GE2025 Polisi wamefika kwa ajili ya kutawanya Wananchi waliofunga barabara Kata ya Terati, jijini Arusha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wananchi wa Kata ya Terati, jijini Arusha, leo Julai 6 wamefunga barabara ya Mapambazuko wakipinga uteuzi wa mgombea udiwani wa CCM, Julias Lenina, ambaye amemaliza muda wake, lakini jina lake limeteuliwa tena kuwa miongoni mwa watakaopitishwa kuwania nafasi hiyo.

Wakieleza sababu za hatua hiyo, wananchi hao wamesema katika kipindi cha miaka Mitano hakuna kitu ambacho amekifanya, kwahiyo hawakubaliani na uteuzi huo wakidai haukuzingatia matakwa yao, na kwamba mgombea huyo hana uungwaji mkono kutoka kwa jamii.

Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio kwa lengo la kuhakikisha usalama na kutawanya watu waliokuwa wamezuia barabara, ili kurejesha hali ya kawaida.

Wananchi hao wamesema kuwa majina matatu yaliopitishwa kwenda wilayani mojawapo ni la mwenyekiti wa mtaa wa Olkung'u ambaye akimuona diwani ambaye amemaliza muda wake na anagombea tena ni mjomba wake na mwingine ni rafiki yake hivyo wamewekwa tu kama kiini macho kwa lengo la kumrudisha tena Lenina ambaye hawamtaki.

Kwa upande wa Julias Lenina ambaye alikuwa diwani na anagombea tena tulipozungumza naye kwa njia ya simu kuhusu tuhuma za kuhonga kamati ya kata ili apitishwe jina lake amesema siyo kweli ni watu wanamzushia uongo.

Mama anapokanyaga ardhi ya mataifa, anabeba heshima ya Tanzania, anatangaza amani, na anaonyesha uongozi wa hekima unaoheshimika kimataifa. Ziara yake ni ishara ya mshikamano wa kweli wa Afrika.
#KaziNaUtu
#TunasongaMbele
 
We uko nje ya point
Sijakosea nilichoandika, hao wananchi wako sahihi maana atakuwa diwani wao watake wasitake akishapitishwa na chama, maana hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Wananchi wa Kata ya Terati, jijini Arusha, leo Julai 6 wamefunga barabara ya Mapambazuko wakipinga uteuzi wa mgombea udiwani wa CCM, Julias Lenina, ambaye amemaliza muda wake, lakini jina lake limeteuliwa tena kuwa miongoni mwa watakaopitishwa kuwania nafasi hiyo.

Wakieleza sababu za hatua hiyo, wananchi hao wamesema katika kipindi cha miaka Mitano hakuna kitu ambacho amekifanya, kwahiyo hawakubaliani na uteuzi huo wakidai haukuzingatia matakwa yao, na kwamba mgombea huyo hana uungwaji mkono kutoka kwa jamii.

Kutokana na hali hiyo, Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio kwa lengo la kuhakikisha usalama na kutawanya watu waliokuwa wamezuia barabara, ili kurejesha hali ya kawaida.

Wananchi hao wamesema kuwa majina matatu yaliopitishwa kwenda wilayani mojawapo ni la mwenyekiti wa mtaa wa Olkung'u ambaye akimuona diwani ambaye amemaliza muda wake na anagombea tena ni mjomba wake na mwingine ni rafiki yake hivyo wamewekwa tu kama kiini macho kwa lengo la kumrudisha tena Lenina ambaye hawamtaki.

Kwa upande wa Julias Lenina ambaye alikuwa diwani na anagombea tena tulipozungumza naye kwa njia ya simu kuhusu tuhuma za kuhonga kamati ya kata ili apitishwe jina lake amesema siyo kweli ni watu wanamzushia uongo.

Safi wana-Arusha ndio tunaanza ile kazi hivyo.
 
Wanamkataa ccm ila bado wanamtaka ccm mwingine, so hawa hawachagui chama, wanachagua mtu?

Wapinzani wakiwa welevu jimbo hilo nje nje
 
Back
Top Bottom