Polisi, Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya/Mikoa na Usalama wa Taifa kuingilia uchaguzi kwa amri toka juu ndio kinaharibu, sio Katiba

Mapungufu ya katiba ya sasa ndiyo chanzo cha yote haya. Kwanza katiba hiyo iliandikwa na maccm tangu kuwe na mfumo wa vyama vingi hakujawa na Katiba mpya. Pili kuna mapungufu mengi sana ikiwemo la jinsi Tume ya uchaguzi inavyopatikana, matokeo ya uchaguzi wa Urais hayawezi kupingwa Mahakamani, vyombo vya dola kuachiwa kushiriki kwenye kupora uchaguzi etc.
Katiba ni KIPAUMBELE nambari one ili kuleta HAKI, UHURU na USAWA kwa wote nchini.
Sawa kabisa, nakuunga mkono. Lakini hoja yangu ni kwamba, Katiba mpya sio suluhisho la tatizo la kuvunja Katiba ya sasa au uongozi wa kimabavu na ulevi wa madaraka!

Hadi sasa kilichobadilika ni vyama vingi tu, na hatuwezi kusema tatizo kubwa la Katiba iliyopo ni jinsi inavyoshughulika na uwepo wa vyama vingi
 
Tatizo la vijana wengi hapa tunaokoteza story za vijiweni tunaweka hapa!! Mbinu za CCM ni mbili kubwa ni Sheria zilizoko kwa mlango mkuwa wa Katiba na Pili ni Uelewa wa Wananchi basi , hapa hatuwezi kutoka.
 
Kuna mambo Katiba inahusika. Lakini fikiria zuio la mikutano, hakuna sehemu katiba imezuia mikutano ya kisiasa, lakini mbona inazuiwa japo Katiba inaruhusu?

Katiba ndio ilimruhusu Magufuli kumtuma Sabaya kwenye mission zao zile? Sawa utasema kama Ktiba ingeruhusu Raisi kufunguliwa mashitaka asingefanya vile. Lakini usisahau alifanya kwa siri. Katiba haikuruhusu kuunda kikosi cha Wasiojulikana
Hili zuio ilitakiwa kuwa challenged mahakamani kwa maana ya kwamba mahakama itoe ufafunuzi lakini kwasababu katiba ni mbovu imeshindwa kusepatate mihimili ndo hivyo unakuta neno la raisi linakua sheria hata kama halijaandikwa
 
Sina tatizo na suala la kuwa na Katiba mpya, lakini tatizo langu ni kuona watu wakidhani Katiba mpya ndio suluhisho la matatizo ya kisiasa nchini. Huko ni kupotoka. Nchi kama Marekani wana katiba ya kidemokrasia sana, lakini leo wanalia Trump na kundi lake kufanya mambo kihuni tu na kwa mabavu. Na hata wanatumia katiba hiyohiyo ya USA kuvuruga demokrasia ya Marekani.

Kwa hiyo tusidhani kwamba tatizo la kukosekana haki na usawa kwa vyama vya upinzani nchini liko kwenye katiba, hapana. Tatizo ni matumizi mabaya ya madaraka na ubabe tu wa wale wanaokuwa katika uongozi. Tatizo ni kiburi na ulevi tu wa madaraka.

Suala la kujiuliza ni kama uwepo wa Katiba mpya utazuia ubabe na ulevi huo wa madaraka. Labda. Lakini tusisahau kwamba viongozi wetu wametumia ubabe hata katika kukiuka mambo ambayo yako wazi kwenye katiba. Mtu ambaye ni mbabe wa kukiuka katiba iliyopo kwa kuwatumia Polisi, Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya/Mikoa na Usalama wa Taifa katika kuingilia uchaguzi na kuufanya usiwe huru na haki, hawezi kuacha kufanya hivyo kwa sababu kuna Katiba mpya. Na hawaingilii uchaguzi kwa kuwa Katiba iliyopo inawapa mamlaka ya kuingilia uchaguzi.

