Polisi wakanusha tuhuma za Abdul kuua mtu Jangwani

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Kuna taarifa inasambazwa kwenye mitandao ya Kijamii yenye kichwa cha habari kinachosomeka "ABDUL NA KUNDI LAKE WAMTEKA MWANDISHI WA HABARI WAMNYONGA NA KUMTUPA MTO JANGWANI".

Maandishi hayo yanaonekana kama ilivyo hapo kwenye kiambatisho na pia kinaonekana kitu kinachoelea.

​
Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuwa kitu kinachoonekana kinaelea kiliripotiwa tarehe 27.8.2025 majira ya saa tatu asubuhi kuwa huko Magomeni Mapipa chini ya daraja la Jangwani kuna mwili wa binadanu unaelea.

Maafisa wataalamu wa kuchunguza matukio makubwa wakiwa pamoja na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji walifika katika eneo hilo na kwa kufuata taratibu zote waliutoa mwili huo kutoka ndani ya maji.

Wakati uchunguzi ukiendelea ndugu wa mtu huyo walipatikana na wakaweza kuutambua mwili huo kuwa ni wa Salehe Shukrani, Mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza mikate, mkazi wa Magomeni Mikumi.
Pia walieleza kuwa, ndugu yao huyo alikuwa na tatizo la kuanguka kutokana na kifafa kilichokuwa kinamsumbua.

Pamoja na maelezo hayo uchunguzi wa kitaalam ulifanyika na mwili haukuwa na alama zote ambazo zilionesha kuwa alishambuliwa au kufanyiwa jambo lolote lile la kumdhui Jeshi la Polisi Tanzania linaendelea kutoa wito kwa Jamii kuzipuuza, kuacha kuzisambaza na kushabikia taarifa za uongo na upotoshaji kama hizo.

​
 
Mgonjwa wa kifafa alikuwa anatembea huku amejitia kwenye kiroba!😁

BTW:Ukimtaja Abdul tu wanajitokeza kukanusha isipokuwa lile tukio la RR iliyomuachia nyoya traffic!
 
Si alikuwa kwenye kiroba? au ?Sawa alikuwa na tatizo la kuanguka sasa aliingiaje kwenye kiroba?..aliangukia ndani ya kiroba?

Kifafa tena amekutwa kwenye kiroba?Jeshi la polisi sijui nani mwandishi wa hizi script zenu.Familia imesema kifafa ndio lakini mbona hakuna uhusiano na mwili kukutwa kwenye kiroba?

Mgonjwa wa kifafa alikuwa anatembea huku amejitia kwenye kiroba!😁

BTW:Ukimtaja Abdul tu wanajitokeza kukanusha isipokuwa lile tukio la RR iliyomuachia nyoya traffic!
Mambo ni mengi, labda tuseme aliingia kwenye gunia ndio kifafa kikapanda.
 
Mgonjwa wa kifafa alikuwa anatembea huku amejitia kwenye kiroba!😁

BTW:Ukimtaja Abdul tu wanajitokeza kukanusha isipokuwa lile tukio la RR iliyomuachia nyoya traffic!
Hivi Lile tukio la kukaidi maagizo ya askari wa usalama bado hawajapata saundi za kutuambia mpaka Leo???....

Si waseme tu kwamba gari ilikua inaendeshwa na kijana wa kazi inapelekwa kuoshwa Kwa hiyo huyo kijana kalikosea sana jeshi ya polisi anatafutwa Kwa udi na uvumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…