Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Sina tatizo na suala la kuwa na Katiba mpya, lakini tatizo langu ni kuona watu wakidhani Katiba mpya ndio suluhisho la matatizo ya kisiasa nchini. Huko ni kupotoka. Nchi kama Marekani wana katiba ya kidemokrasia sana, lakini leo wanalia Trump na kundi lake kufanya mambo kihuni tu na kwa mabavu. Na hata wanatumia katiba hiyohiyo ya USA kuvuruga demokrasia ya Marekani.
Kwa hiyo tusidhani kwamba tatizo la kukosekana haki na usawa kwa vyama vya upinzani nchini liko kwenye katiba, hapana. Tatizo ni matumizi mabaya ya madaraka na ubabe tu wa wale wanaokuwa katika uongozi. Tatizo ni kiburi na ulevi tu wa madaraka.
Suala la kujiuliza ni kama uwepo wa Katiba mpya utazuia ubabe na ulevi huo wa madaraka. Labda. Lakini tusisahau kwamba viongozi wetu wametumia ubabe hata katika kukiuka mambo ambayo yako wazi kwenye katiba. Mtu ambaye ni mbabe wa kukiuka katiba iliyopo kwa kuwatumia Polisi, Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya/Mikoa na Usalama wa Taifa katika kuingilia uchaguzi na kuufanya usiwe huru na haki, hawezi kuacha kufanya hivyo kwa sababu kuna Katiba mpya. Na hawaingilii uchaguzi kwa kuwa Katiba iliyopo inawapa mamlaka ya kuingilia uchaguzi.
Kwa hiyo watu wasijikite kwenye suala la katiba mpya peke yake kama wanataka mabadiliko hapa nchini. Kuna njia nyingi za kumchuna mbuzi ili aliwe kitoweo.