LGE2024 Polisi wamkamata na kumuweka Lock up Steven Membe, Mwanachama wa CHADEMA, nyumbani kwao Rondo

LGE2024 Polisi wamkamata na kumuweka Lock up Steven Membe, Mwanachama wa CHADEMA, nyumbani kwao Rondo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Yericko Nyerere ameandika;

Jeshi la Polisi limemkamata Kamanda wetu Mwanachama wa Chadema Mhe. Steven Kamilius Membe nyumbani kwao Rondo na kumuweka Lock up ya Kituo kikubwa cha Polisi Lindi Mjini.

Bado hakuna uwazi wa makosa wanayomshikilia nayo. Tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu sana. Ila mtoa taarifa wetu ambaye ni Mtoto wake ametueleza Chadema Kusini kwamba wanamshilia kwa masuala ya kisiasa kutokana na hoja nzito alizotoa kwa wananchi siku ya Mkutano wa Chadema wa uzinduzi wa Kampeni za chaguzi wa serikali za mitaa.

Pia, Soma: Kukamatwa viongozi wa CHADEMA, Polisi wadai "CHADEMA walikaidi amri ya Askari, walirusha mawe na kujeruhi Askari"

Aidha inasemekana ni agizo la Viongozi wa CCM wa Kata na Wilaya kuhakikisha anawekwa ndani ili kufifisha Kampeni za CHADEMA kule Rondo.

Taarifa na Chadema Kanda ya Kusini
IMG_0881.jpeg
IMG_0880.jpeg
 
Mashetani CCM yanaendelea na uovu wao. Adui mkubwa wa kila kilicho chemanchihii ni CCM.
Tunaomba mkono wa BWANA ukawafikie wote wanaotumia madaraka kudhulumu haki za watu. Hakika nimeapa, wadhulumaji wote watauona ukuu wa Bwana, asema BWANA.WA

Waovu hawa hata wakiyapata madaraka, kamwe hawataionja furaha maana nyumba zao zimelaanika. Wala wasishangae.
 
Hao polisi waache haki-asilia itendeke na demokrasia itawale. Chadema wakiingia madarakani 2024 na urais 2025 hawatalipa kisasi Kwa matendo maovu waliyoyatenda ccm huko nyuma . Chadema watasamehe na kuongoza nchi kuelekea mwelekeo mpya kwa faida ya watanzania wote .

Ccm acheni kuogopa mabadiliko. Acheni kuyahofia mabadiliko. Mabadiliko hayaepukiki.
 
Yap
 
Back
Top Bottom