Kwa hiyo watu wasijikite kwenye suala la katiba mpya peke yake kama wanataka mabadiliko hapa nchini. Kuna njia nyingi za kumchuna mbuzi ili aliwe kitoweo.
Mkuu hao ulio mention hapo wote vibarua vyao vinatokana na rais lazima wamuheshimu bosi wao na wamsikilize kwa lolote atakalowaambia wafanye

yeye ndiyo amewaweka na anaweza kuwatoa na hata kuwafunga kwa kesi ya hovyo atakayoamua yeye kuwabakizia
Kama wataenda kinyume nae

Lakini kama rais hatakuwa na mamlaka nao ya kuwaweka kazini au kuwatoa watafanya maamuzi sahihi bila kumuhofu huyo Rais na badala yake watahofia kubanwa na sheria tofauti na sasa ambapo wanatokana na rais hivyo na wao outomatic wanakuwa untouchable
Yote hiyo ni katiba
Mfano mdogo ni pale zambia leo tume ilichokifanya

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mleta mada lazima ajue kuwa kwa mujibu wa katiba hii ya sasa almost kila kitu nchini kinarevolve around rais.
Rais ana Kinga ya kutoshtakiwa na ana mamlaka ya kuwafukuza kazi wateule wake wa vyombo vya usalama kadri atakavyotaka, na ana uwezo wa kuinfluence anachokitaka mahakamani kupitia kwa mteule wake huko, yaani DPP
Sasa Raisi anaweza kuamua kushiriki UOVU kwa kuwatumia wateuoe wake wa vyombo vya usalama na akawalinda kwa sababu huwezi kufungua kesi yoyote dhidi yao bila kupitia kwa DPP ambaye ni mteule wa rais, na wala hakuna uchunguzi wowote wa makosa ya Jinai unaweza kufanywa bila serikali kuridhia.
Ila Ukibadili katiba, ukapunguza madaraka ya rais na kuyaweka kwenye taasisi mbalimbali unakuwa unamfunga mikono rais kuabuse power. Chukulia mfano ubadili kitu kimoja tu kwenye katiba, kuwa rais anaweza kushitakiwa kwa makosa ya jinai atakayotenda. Hii itabadili vitu vingi sana vya namna marais wanavyobehave madarakani
 
Hili andiko fupi lakini linanitia moyo kwa sababu huyu mwandishi ni baadhi ya Watanzania wachache wanaofikiri!! Nuru katika giza nene la siku hizi hapa Tanzania. Shukran sana.
 
Mkuu hao ulio mention hapo wote vibarua vyao vinatokana na rais lazima wamuheshimu bosi wao na wamsikilize kwa lolote atakalowaambia wafanye

yeye ndiyo amewaweka na anaweza kuwatoa na hata kuwafunga kwa kesi ya hovyo atakayoamua yeye kuwabakizia
Kama wataenda kinyume nae

Lakini kama rais hatakuwa na mamlaka nao ya kuwaweka kazini au kuwatoa watafanya maamuzi sahihi bila kumuhofu huyo Rais na badala yake watahofia kubanwa na sheria tofauti na sasa ambapo wanatokana na rais hivyo na wao outomatic wanakuwa untouchable
Yote hiyo ni katiba
Mfano mdogo ni pale zambia leo tume ilichokifanya

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Point nzuri sana Mkuu. Ila sasa, hatutakuwa tunaongelea Katiba ambayo inamwondolea madaraka raisi yote ya kuteua? Je tatizo tulilonalo ni raisi kuwa na madaraka ya kuteua au raisi kutumia vibaya madaraka yake? Kuna katiba yeyote duniani ambayo kwa 100% inamzuia raisi kutumia madaraka yake vibaya? Nimetoa mfano wa Trump jinsi alivyotumia madaraka yake vibaya katika mazingira ya Katiba ya USA! Tatizo lilikuwa Trump au Katiba ya USA?
 
