Polisi wakimbizana na Wamachinga Dar

Polisi wakimbizana na Wamachinga Dar

Picha ya ndege polisi wamekuja usiku wakachoma moto meza zote za hawa machinga, mbinu hii hii ifanye kazi kwa dar es salaam hawa watu wamekuwa kero mno mtaani
Hawa wajasiriamali sio wastaarabu mtu mwenye akili zake timamu hawezi shabikia,Mtu anayepanga biashara kwenye njia ya watembea kwa miguu walivyo wa ajabu maganda ya miwa na machungwa wanatupa kwenye mitaro ya maji matokeo ikinyesha mvua maji yanaingia mitaani kati ya kumi ya chinga nina imani wawili tu ndio wenye vitambulisho vya ujasiriamali.
 
kwenye simu unaweka tozo za kufa mtu
mtaani unawafukuza vijana wasipate riziki

Hivi hii serikali inafikiria mara mbilimbili maamuzi yake?
Wewe jamaa mchonganishi sana, inaonesha ni furaha sana kwako unapoona mambo hayaendi sawa ndani ya nchi!! Nchi ikitulia unakereka sana, mlikuwepo watu kama nyinyi Rwanda 1990-1994
 
Msipotoshe....hakuna Biashara isiyo na mpangilio. Kwanini hawataki kwenda maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya biashara ya kimachinga?!
Jamaa mchonganishi sana huyu, hapendi nchi itulie kabisa, amekaa sharishari tu, hawa hawa walikuwa wanamtukana Jiwe kuhusu Machinga, leo hii suala la Machinga linatafutiwa suluhishi watu walewale wanapinga na kuleta uchochezi, Stupid people
 
Msipotoshe....hakuna Biashara isiyo na mpangilio. Kwanini hawataki kwenda maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya biashara ya kimachinga?!
Wewe unadhani kwanini hawataki kwenda huko? Likipatikana jibu la hili, suluhisho haliko mbali.
 
Back
Top Bottom