Polisi wabadili gia angani, Wanadai hawajui alipo Mfanyakazi wa LHRC Tito Magoti

Polisi wabadili gia angani, Wanadai hawajui alipo Mfanyakazi wa LHRC Tito Magoti

_point_right_Mambosasa tumemkamata Tito _point_right_RPC Kinondoni sina taarifa ya kukamatwa T...jpg


Hapa ndipo lilipofikia Jeshi la Polisi la Tanzania , bila shaka kuna laana inaliandama .
 

Attachments

  • Two contradicting statements.! ( 268 X 480 ).mp4
    1.1 MB
Hizo ni ngonjera tu. Hivi ni operation ya siri kiasi gani hata ushindwe kumjulisha RPC wa eneo hilo? Halafu imefanywa na askari kanzu hivi askari wengine wakiwaona wafikiri ni majambazi si wanaweza kuwarushia risasi wakawaua wenzao?

Ukiona operesheni ya siri hata RPC haambiwi basi inamaana bosi amekosa imani na huyo RPC na ingekua bora amuondoe halafu aweke ambaye anamuamini.
Sijaona utata wowote ... naona mwandishi ama mtu aliyeanzisha huu uzi ndio ana lengo lake aidha kupotosha ama hajaelewa ... maana kamanda wa kinondoni kasema kabisa yeye hana taarifa na ya kuwa kamanda mambosasa hawajibiki kumpa taarifa yeye .. na ya kuwa kuna operation nyingine ni za siri ... sasa mpaka hapo mlitaka aseme nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilivyomuelewa kamanda wa kinondoni ni kwamba yeye kama yeye kwenye mkoa wake hajamshika Tito ila kuna Operation zinawezwa kufanywa na mkuu wa kanda nzima na yeye asipewa taarifa kwa mantiki hiyo Mambosasa na BASHITE ndio wamemkamata Tito/Bolleni ukiunganisha nukta.
Mkuu @Bollen Ngeti nae wanamshikilia?!,nimezimisi sana makala zake kule fb

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka tutekwe wote ndio tutajua umuhimu wa kuungana kama Taifa kupinga huu udhalimu.

Naanza kupata mashaka kama Tito bado tunae na kama tunae,basi sijui atakuwa katika hali gani.

Ukiona hivi, ujue kuna uwezekana wa mambo mawawili:wamemtanguliza au wamemuumiza na kumjeruhi vibaya kiasi kwamba hawako tayari kuhusishwa/kutuhumiwa na hivyo tunaweza kumuokota akiwa kama Dr.Ulimboka.
Hivi Ulimboka alipotelea wapi? Roma yeye anasemaje kuhusu masahibu yake na kwanini Makonda (Bashite) huwa anajishughulisha na watu wanaotekwa?
 
Back
Top Bottom