Mleta mada lazima ajue kuwa kwa mujibu wa katiba hii ya sasa almost kila kitu nchini kinarevolve around rais.
Rais ana Kinga ya kutoshtakiwa na ana mamlaka ya kuwafukuza kazi wateule wake wa vyombo vya usalama kadri atakavyotaka, na ana uwezo wa kuinfluence anachokitaka mahakamani kupitia kwa mteule wake huko, yaani DPP
Sasa Raisi anaweza kuamua kushiriki UOVU kwa kuwatumia wateuoe wake wa vyombo vya usalama na akawalinda kwa sababu huwezi kufungua kesi yoyote dhidi yao bila kupitia kwa DPP ambaye ni mteule wa rais, na wala hakuna uchunguzi wowote wa makosa ya Jinai unaweza kufanywa bila serikali kuridhia.
Ila Ukibadili katiba, ukapunguza madaraka ya rais na kuyaweka kwenye taasisi mbalimbali unakuwa unamfunga mikono rais kuabuse power. Chukulia mfano ubadili kitu kimoja tu kwenye katiba, kuwa rais anaweza kushitakiwa kwa makosa ya jinai atakayotenda. Hii itabadili vitu vingi sana vya namna marais wanavyobehave madarakani
Mkuu nakuelewa sana, lakini bado hujaelewa thread yangu. Unaeleza mambo mengi ambayo ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwa katiba inampa madaraka raisi kupita kiasi, na tukiwa na raisi asiye na busara atatumia mwanya huo. Lakini ni katiba hiyo hiyo ambayo ilitumika kwa Mwinyi, Mkapa na Kikwete, na hatukuwa na matatizo hayo.

Point yangu hasa ni hii, labda niiseme moja kwa moja; je, upinzani wanakuwa sahihi pale ambapo wanadhani ni mabadiliko ya Katiba tu ndio yanaweza kuwaweka katika kuchukua hatamu za uongozi?

Kumbuka kuna wakati Augustine Mrema kidogo ashinde uraisi, na bila Nyerere Mrema ngekuwa raisi. Nyerere hakutumia katiba vibaya ili Mrema ashindwe na Mkapa uchaguzi wa uraisi.
 
Point nzuri sana Mkuu. Ila sasa, hatutakuwa tunaongelea Katiba ambayo inamwondolea madaraka raisi yote ya kuteua? Je tatizo tulilonalo ni raisi kuwa na madaraka ya kuteua au raisi kutumia vibaya madaraka yake? Kuna katiba yeyote duniani ambayo kwa 100% inamzuia raisi kutumia madaraka yake vibaya? Nimetoa mfano wa Trump jinsi alivyotumia madaraka yake vibaya katika mazingira ya Katiba ya USA! Tatizo lilikuwa Trump au Katiba ya USA?

Issue siyo kumuondolea rais mamlaka yoote kabisa ya kuteua hapana lakini inabidi haya mamlaka yapunguzwe sana

Matatizo tunayo mengi lakini moja kubwa ni pamoja na haya mamlaka ya kuteua

Rais ana mamia ya watu wa kuteua kama siyo maelfu kinachotokea ni nini ndugu,
Marafiki, classmates, schoolmates, wanakijiji wenzie, kabila lake ndiyo wanajaa kwenye serikali yake siyo nje ya hapo
haya yote hayawezi kuzingatia sana taaluma na weledi
Matokeo yake ni kushindwa kuwajibishana makosa yanapofanyika
Serikali inakuwa ya hovyo tu

Tukifanya kinyume na hivi watu watawajibishana huko serikalini hakutakuwa na kuogopana wala kuonekana aibu kama mtu akikosea

Matumizi mabaya ya madaraka yapo na yanatokana na mtu mwenyewe
Lakini akiwa na limit ya baadhi ya mambo hatoleta madhara makubwa kwa taifa

Huyo Trump unayemsema amefeli kwenye mambo mengi ya hovyo aliyotaka kufanya kwa sababu ya katiba yao kuwa strong
Leo hii wangekuwa na katiba ya Tanzania ni wazi kwamba Trump angekuwa ikulu mda huu

Katiba mpya inaweza kuangalia upya vigezo vya mtu kuwa rais
Ili chama kimsimamishe mgombea inabidi awe na vigezo vya kutosha ikibidi serikali iwe inasimamia hilo jambo kujua historia zao elimu zao kupima afya zao wagombea wote wa nafasi ya rais hata wagombea wenza pia wawe na vigezo kamili anavyotakiwa kuwa navyo rais
Hii itaondoa mihemko binafsi kuendesha nchi lakini hata kwa baadhi ya mambo ambayo rais ana mamlaka nayo hawezi kuyafanya hovyo kwa sababu yuko pale ni mtu smart

