Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Huyu dada inaonekana kama ana maadui wengi sasa sijui ni fitna au wivu tu juu yake au ni nini?
Maana nimesikia leo kioind wasafi radio akina zembwela na kitenge wanamkalia kooni haswa mpaka nikajiuliza ,shida ni hii hii michango au labda kuna mengine?
Wivu WATANZANIA tunachuki sana, ata kama kafanya makosa ilitakiwa apewe elimu jinsi na sio kushambuliwa Serikali ilivyoona anachangisha wao wange zilinda pesa kwa kuzizuia zisitoke yani zingekua zinaingia tu.
 
Nilichokiona ni tumeenda haraka sana, nafikiri Mkuu angesema tu wote waliochangisha wawasilishe kwenye kamati ya maafa. Nimeona dada alikuwa wazi sana kusema kiasi alichokipata hadi ule wakati.

Ila na yeye dada alikosea namna ya kuukabili huu upepo, sijui kile kitabu cha 48 Laws alichosema anakisoma kimemsaidia nini kwenye huu upepo. Au yalikuwa maigizo tu.
Mimi hata sijaona ubaya wa kuchangisha pesa mara mia pesa yangu ipitie kwa niffer maana nitakua na uhakika itawafikia wahanga kuliko kwa hao mafisadi wa ccm
 
Kujifunza nini!!! Kosa limefanyika wange muelimisha wamuachie. Jeshi lipo na serikalini ndio inajichemsha zaidi na zaidi.

Nyota Nyota anayo Niffer.

Atayavuka haya, pesa si wachukue tu haraka wakazile sio kumsumbua mtoto wa watu.
Wakazile ivoo.
Na hiko ndio kilichowauma. Wanaona vp wao wakose chochote
 
Wazungu kila leo wanachangisha mabilioni kwa ajili ya watu weusi na utapeli mwingi
Kila mtu anaomba awe na charity eti anasaidia Africa
Huku Ulaya mpaka matapeli yamejaa sasa, wanachapisha mifuko wanaandikia Saidia wanaohitaji Africa nguo

Wanatuletea mpaka majumbani mifuko tuijaze nguo, mikanda, viatu nk
Kumbe ni biashara za watu zikifika huko mtu kanunua na anauza hakuna cha bure

TV Ulaya matangazo kila saa kuhusu watoto wanaokufa kwa kunywa maji machafu na maradhi mengi
Halafu wanasema please donate $20 itasaidia kutibu watoto 5
Hizo hela hazifiki zote bali asilimia ndogo sana sana
Sasa na huyu nae angefanikisha kuchangisha hata 20m unadhani angepeleka wapi?
Huu ni utapeli kama utapeli mwingine
Halafu viongozi wetu kutwa kuwainamia wazungu badala ya kuwapa ukweli na kusema sisi sio mradi au sehemu ya kupatia hela kwa kutudhalilisha
Yaani ukiona jamaa wazungu wanavyotajirika na wengine mpaka kujifanya wanafungua sehemu za kulelea watoto sasa nenda kaone mswahili kaachiwa watoto anavyowanyanyasa halafu hata nguo hawapi anaenda omba tshirt za Chama ndio wanavalishwa, ndio nimeona watoto yatima wamevishwa
Hao ilikuwa wawe na nguo za maana tena smart ila ndio hivyo ni miradi ya watu wasiokuwa na Utu kwa muafrika
Najua nimevuka sana hii mada ila similarities ni hizo hizo
 
Mimi katika hili nadhani hakukuwa na haja kabisa kutokea lingefanyika ki busara kwa maana mtuhumiwa hakuwa anachangisha kimya kimya ni wazi hakujuwa kisheria ni kosa sasa elimu na hatua ingechukuliwa labda kuhamisha michango yote kwenye sehemu husika lakini kufanya conference kama wamefanya kosa kubwa sana lakini watu tunaodhani leo hii wangefanyiwa hayo mwenye jengo, watoa vibali na mhandisi aliyekuwa anafanya kazi hawa ndio walikuwa wawepo ndani kusaidia police. Anyway nchi hii usije kushangaa kuna vijimambo vya pembeni huko vinagharimu haya wala sio michango.
 
Napenda kutoa ushauri ufuatao kwa watu wenye ushawishi kwa jamii;

1. Kukitokea maafa/janga la kitaifa, usichangishe fedha. Sheria ya usimamizi wa maafa ya mwaka 2022, kifungu cha 26(2) inasema jukumu la kuchangisha litafanywa na Kamati ya maafa iliyo chini ya ofisi ya Waziri mkuu, kupitia akaunti maalumu.

2. Ukichangisha fedha kwa matatizo mengine ambayo si maafa (eg matibabu, elimu, yatima) usitumie namba/akaunti binafsi. Ni kosa kisheria. Tumia taasisi (NGO) iliyosajiliwa.

Kwa mujibu wa Sheria ya NGO namba 24 ya mwaka 2002, kifungu cha 32, michango ya kibinadamu (charitable initiatives) inaratibiwa na mashirika yaliyosajiliwa na sio mtu binafsi. Lengo la sheria ni kuweka "Check & Balance" ili kudhibiti ubadhirifu kwa sababu NGO inafanyiwa auditing angalau mara 2 kwa mwaka (internal & external).

3. Kama unataka kumsaidia mtu na huna NGO, tumia namba za mhusika mwenyewe, lakini kwanza upate kibali kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya. Kifungu cha 122 cha sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 inataka michango inayokusanywa na mtu binafsi kwa ajili ya "charity" ipate kibali kwa DC.

#Swali: Je watu wanafahamu haya?

