Polisi wakanusha tuhuma za Abdul kuua mtu Jangwani

Bado kimya kama hawajaiona!
 
Tufanye kajiua au ana huo ugonjwa wa kuanguka ndo awekwe kwenye kiroba afungwe halafu atupwe?.

Na kwanini wamefunga uwanja wa comment na kwanini wapost kwenye mtandao waliofungia?
 
Kuna
Niulize tu swali jepesi.

Lini polisi waliwahi kukiri kuhusika na matukio hayo?

Bado kimya kama hawajaiona!
Ila sio fair kabisa kuna yule deleva wa serikali aliyempita traffic video yake ikavuja alichukuliwa Sheria mara moja pamoja na kupokonywa leseni yake Tena walimtangaza mara moja... ila hilo la Abdul kama hakuna kilichotokea ukijifanya unakumbushia unatafutiwa KESI ya saizi Yako ama kweli Duniani hakuna haki
 
Hivi mtu mwenye kifafa anajifunga kwenye shuka/kiroba ili akajiangushe kwa kifafa jangwani ili age?
 
Mkuu hebu acha utani.

Hawa watu walitonywa kuna ripoti yao kule UNHRC imekuwa filed mwezi June na ina matukio ya watu 200 waliopotea,kutekwa au kuuwawa tangu 2016 wao wakaona waje na hii kama kujitetea sasa kama kawaida yao wakafunga comments.

Ajabu ni kuwa katika ripoti yao hakuna majina kama Ben Saanane, Azory Gwanda, Leopold Lwajabe, Ali Kibao, Sativa, Shadrack Chaula , Mdude Nyagali na wengine wengi.

Cha kusikitisha ni kuwa Ali Kibao alitekwa mchana kweupe na Mdude alitekwa kwa kuvamiwa na walijitambulisha ni askari sasa wanakosekana vipi kwenye ripoti yao?

Angalia ripoti hiyo ndio utagundua ni geresha tu.


View: https://x.com/tanpol/status/1935339603243733001?t=gSDnsMXsaaViHZ7Hfe9dOQ&s=19
 
Hata kama ni kifafa toleo jipya ndio mtu atafute kiroba ajivalishe ajifunge na kamba halafu ajitupe mtoni??? Basi huu ugonjwa utakua mbaya sana
Nimecheka sana eti kifafa toleo jipya.
 
Kwa maelezo ya walioshuhudia na picha zilizo sambaa mtandaoni mwili haukuwa kwenye kiroba.
Na marehemu alikuwa kavaa jezi mpya za Yanga.
Alikuwa na simu na fedha.
Si alikuwa kwenye kiroba? au ?Sawa alikuwa na tatizo la kuanguka sasa aliingiaje kwenye kiroba?..aliangukia ndani ya kiroba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…