Polisi, Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya/Mikoa na Usalama wa Taifa kuingilia uchaguzi kwa amri toka juu ndio kinaharibu, sio Katiba

Huo ndio ubovu wenyewe wa katiba.
Ingelikuwa katiba iko sawasawa hayo maagizo toka juu na wapokea maagizo kila mmoja angejua na kutimiza wajibu wake.
 
Hapo ndipo hamjaelewa! Jacha ni zao la katiba inayopigwa! Alipatikanaje kuwa mkurugenzi wa uchaguzi.. mmoja wa washidani ndie anamteua msimamizi!!!.....
 
Hata kwa katiba hiihii zikitolewa kinga za viongozi waliopo madarakani na wasitaafu itatufaa tu.
Kama tunasubiri katiba mpya baada ya 2025 basi ipelekwe hoja ya dharula kufuta hiyo sheria.
 
Uko sawa Mkuu! Kama bado Rais yuko juu ya Katiba hata tungepata Katiba kutoka wapi! Kama Rais hawezi kushitakiwa kwa kutumia madaraka vibaya au kukanyaga Katiba bado safari ni ndefu.
 
Umesema vema. Lakini kumbuka Katiba mpya inaandamana na Tume Huru ya Uchaguzi, ambayo haiwajibiki kwa Rais wala hao viongozi wa Serikali katika ngazi nyingine. Kenya, Malawi na Zambia iliwezekana mpaka Incumbent President anasema Tume imemwonea
 
Huo ndio ubovu wenyewe wa katiba.
Ingelikuwa katiba iko sawasawa hayo maagizo toka juu na wapokea maagizo kila mmoja angejua na kutimiza wajibu wake.
Mkuu, sio kila jambo la kijinga na ovyo linalotendeka nchini suluhisho lake litapatikana katika katiba. South Africa wana katiba ambayo ni moja wapo ya most democratic constitutions in the world, lakini bado wana mambo ya kijinga sana katika uongozi kwa sababu tu ANC ni chama kikongwe
 
Umesema vema. Lakini kumbuka Katiba mpya inaandamana na Tume Huru ya Uchaguzi, ambayo haiwajibiki kwa Rais wala hao viongozi wa Serikali katika ngazi nyingine. Kenya, Malawi na Zambia iliwezekana mpaka Incumbent President anasema Tume imemwonea
Tukipata tume huru na katiba mpya, na CCM au Chadema au TLP ni wale wale, unafikiri itatupa uhakika wa mjinga mwingine kutuharibia nchi? Ndio maana nikauliza, katiba ya USA ina tatizo gani? Lakini mbona ilileta kiongozi aliezua taharuku kali sana huko? Katiba ya South Africa ina tatizo gani? Lakini mbona bado inatoa viongozi wabovu na poor social services huku kundi kubwa la wananchi likiwa kwenye umasikini mkubwa miaka zaidi ya 20 toka wapate katiba iliyosemwa ni one of the best in the world?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…