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo katiba mpya itafanya kichwa chako kiume? Ama ajira yako kukoma? Mbona ukisikia katiba mpya moyo wako unadunda?
Sina tatizo na suala la kuwa na Katiba mpya, lakini tatizo langu ni kuona watu wakidhani Katiba mpya ndio suluhisho la matatizo ya kisiasa nchini. Huko ni kupotoka. Nchi kama Marekani wana katiba ya kidemokrasia sana, lakini leo wanalia Trump na kundi lake kufanya mambo kihuni tu na kwa mabavu. Na hata wanatumia katiba hiyohiyo ya USA kuvuruga demokrasia ya Marekani.

Kwa hiyo tusidhani kwamba tatizo la kukosekana haki na usawa kwa vyama vya upinzani nchini liko kwenye katiba, hapana. Tatizo ni matumizi mabaya ya madaraka na ubabe tu wa wale wanaokuwa katika uongozi. Tatizo ni kiburi na ulevi tu wa madaraka.

Suala la kujiuliza ni kama uwepo wa Katiba mpya utazuia ubabe na ulevi huo wa madaraka. Labda. Lakini tusisahau kwamba viongozi wetu wametumia ubabe hata katika kukiuka mambo ambayo yako wazi kwenye katiba. Mtu ambaye ni mbabe wa kukiuka katiba iliyopo kwa kuwatumia Polisi, Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya/Mikoa na Usalama wa Taifa katika kuingilia uchaguzi na kuufanya usiwe huru na haki, hawezi kuacha kufanya hivyo kwa sababu kuna Katiba mpya. Na hawaingilii uchaguzi kwa kuwa Katiba iliyopo inawapa mamlaka ya kuingilia uchaguzi.

Kwa hiyo watu wasijikite kwenye suala la katiba mpya peke yake kama wanataka mabadiliko hapa nchini. Kuna njia nyingi za kumchuna mbuzi ili aliwe kitoweo.
 
Issue siyo kumuondolea rais mamlaka yoote kabisa ya kuteua hapana lakini inabidi haya mamlaka yapunguzwe sana

Matatizo tunayo mengi lakini moja kubwa ni pamoja na haya mamlaka ya kuteua

Rais ana mamia ya watu wa kuteua kama siyo maelfu kinachotokea ni nini ndugu,
Marafiki, classmates, schoolmates, wanakijiji wenzie, kabila lake ndiyo wanajaa kwenye serikali yake siyo nje ya hapo
haya yote hayawezi kuzingatia sana taaluma na weledi
Matokeo yake ni kushindwa kuwajibishana makosa yanapofanyika
Serikali inakuwa ya hovyo tu

Tukifanya kinyume na hivi watu watawajibishana huko serikalini hakutakuwa na kuogopana wala kuonekana aibu kama mtu akikosea

Matumizi mabaya ya madaraka yapo na yanatokana na mtu mwenyewe
Lakini akiwa na limit ya baadhi ya mambo hatoleta madhara makubwa kwa taifa

Huyo Trump unayemsema amefeli kwenye mambo mengi ya hovyo aliyotaka kufanya kwa sababu ya katiba yao kuwa strong
Leo hii wangekuwa na katiba ya Tanzania ni wazi kwamba Trump angekuwa ikulu mda huu

Katiba mpya inaweza kuangalia upya vigezo vya mtu kuwa rais
Ili chama kimsimamishe mgombea inabidi awe na vigezo vya kutosha ikibidi serikali iwe inasimamia hilo jambo kujua historia zao elimu zao kupima afya zao wagombea wote wa nafasi ya rais hata wagombea wenza pia wawe na vigezo kamili anavyotakiwa kuwa navyo rais
Hii itaondoa mihemko binafsi kuendesha nchi lakini hata kwa baadhi ya mambo ambayo rais ana mamlaka nayo hawezi kuyafanya hovyo kwa sababu yuko pale ni mtu smart

