Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Jeshi la polisi limeendelea na danadana zake kukwepa kumpeleka msanii Optter Mahakamani huku likiendelea kuzuia dhamana yake.
Wakili kutoka kituo cha THRDC amepeleka hati ya kimahakama kuwataka Polisi kumpeleka mchora katuni Mahakamani.
Kwa mujibu wa sakata hili, RCO wa Kinondoni ameendelea kushikilia suala la mchora katuni huyu huku akielezea kuwa anatekeleza maagizo.
Jana afisa upelelezi wa shauri hili anadaiwa kuchukua maelezo ya mtuhumiwa na jana hiyo hiyo polisi wameenda kupekua kwenye makazi ya Optter. Inadaiwa mazingira yanaonesha kuwa Polisi wamekuwa wakimlazimisha mtuhumiwa akiri makosa wanayomtuhumu nayo au la ataozea jela
Polisi kituo cha Oysterbay wanadaiwa kuendelea kutengeneza mazingira ya kuhakikisha wanaendelea kumshikilia hapo kituoni.
Baadhi ya Askari wanadai, kuna shinikizo kutoka kwa wavaa viatu wakitaka kujua msanii ametumwa na nani kuchora picha inayowasumbua wakubwa.
Tutaendelea kuwajuza kinachojiri