Polisi wadai kumhoji 'mtesaji' wa Ulimboka

Polisi wadai kumhoji 'mtesaji' wa Ulimboka

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
JESHI la Polisi nchini limedai kumhoji mtu anayedaiwa kuwa Afisa Usalama wa Ikulu, Ramadhan Ighondu, anayetuhumiwa kuwa mhusika mkuu katika tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk. Steven Ulimboka.

Akizungumza na Tanzania Daima jana ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi, Isaya Mngulu, alisema kuwa tayari polisi ilishamhoji Ighondu kwa tuhuma hizo.

Juni 26, mwaka jana, Dk. Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana na kupelekwa katika pori la Mabwepande ambako alipigwa na kuteswa vibaya kwa kunyofolewa kucha na kung'olewa meno na kisha kutelekezwa huko kabla ya kuokolewa na msamaria mwema na kukimbizwa hospitalini.

Dk. Ulimboka alimtaja wazi wazi Ighondu kuwa ndiye alipanga na kuratibu njama za kutekwa kwake, na kusisitiza kauli yake hiyo kwa kula kiapo mbele ya wakili wake, Dk. Rugemezela Nshala, ambayo ilisomwa mbele ya waandishi wa habari.

Mngulu alisema kuwa jeshi la polisi lilishamuita na kumhoji Ighondu kuhusiana na tuhuma za utekaji na kutesa zilizotolewa dhidi yake na Dk. Ulimboka na kwamba hawakubaini ushahidi wa kutosha kuweza kumfungulia mashtaka mahakamani.

"Sisi tulishamhoji huyo Ramadhan Ighondu kuhusiana na tuhuma za Ulimboka dhidi yake, lakini hatukumfikisha mahakamani kwa sababu ushahidi haukujitosheleza.

"Sisi tunapeleka mtuhumiwa mahakamani tunaporidhika kuwa ushahidi tulioupata una nguvu, na siyo kweli kwamba kila mtu anayehojiwa na polisi lazima afikishwe mahakamani," alifafanua Mngulu.

Aidha Mngulu alisema kuwa mbali ya kumhoji Ighondu, pia walimhoji wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, kuhusiana na suala hilohilo.

Hata hivyo, Kicheere alikanusha kuhojiwa na polisi kuhusiana na suala la Dk. Ulimboka, bali aliitwa polisi kuwasilisha tamko la kisheria (hati ya kiapo) la Dk. Ulimboka ambamo anathibitisha kuwa Ramadhan Ighondu ndiye aliyepanga na kuratibu njama zote za kutekwa na kuteswa kwake.

"Siyo kweli kwamba nimewahi kuhojiwa na polisi kuhusu suala la Dk. Ulimboka, hawajanihoji, ila niliitwa makao makuu ya polisi na nilipofika pale hawakunihoji chochote bali waliomba niwape ile hati ya kiapo ya Dk. Ulimboka ambayo niliisoma mbele ya waandishi wa habari, na pia niliwapatia cheti cha kisheria cha kuniidhinisha kuisoma hati hiyo kwa waandishi wa habari," alibainisha Kicheere na kuongeza:

"Ila nimepata taarifa kwamba polisi wamepanga kuniita tena ili nikaandikishe maelezo, kwa hiyo nawasubiri waniite rasmi, lakini nasisitiza kuwa kwa sasa polisi hawajanihoji chochote kuhusu suala hilo," alisisitiza.

Hata hivyo, wakati polisi wakidai kumhoji Ighondu, hawajawahi kumuita wala kumhoji Dk. Ulimboka ambaye ndiye shahidi namba moja na mtu pekee anayewajua bila chembe ya shaka watekaji na watesi wake.


CHANZO:
TANZANIA DAIMA ONLINE LA TAREHE 23/03/2013.
 
Swali,walikuwa wapi siku zote?

Kelele za members wa JF zimechangia kuwaamsha?

Je,wanatuzuga tu?
 
Wanajaribu kufukua mizimu ili kufukia hili la Kina Lwakatare. Mtu wa kwanza kufika Eneo la tukio alipotekwa Dkt Uli alikuwa Kijokisimba maana alikuwa anaskilizia maana alifanikiwa kwenda na Jopo la waandishi ili wampige Picha Uli akiwa eneo la Tukio, baada ya hapo aka Organise maandamano yalokosa watu Pale salenda Bridge, baadae eti akaenda Amnest Internation 'kumlilia' Dkt Uli, Msiban mafia huwa wanalia mpaka kukosa nguvu sijui kwa nn?Ukweli uliahirishwa ila haukufutwa!
 
Wana JF heshima kwenu wakuu !!

Ni vyema afande Isaya Mngulu akalifahamu hili mapema " Watanzania wa leo siyo wadanganyika tena, na tumesha poteza imani na poliCCM kwa zaidi ya asilimia 200".
 
Je polisi imewahi kumhoji Mwigulu Nchemba? Ninayo maswali mengi kwa Mkuu wa Polisi Said Mwema ila nadhani kwa sasa naota tu, nauchapa usingizi mzito! Kiukweli hatuna jeshi la polisi, tuna genge tu la vibaka lililoajiriwa na serikali inayoundwa na chama cha mafisadi.
 
Polisi wanaona wamebanwa kila upande sasa wanatafuta pa kutokea.Mbona wanashindwa kumhoji Dr Ulimboka mwenyewe
 
kama mnabisha rama hakuojiwa,wakati mnaambiwa alihojiwa hailet mantik.mlitaka ahojiwe ktk tv ama.
 
Je polisi imewahi kumhoji Mwigulu Nchemba? Ninayo maswali mengi kwa Mkuu wa Polisi Said Mwema ila nadhani kwa sasa naota tu, nauchapa usingizi mzito! Kiukweli hatuna jeshi la polisi, tuna genge tu la vibaka lililoajiriwa na serikali inayoundwa na chama cha mafisadi.

Ee bwana hapo umeua! Lakini chonde chonde wasije kukutoa meno yako na kucha!
 
Kwa hiyo yule Mkenya ws Kova cinema string amekufa???? Tanzania bwana,!! Sawa na jiwe lililo karibu ma nyani. Akijisikia kijikuna analitumia.
 
Na bado watazidi kulikoroga. damu ya Dr Uli haikumwagika bure wanafikiri Watanzania wa Leo ni mambumbumbu hawajui kuchambua habari na kuzifuatilia.
 
'Mh habari za kazi'
'nzuri tu, kuna nin?
'aaaaa... Eeeeee... Karibu chai kwanza mheshimiwa'
'sina mda wa kunywa chai hapa, nambie ulichoniitia'
'Akchuale..aaa ..unajua bwana vyombo vya habari vinaandika upuuzi sana... aaaa hasa hawa mwanahalisi aaaa kuhusu hii ishu ya huyu mjinga Ulimboka.., sasaaa, sijui tunafanyaje..'
'hakuna shida, mwanahalisi nimeshaagiza lifungiwe... hao wengine waache tu waongee, si wanatumiwa na cdm?... Aaa haina shida kuna mpango tunakamilisha kuhakikisha hili suala linawageukia cdm... Watakomaje?.... Hahhahahaaa... Kuna jingine?'

'hakuna mheshimiwa sisi tunawaahidi tu kutoa ushirikiano wa hali ha juu kwa lolote mtakapotutaka tufanye kukamisha hiyo mipango yenu.... hahahhahhaaaa..asante mheshiwa, pole kwa usumbufu... si unajua tena fomalite?
'hakuna cha fomalite wewe, hizo fomalite zinafanya kazi huko kwa akina mramba na yona, sio ikulu... Kwaheri'
 
Back
Top Bottom