"Sisi tunapeleka mtuhumiwa mahakamani tunaporidhika kuwa ushahidi tulioupata una nguvu, na siyo kweli kwamba kila mtu anayehojiwa na polisi lazima afikishwe mahakamani," alifafanua Mngulu.
Aidha Mngulu alisema kuwa mbali ya kumhoji Ighondu, pia walimhoji wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, kuhusiana na suala hilohilo.
Hata hivyo, Kicheere alikanusha kuhojiwa na polisi kuhusiana na suala la Dk. Ulimboka, bali aliitwa polisi kuwasilisha tamko la kisheria (hati ya kiapo) la Dk. Ulimboka ambamo anathibitisha kuwa Ramadhan Ighondu ndiye aliyepanga na kuratibu njama zote za kutekwa na kuteswa kwake.
"Siyo kweli kwamba nimewahi kuhojiwa na polisi kuhusu suala la Dk. Ulimboka, hawajanihoji, ila niliitwa makao makuu ya polisi na nilipofika pale hawakunihoji chochote bali waliomba niwape ile hati ya kiapo ya Dk. Ulimboka ambayo niliisoma mbele ya waandishi wa habari, na pia niliwapatia cheti cha kisheria cha kuniidhinisha kuisoma hati hiyo kwa waandishi wa habari," alibainisha Kicheere na kuongeza:
"Ila nimepata taarifa kwamba polisi wamepanga kuniita tena ili nikaandikishe maelezo, kwa hiyo nawasubiri waniite rasmi, lakini nasisitiza kuwa kwa sasa polisi hawajanihoji chochote kuhusu suala hilo," alisisitiza.
Hata hivyo, wakati polisi wakidai kumhoji Ighondu, hawajawahi kumuita wala kumhoji Dk. Ulimboka ambaye ndiye shahidi namba moja na mtu pekee anayewajua bila chembe ya shaka watekaji na watesi wake