Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Nilichokiona ni tumeenda haraka sana, nafikiri Mkuu angesema tu wote waliochangisha wawasilishe kwenye kamati ya maafa. Nimeona dada alikuwa wazi sana kusema kiasi alichokipata hadi ule wakati.

Ila na yeye dada alikosea namna ya kuukabili huu upepo, sijui kile kitabu cha 48 Laws alichosema anakisoma kimemsaidia nini kwenye huu upepo. Au yalikuwa maigizo tu.
 
Huwezi kupewa 'agizo' na mamlaka za kiserikali then ukaja kujibu mitandaoni huku ukijinasibu una jeshi nyuma yako. Pesa, mafanikio & nyota njema bila akili za kawaida (Common sense) ni sifuri. BTW Hatosumbuliwa sana ila ataipata elimu kwa njia ngumu kutokana na kutokuchunga mdomo/mikono yake. Hata huko tunapoiga demokrasia na uhuru wa kutoa maoni unapoombwa/agizwa na mamlaka za kiserikali juu ya jambo fulani huwezi kujibu kuwa una 'jeshi kubwa nyuma yako' na hata serikali inajua. Unaweza ukaitukana Serikali kadiri utakavyo lakini kamwe usijaribu 'kuitishia'.
Amejichanganya sana hapa.
 
Naona umefurahiiii sana mkuu. Tupe kisa kimoja tu cha "nchi za wenzetu" kama hiki cha kwetu ambapo raia alifunzwa kwa namna hii.
 
Hivi kweli kulikuwa na haja ya kumsafirisha? Wameshindwa kufanya nae mahojiano akiwa Dodoma, sio matumizi mabaya ya kodi zetu haya? Haya mambo mengine yanashangaza. Sasa nini maana ya kuwa na makao makuu Dodoma? Au ilitakiwa aje aonenane na Waziri mkuu? Sioni logic ya jambo hili, labda kama kuna mtu alie elewa sababu/na umuhimu wa kumsafirisha atuambie.
Na wewe .....tumia logic basi.......yeye yupo Dodoma amekusanyaje pesa ya wahanga akiwa Dodoma....kama sio utapeli ni nini?😀
 
Tunajua kutumia miguvu mingi kwa masuala yasiyo ya msingi wakati wenzetu wanakata kauli chini ya kifusi kwakweli inaskitisha sana , narudia tena nchi hiyo ina laana flani hivi.
Wapi nguvu imetumika?........jiongeze wewe....maafa yapo Dar es salaam yeye yupo Dodoma anachangisha......huo ni utapeli 😀 😀
 
Jeshi la Polisi limemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam mfanyabiashara wa mtandaoni, Jenifer Jovin maarufu Niffer baada ya kujisalimisha polisi jana.

Mfanyabiashara huyo alijisalimisha kwa Jeshi la Polisi jana baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza Jeshi hilo kumhoji kwa kosa la kukusanya fedha za michango kwa ajili ya waathirika walioporomokewa na ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam bila kibali.
Pia, Soma:

Jengo hilo liliporomoka Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo vya watu 16, majeruhi 86 na uharibifu wa mali za mamilioni ya fedha.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 19, 2024 jijini Dodoma, Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Anania Amo amesema Niffer amekamatwa na polisi baada ya kujisalimisha jana.

“Alijisalimisha jana baada ya kumtafuta, tayari tumemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam,”amesema.

Credit: Mwananchi
Ni upuuzi tupu.

A good Police Officer is only a dead Police Officer!

Mimi nilidhani Jeshi la Polisi limewafikisha Mahakamani Watu waliosababisha ajali hii ya kuporomoka kwa jengo na kuua Watu!
 
Jeshi la Polisi limemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam mfanyabiashara wa mtandaoni, Jenifer Jovin maarufu Niffer baada ya kujisalimisha polisi jana.

Mfanyabiashara huyo alijisalimisha kwa Jeshi la Polisi jana baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza Jeshi hilo kumhoji kwa kosa la kukusanya fedha za michango kwa ajili ya waathirika walioporomokewa na ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam bila kibali.
Pia, Soma:

Jengo hilo liliporomoka Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo vya watu 16, majeruhi 86 na uharibifu wa mali za mamilioni ya fedha.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 19, 2024 jijini Dodoma, Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Anania Amo amesema Niffer amekamatwa na polisi baada ya kujisalimisha jana.

“Alijisalimisha jana baada ya kumtafuta, tayari tumemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam,”amesema.

Credit: Mwananchi
"Namuagiza waziri mkuu na hili nalo akaliangalie"
 
Kwahio tunatumia nguvu kazi, kodi zetu na muda wa kudeal na haya mambo ya maafa yamechukua second fiddle...

Haya mambo ni rahisi sana angepewa tu akaunti namba ya kuweka kwenye mfuko wa maafa akapewa shukrani zake na kuwaambia wengine ili kuepuka utapeli na wizi kama kuna kitu kama hiki wakifanye officially...
 
Kutaka Kiki tu, kwanini asingetoa mchango yeye kama yeye?
Huyu binti nimetafakari alipoanzia nikaona ilikuwa hivi:
1. Aliwaza peke yake "Ngoja nitume mchango kwa ajili ya maafa ya mporomoko wa Ghorofa Kariakoo.
2. Akamshirikisha mwenzi, " Nataka nitume hela kuchangia wenzetu waliobanwa kwenye vifusi Kariakoo. "
3. Mwezie akamuumga mkono.
4. Mwezie naye akamtaarifu jirani yake " jamani tunakusanya hela tuzitume Dar kwa walio athirika na maporomoko ya Ghorofa.
5. Wachangiaji wakaongezeka tena na tena na tena.
6. Awali alikuwa mmoja kwa nia njema baada ya muda wakawa wengi kwa nia njema kabisa.
7. Tatizo ni RUKSA HAWAKUPATA.
8. Bila shaka hela zote walizokwisha zichangisha wanazo wakizitoa zote bila kubakiza senti moja mmuachie hakuwa na nia mbaya.
9. Wakimtia ndani wakamfungulia mashitaka huyu binti watakuwa wamekosea kabisa moyo wa kujitolea utakuwa umefifishwa kwa amri ya serikali.
10. Binti kama alikusudia kuiba angefanya kimya kimya, kakini alijiweka wazi. " Tulipoona anachangisha bila kibali tusione yeye ni Mwizi" Binti asamehewe baada yabkuonywa hakuwa nania mbaya kwa mtazamo wangu.
 
Anaitwa binti, kwani hajaolewa na hana mtoto? Nifter kajipatia umaarufu zaidi kupitia janga. Wanamkamata kwani kuna kosa kukusanya michango kwa ajili ya wahanga wa janga hilo. Sasa kama serikali ilichelewa kufanya hivyo why wasamaria wema wasifanye hivyo? Itungwe sheria ya msamaria mwema
 
Back
Top Bottom