Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Naunga mkono hoja hiyo yote ni kuziua tupate muda mwingi kujadili ujinga
Tunajua kutumia miguvu mingi kwa masuala yasiyo ya msingi wakati wenzetu wanakata kauli chini ya kifusi kwakweli inaskitisha sana , narudia tena nchi hiyo ina laana flani hivi
 
Kutaka Kiki tu, kwanini asingetoa mchango yeye kama yeye?
Asante mzeiya, hata mimi nimewaza hivi hivi, mm naona Niffer anavopost mtandaoni kuwa ana pesa nyingi, like anamiliki range 2 plate no jina lake, trip to Dubai etc,

Kwa social media status aliyonayo Niffer angetoa tsh million 10 au hata million 2 tu, au bidhaa zenye thamani ya hela hiyo, a post kwenye wall yake ili awa inspire followers wake mtandaoni wachangie walio kwenye maafa, vijana wenye hela kama kina b lord kule Nigeria ndo wanafanyaga ivo mara moja Moja wanaenda mahali Wana-donate hata $50,000

Kilichomkuta Niffer nafikiri ni matokeo ya mtu kujionesha una hela nyingi kumbe kiuhalisia mfukoni ni apeche alolo unapumulia mashine, almost kila tukio unaona fursa
G - The Apostle MastaKiraka reymage cocochanel Miss Natafuta Nifah
 
Well said, solution ni simple kama hiyo uliyoongea, wakiendelea kumweka Niffer lockup, labda Watakua na Yao mengine, ils polisi wengi wa tz walivyo na njaa huenda watamtaftia na makosa mengine ili wamtoe hela Logikos
 
Key word- WIVU. Hauwezi ukawasikia strongly wakiichambua serikali inavyokalia kimya(inavyowalinda) au inavyowafuga watekaji. Toka Jiwe aanzishe(yes JIWE) utaratibu wa kuteka mpaka sura za watekaji(popularly WASIOJULIKANA) zinakuwa published mitandaoni huku wakikanwa na polisi hutawasikia hao chawa wakivalia njuga suala hilo.
 
Ana maduka kibao na hzo mall za mchongo, kwann asingetoa hela yake yy kama yy, awachangie waathirika. Ule ulikuwa ni upigaji.
Umewaza kama mimi nlivowaza, ndo shida ya kujionesha mtandaoni kuwa una pesa nyingi kumbe kiuhalisia ni apeche alolo Geok
 
Nchi ya Tanzania na maajabu yake, hako kabinti ndiyo kamekuwa most wanted kwenye sakata la kuporomoka ghorofa au ndiyo njia ya ku-divert attention ili Engineers, Construction company na mmiliki wa jengo wasiguswe?
 
Anadeal nao kimya kimya relax
Mbona huyo binti haku-deal naye kimyakimya?
Na wale watekaji walioonekana live ana-deal nao kimyakimya?
Kwanini hajawahi kutoa kauli za kwamba watekaji wakamatwe kwani sura zao si zimeonekana live?
Kama ameweza(imempendeza) kutoa kauli ya kukamatwa huyo binti angetoa kauli kali zaidi ya kukamatwa wahusika wa maafa kuanzia msanifu wa jengo, Engineers na Company(companies) zilizohusika kujenga na kusimamia ujenzi wa ghorofa hilo lililoanguka.
Amejua kauli ya kumkamata huyo binti itaenda viral naye stupidly akaona aende nayo, huyo Kasimu awe anatumia akili japo kidogo kama ameamua kuwa kiongozi wa matamko aanze kutamka kukamatwa kwa watu wanaotishia amani raia na wanaoteka na kuua raia pamoja na watu 'wanaopotea' wakiwa mikononi mwa polisi.
Simple issue kama hii yangetoka tu maelekezo kuwe na transparency na pesa zielekezwe kwenye mfuko upi, stupid Kasimu.
 
Huyu binti achunge sana, waliompandisha wanaenda kumshusha na kumchakaza sana kuna waya kakanyaga mahali.
Haijui hii nchi. Ukisa na vibiashara vyako usijikweze sana eti una hela. Watakuundia zengwe hutakaa uamini. Kuna dada mmoja alikuwaga almaarufu anaagiza bidhaa China kwa pesa za wateja, alichokipata hatasahau. Kakimbia mji umaarufu kwisha. Wapo wanawake wana biashara kubwa tu na hatuoni wakijikweza.
Halafu kama una hela , toa zako halafu hamasisha watu waunge mkono. Sio unaokoteza tu elfu twa Watanzania halafu unajitapa una moyo wa kujali.
Wapo wato maarufu kibao na wana hela lakini sijaona wakiwa na kiherehere .
 
Waamiliki tu wa jengo,waandisi mpaka sasa kimya
Nguvu kubwa imepelekwa kuwakamata hao tu

Ova
 
Tunajua kutumia miguvu mingi kwa masuala yasiyo ya msingi wakati wenzetu wanakata kauli chini ya kifusi kwakweli inaskitisha sana , narudia tena nchi hiyo ina laana flani hivi.
Nguvu Gani Nyingi imetumika Hapo? Si ameenda Mwenyewe Polisi

Nchi ina miongozo yake na Sheria zake. Hata Wewe sasa hivi huwezi kwenda Hospitalini ukaanza Kugawa Sabuni na Sukari kwa Wagonjwa Lazima Utakamatwa Tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…