www.jamiiforums.com
View attachment 1301208
ukimsikiliza vizuri huyo RPC wa kinondoni amesema hana taarifa na watu wake wote amewauliza hawana taarifa,sio mzembe wala mpumbavu kusema hivyo maana kwa utaraatibu wa kipolisi jambo lolote linalotokea chini ya himaya yake ni lazima awe na taarifa nalo hasa kama waliohusika ni askari polisi hata kama wametokea mkoani ripoti lazima ifike kwake.Tatizo liko wapi? Mambosasa kazu gumza kwa niaba ya jeshi la polisi. Huyo RPC wa Kinondoni kanusho lake ni upumbavu mtupu, maana wa kwanza kutoa tamko ni boss wake hivyo ndio aliye sahihi kuwa kakamatwa kinondoni na hata kama kapelekwa Kigamboni bado ofisi ya RPC Kinondoni lazima inataarifa kama hajui ni uzembe wake tuu
Sent using Jamii Forums mobile app
nadhani wewe ndio hujafanya reasoning,jambo likishavuka mamlaka ya kikanda ni lazima mwenye kanda yake awe na taarifa fullstop.labda kama yanafanyika mambo kwa mazoea bila kufuata utaratibu,nilikuwa naomuona ndugu yangu mmoja wa jeshi silitaji akitoka mkoani kuja hata ikiwa ni likizo lazima aripoti makao makuu,hata kama atakaa siku nne tu.Sina hakika kama huwa tunafanya reasoning kabla ya kufikia conclusion. Aliyekiri kwamba huyo Tito kakamatwa na polisi ni Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam. Sasa mtu unaenda kumuuliza RPC wa Kinondoni halafu anakumbia hana taarifa hizo kisha mbio mbio unakuja kubandika bandiko hapa kuwa polisi imekanusha. Hivi RPC wa Kinondoni anajua yanayofanyika na vikosi vya kanda maalum? Hivi RPC wa kinondoni anajua yanayofanyika Central Police? Hivi RPC wa Kinondoni anajua yanayofanyika Temeke? Hivi RPC wa Kinondoni anajua yanayofanyika Ilala? Kwa nini hatupendi kwenda extra mile kuwa kwa sababu wa Kinondoni hajui basi tumuulize wa Temeke, wa Ilala na tukishindwa basi turudi kwa Mambosasa ambaye ndiye mwenye utawala katika mikoa yote mitatu ya kipolisi. Mtu kukamatwa Mwenge siyo lazima awe amepelekwa kwenye vituo vya polisi Kinondoni tena hasa kama waliohusika na kumkamata ni polisi wanaofanya kazi katika mikoa yote mitatu, yaani kanda maalumu.
Umeandika UTOTO,operation ya siri ni kwetu sisi wananchi ndio inakuwa siri lakini sio kwa RPC!Sijaona utata wowote ... naona mwandishi ama mtu aliyeanzisha huu uzi ndio ana lengo lake aidha kupotosha ama hajaelewa ... maana kamanda wa kinondoni kasema kabisa yeye hana taarifa na ya kuwa kamanda mambosasa hawajibiki kumpa taarifa yeye .. na ya kuwa kuna operation nyingine ni za siri ... sasa mpaka hapo mlitaka aseme nini?
ukisoma michango ya watu humu ndugu yangu ndio utaelewa sisi WATANZANIA ni watu wa aina gani.tupo tupo tu,hatujui wajibu wala haki zetu,bado tuna safari ndefu.Operation ya ikfanyika eneo Fulani mkuu wa eneo husika lazima ajue!!!!!
Mkuu wa eneo husika kasema hajui hiyo operation.
Au ukiona operation ya siri hata RPC haambiwi basi ujue haijafuata utaratibu wa kipolisi na kuna genge ambalo linatumika ndani ya polisi kufanikisha matukio kama hayo,sasa kuna watu wengine hawapendi kuunganishwa na matukio hayo ya kiuhalifui wao wakiwa viongozi maana wanajua JINAI haina EXPIRE DATE.Hizo ni ngonjera tu. Hivi ni operation ya siri kiasi gani hata ushindwe kumjulisha RPC wa eneo hilo? Halafu imefanywa na askari kanzu hivi askari wengine wakiwaona wafikiri ni majambazi si wanaweza kuwarushia risasi wakawaua wenzao?
Ukiona operesheni ya siri hata RPC haambiwi basi inamaana bosi amekosa imani na huyo RPC na ingekua bora amuondoe halafu aweke ambaye anamuamini.
Sent using Jamii Forums mobile app
Confuse them
Confuse again
Confuse them once more
Dah!...Mimi nadhani polisi hawakumkamata Tito Magoti badala yake alikamatwa na WATU WASIOJULIKANA ambao ni kikundi kinachopewa amri na mkuu wa rogue elements za ikulu au TISS. Baada ya makelele mengi kwenye social media waliomteka Magoti wameitaka polisi kufanya kile kinachoitwa DAMAGE CONTROL. Hiyo ndo maana RPC wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni hajui lolote kuhusu kukamatwa kwa Magoti nacwenzake watatu.
Nchi hii imeanza kushindikana kutawala!
Sent from my iPhone using JamiiForums
Usiseme sisi Wa tanzania hatujui haki! acha maneno yako hayo! temea mate chini, inawezekana bado mdogo weye Duniani kote hakuna haki, nenda popote ndiyo utajua bora uliyo yaacha nyuma ni nafuu, fanya chochote! Neno ''haki '' itabaki kuwa siasa tu na maneno ya propaganda! kutoka kwa Tabaka tawala dhidi ya tabaka tawaliwa milele yote!ukisoma michango ya watu humu ndugu yangu ndio utaelewa sisi WATANZANIA ni watu wa aina gani.tupo tupo tu,hatujui wajibu wala haki zetu,bado tuna safari ndefu.