The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni asema hana taarifa za kukamatwa na kushikiliwa kwa mwanaharakati,Tito Magoti
Mussa Taibu amesema kuwa mpaka sasa hana taarifa ya kukamatwa kwa Ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu [LHRC] Tito Magoti, katika eneo la himaya yake na hata amejaribu kuwauliza wenzake lakini nao hawana taarifa hizo.
Awali Kamanda Lazaro Mambosasa aliuthibitisha Umma kwamba Magoti alikamatwa Mwenge wilayani Kinondoni
Taarifa za awali kuhusu kutekwa kwa Tito Magoti ni kuwa alikuwa katika bodaboda akielekea Mwenge kununua simu, alipofika katika kituo cha mafuta cha Puma watu 5 waliokuwa na gari aina ya Harrier walimchukua kwa mabavu kisha kuondoka kwa uelekeo wa Posta, Dar es Salaam.
Jana Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar, Lazaro Mambosasa amekaririwa akisema Polisi inamshikiliwa Magoti na wenzake watatu kwa uchunguzi wa tuhuma za makosa ya jinai inayowakabilia.
Hata hivyo, Mambosasa hajawahi kubainisha ni kituo gani ambacho Magoti anashikiliwa.
Zaidi, soma:
View attachment 1301209Mwanasheria Tito Magoti wa LHRC achukuliwa na watu wasiojulikana; Polisi wasema wanamhoji na wenzake 3
Tito ambaye ni Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) inadaiwa ametekwa maeneo ya Mwenge, Jijini Dar Yaelezwa amechukuliwa na watu 5 waliovalia kiraia ambao walimfunga pingu kabla ya kuondoka naye Watu hao walikuwa kwenye gari aina ya Harrier. Taarifa za awali kuhusu...www.jamiiforums.com
View attachment 1301208
Inawezekana ACP Mambosasa ni polisi wa Rwanda na ACP Mussa ndiyo polisi wa Tanzania....
Kwanini polisi wa nchi moja tena wakiwa wanaongoza mkoa mmoja wawe na kauli za kutofautiana juu ya tukio moja la uhalifu lililotokea ndani ya eneo lao la kiutawala???
Tuseme nini sasa? Kwamba, serikali ina kikundi cha askari cha utekaji wa watu wakosiaji wa utawala huu huku baadhi ya viongozi wakuu wa polisi wakiwa hawajui??
For sure, kauli hizi mbili zinazokinzana za viongozi wakubwa wawili wa polisi ndani ya mkoa mmoja, nchi moja zinathibitisha kuwa utekaji wote wa critics wa serikali, kushambuliwa kwa risasi kwa watu kama Tundu Lissu na uhalifu wote unaofanana na huu, unatekelezwa na dola chini ya uratibu wa ikulu....!!