#Jibu: Hapana. Kuna watu wanachangisha pesa kwa nia njema kabisa (utmost good faith) lakini hawajui utaratibu wa kisheria ulivyo.

#Swali: Je nini kifanyike?

#Jibu: Wapewe elimu. Hawapaswi kutishwa, kubezwa au kukatishwa tamaa. Kama mtu amechangisha fedha kupitia akaunti yake binafsi ili aokoe maisha ya mgonjwa kwanini umshtaki? Ni kweli hajafuata utaratibu lakini kafanya jambo jema. Kwahiyo kunaweza kuwa na "actus reus" lakini kusiwe na "mens rea" na hivyo ikawa ngumu kuestablish jinai.

#Points3ZaKukariri;
1. Michango ya maafa/majanga inakusanywa na serikali tu.

2. ⁠Michango ya "charity" inakusanywa na taasisi/NGO iliyosajiliwa na inayowasilisha auditing report wizarani.

3. ⁠Ukitaka kuchangisha na huna NGO tumia namba/akauti za mhitaji mwenyewe kwa kibali cha DC.

Use#UshauriKwaSerikali: Watanzania wanapendana sana, lakini wengi hawana imani na serikali kuhusu michango. Wanakumbuka kuchangia wahanga Kagera pesa zikabadilishwa matumizi. Kwahiyo tumieni watu wenye ushawishi kuhamasisha (eg wasanii, viongozi wa dini, wanamichezo, wanahabari etc).!
 
Napenda kutoa ushauri ufuatao kwa watu wenye ushawishi kwa jamii;

1. Kukitokea maafa/janga la kitaifa, usichangishe fedha. Sheria ya usimamizi wa maafa ya mwaka 2022, kifungu cha 26(2) inasema jukumu la kuchangisha litafanywa na Kamati ya maafa iliyo chini ya ofisi ya Waziri mkuu, kupitia akaunti maalumu.

2. Ukichangisha fedha kwa matatizo mengine ambayo si maafa (eg matibabu, elimu, yatima) usitumie namba/akaunti binafsi. Ni kosa kisheria. Tumia taasisi (NGO) iliyosajiliwa.

Kwa mujibu wa Sheria ya NGO namba 24 ya mwaka 2002, kifungu cha 32, michango ya kibinadamu (charitable initiatives) inaratibiwa na mashirika yaliyosajiliwa na sio mtu binafsi. Lengo la sheria ni kuweka "Check & Balance" ili kudhibiti ubadhirifu kwa sababu NGO inafanyiwa auditing angalau mara 2 kwa mwaka (internal & external).

3. Kama unataka kumsaidia mtu na huna NGO, tumia namba za mhusika mwenyewe, lakini kwanza upate kibali kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya. Kifungu cha 122 cha sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 inataka michango inayokusanywa na mtu binafsi kwa ajili ya "charity" ipate kibali kwa DC.

#Swali: Je watu wanafahamu haya?

#Jibu: Hapana. Kuna watu wanachangisha pesa kwa nia njema kabisa (utmost good faith) lakini hawajui utaratibu wa kisheria ulivyo.

#Swali: Je nini kifanyike?

#Jibu: Wapewe elimu. Hawapaswi kutishwa, kubezwa au kukatishwa tamaa. Kama mtu amechangisha fedha kupitia akaunti yake binafsi ili aokoe maisha ya mgonjwa kwanini umshtaki? Ni kweli hajafuata utaratibu lakini kafanya jambo jema. Kwahiyo kunaweza kuwa na "actus reus" lakini kusiwe na "mens rea" na hivyo ikawa ngumu kuestablish jinai.

#Points3ZaKukariri;
1. Michango ya maafa/majanga inakusanywa na serikali tu.

2. ⁠Michango ya "charity" inakusanywa na taasisi/NGO iliyosajiliwa na inayowasilisha auditing report wizarani.

3. ⁠Ukitaka kuchangisha na huna NGO tumia namba/akauti za mhitaji mwenyewe kwa kibali cha DC.

#UshauriKwaSerikali: Watanzania wanapendana sana, lakini wengi hawana imani na serikali kuhusu michango. Wanakumbuka kuchangia wahanga Kagera pesa zikabadilishwa matumizi. Kwahiyo tumieni watu wenye ushawishi kuhamasisha (eg wasanii, viongozi wa dini, wanamichezo, wanahabari etc).!
 
waTz hamjui sheria, na hilo ndio tatizo. Na serikali imezificha kwenye makaratasi badala hata waanzishe kipindi cha mahakama live kama kipindi cha judge Judy channel e, ili watu wa kesi flani ambazo ni za kutoa knowledge kwa wananchi waelewe sheria inasemaje waone live kila kitu, ushahidi, maelezo hadi hukumu.

alichofanya huyo binti amevunja sheria, na sababu alikua hajui sheria hio, ila kutokujua sheria hakukupi kusanehewa kisa hujui sheria. I'm.in law issues, hekima tu is what she need to wish itumike, but ametenda kosa.
Bora hata angekua hajatumia angekua na room ya kusema watu walikua bado wanachanga ningeelekeza kamati ya maafa
 
Kwani kuna mtanzania mwenye akili timamu alichanga kwa Niffer kweli??Watu wanapesa za kuchezea

Na hawa polisi - hilo ni suala la kumleta DSM kweli, mbona kama resources zimepotoea..- huyo ingieni kwenye akaunti take aseme alipokea Tshs. ngapi..hakiki..ichomlewe iende sijui ndo hiyo account ta BOT mpeni onyo kali - mwacheni aendelee kuzisaka..hali ngumu.
 
Back
Top Bottom