Kuna taarifa inasambazwa kwenye mitandao ya Kijamii yenye kichwa cha habari kinachosomeka "ABDUL NA KUNDI LAKE WAMTEKA MWANDISHI WA HABARI WAMNYONGA NA KUMTUPA MTO JANGWANI".
Maandishi hayo yanaonekana kama ilivyo hapo kwenye kiambatisho na pia kinaonekana kitu kinachoelea.
Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi kuwa kitu kinachoonekana kinaelea kiliripotiwa tarehe 27.8.2025 majira ya saa tatu asubuhi kuwa huko Magomeni Mapipa chini ya daraja la Jangwani kuna mwili wa binadanu unaelea.
Maafisa wataalamu wa kuchunguza matukio makubwa wakiwa pamoja na Maafisa wa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji walifika katika eneo hilo na kwa kufuata taratibu zote waliutoa mwili huo kutoka ndani ya maji.
Wakati uchunguzi ukiendelea ndugu wa mtu huyo walipatikana na wakaweza kuutambua mwili huo kuwa ni wa Salehe Shukrani, Mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza mikate, mkazi wa Magomeni Mikumi.
Pia walieleza kuwa, ndugu yao huyo alikuwa na tatizo la kuanguka kutokana na kifafa kilichokuwa kinamsumbua.
Pamoja na maelezo hayo uchunguzi wa kitaalam ulifanyika na mwili haukuwa na alama zote ambazo zilionesha kuwa alishambuliwa au kufanyiwa jambo lolote lile la kumdhui Jeshi la Polisi Tanzania linaendelea kutoa wito kwa Jamii kuzipuuza, kuacha kuzisambaza na kushabikia taarifa za uongo na upotoshaji kama hizo.