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Basi jambo la msingi sana ni Watanzania wote kuelewa kwamba suala la mabadiliko ya Katiba ni zaidi ya kuvipa vyama vya upinzani wigo wa kushinda uchaguzi. Na inakuwa kosa sana kwa vyama vya upinzani kuunganisha haya mawili - kwamba wanapotaja katiba mpya ni pale tu wanapolalamikia mambo ya kuonewa katika uchaguzi. Viongozi wa hivi vyama vya upinzani wana jukumu la kuwaonyesha Watanzania kwamba katiba mpya ni zaidi ya uhuru na haki katika uchaguzi.

Ndio maana nikasema hapo juu kwamba wakati Mrema anaelekea kushinda kiti cha uraisi kupoitia NCCR Mageuzi na Nyerere akafanya kila njia kuzuia hilo, Nyerere hakutumia vibaya Katiba, bali alitumia mbinu za kikampeni kumshinda Mrema. Na hiyo ndio theme ya thread yangu
 
Jielimishe kidogo ndugu. Hauwezi kutenganisha katiba na hilo ulilolitaja hapo juu. Katiba inayotoa udhabu kwa wavunjaji itakuwa na nguvu. Usione CCM wanapinga. Wanalijua hilo...
Kama huna la maana la kusema si ukae kimya tu? Unaona raha kutukanwa?
 
Katiba yetu ina matatizo makubwa.

Kiini cha matatizo yetu mengi yanaanzia kwenye katiba .
 
Jielimishe kidogo ndugu. Hauwezi kutenganisha katiba na hilo ulilolitaja hapo juu. Katiba inayotoa udhabu kwa wavunjaji itakuwa na nguvu. Usione CCM wanapinga. Wanalijua hilo...
Na hilo ndilo wapinzani nitawalaumu siku zote. Manaongelea Katiba mpya pale tu mnapolalamikia ukosefu wa usawa na haki katika uchaguzi. Nimewakumbusha kwamba nchi hii, kwa katiba hii hii, ilitaka kuandika histria ya Mrema kuwa raisi wa kwanza kutoka upinzani. Kwa hiyo hata kama mnataka wananchi wengi waunge mkono suala la katiba mpya, msifanye uchaguzi kuwa jambo kubwa la Katiba mpya. Kuna mengi ya kuvutia watu kuunga mkono jitihada za Katiba mpya kuliko Raisi kuamrisha wakurugenzi kusimamia uchaguzi
 
Mkuu, unapingana na kilichoandikwa hapa?
Hata Diallo alikiongelea hicho! Hata katiba iwe nzuri kiasi gani, mtawala anaweza kuikanyaga tu!
Kule Zenji kulikuwa na Tume huru, lakini CCM kwa kumtumia Jecha, akafanya yake. Alifanywa nini? Nakubalina na mleta uzi huu, kwa 100%.
mzee wacha bangi toka lini Zanzibar kukawa na tume huru chini ya ccm
 
Achana nae huyu. Hawa ndio wanaotaka kuwapotosha kina Mbowe kwamba jibu la matatizo yao liko kwenye Katiba mpya. Zambia wapinzani walinyanyasawa sana na serikali ya Lungu, lakini wameshinda bila Katiba mpya. Nadhani kina Mbowe hawapaswi kusahau kwamba wasielekeze nguvu zote kwenye Katiba
Mkuu,acha tuipate kwanza angalau watawala atakuwa na hofu na si kuichezea katiba wanavyotaka kimsingi hapa hakuna katiba kuna mfano wa katiba,Nyerere alisema katiba hii ikimpata raisi kichaa atakuwa dikteta hiyo sasa ni nini??umetoa mfano wa Zambia ulisha sikia Zambia wanahitaji katiba mpya??hujasikia juzi hapa Lungu alitaka kwenda mahakamani kupinga matokeo??hapa je inaruhusiwa kupinga matokeo ya uraisi mahakamani baada ya tume kutangaza??Acha tuipate kwanza hayo mengine ni ya kufikirika tu yakitokea kwingine si lazima yatokee hapa.
 
Back
Top Bottom