Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Polisi wamsafirisha Niffer hadi Dar kutokea Dodoma baada ya kujisalimisha kufuatia agizo la Waziri Mkuu la kukamatwa

Jeshi la Polisi limemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam mfanyabiashara wa mtandaoni, Jenifer Jovin maarufu Niffer baada ya kujisalimisha polisi jana.

Mfanyabiashara huyo alijisalimisha kwa Jeshi la Polisi jana baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuagiza Jeshi hilo kumhoji kwa kosa la kukusanya fedha za michango kwa ajili ya waathirika walioporomokewa na ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam bila kibali.
Pia, Soma:

Jengo hilo liliporomoka Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo vya watu 16, majeruhi 86 na uharibifu wa mali za mamilioni ya fedha.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 19, 2024 jijini Dodoma, Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Anania Amo amesema Niffer amekamatwa na polisi baada ya kujisalimisha jana.

“Alijisalimisha jana baada ya kumtafuta, tayari tumemsafirisha kwenda jijini Dar es Salaam,”amesema.

Credit: Mwananchi
Majaliwa huyu huyu wa kwa magufuli ndiye aliye toa amli hiyo?
 
Nguvu Gani Nyingi imetumika Hapo? Si ameenda Mwenyewe Polisi

Nchi ina miongozo yake na Sheria zake. Hata Wewe sasa hivi huwezi kwenda Hospitalini ukaanza Kugawa Sabuni na Sukari kwa Wagonjwa Lazima Utakamatwa Tu
Hizo sheria zi kwa aina fulani ya watu, wale watekaji wa yule bonge huyo Kasimu champion wa matamko ametoa tamko gani? Je ametoa tamko lolote kuhusu companies na engineers pamoja na mmiliki wa jengo?
We ain't fools, we can read through that stupid Kasimu.
 
Jaribu Kwenda Kutoa Msaada hata Shule ya Msingi hapo Mtaani Kwenu bila Kuomba Kibali kwa Wenyeviti wa Mtaa na Mabalozi halafu Waambie Mbona Watekaji wa Bonge Hawajakamatwa Uone Utakachofanywa

Huwezi acha Watu wengine wasifuate Miongozo ya Nchi kisa Mambo Mengine hayajafanyiwa kazi au yapo kwenye Uchunguzi.. Tatizo la Watanzania Hatupendi Kuviacha Vyombo vyetu vifanye Kazi ni kulaumu tu kwenye Keyboard ⌨️
 
Jaribu Kwenda Kutoa Msaada hata Shule ya Msingi hapo Mtaani Kwenu bila Kuomba Kibali kwa Wenyeviti wa Mtaa na Mabalozi halafu Waambie Mbona Watekaji wa Bonge Hawajakamatwa Uone Utakachofanywa

Huwezi acha Watu wengine wasifuate Miongozo ya Nchi kisa Mambo Mengine hayajafanyiwa kazi au yapo kwenye Uchunguzi.. Tatizo la Watanzania Hatupendi Kuviacha Vyombo vyetu vifanye Kazi ni kulaumu tu kwenye Keyboard [emoji3491]
Utakuja kubaliana na hii yakikufika hii dunia kigeugeu sana yaani ujue inapo mgeoka huyu nawewe kesho itakugeuka. Kumbuka Sabaya
 
Sasa hii ni akili au makamasi? Yaani mtu kutoa sadaka na penyewe akamatwe?
Ndio Utakamatwa maana si kila Sadaka ni Njema, na kama Unatoa sadaka ikaleta madhara kwa Wahusika Utajibu pia. Ndio maana Unaambiwa kaombe Kibali cha Kutoa Sadaka ili hata Jambo lolote likitokea Hutawajibika Maana Ulipewa Kibali

Kwani Nyie hamjawahi kwenda Hata Kutembelea Jela wafungwa. Unapeleka Chakula Ila Utaambiwa kionje Kwanza Hata Kama Umempelekea Mzazi wako huko
 
Mwamposa aliwajibika kwa kuuwa watu uwanjani?
 
Huyu muhaya wenu ajifunze kutumia akili na aache kiherere, jana althubutu hadi kujibizana na waziri mkuu unategemea nini kweli?
Mbona hakujibizana na kifusi?. Sifia lakini sisi kwenye maafa sawa na mavi tu. Mnaona watu hawana thamani kwenu. Pale mgesikia kunamtoto wa waziri mkuu au wa rais naye kafukiwa mngejipanga kutoa hata jiwe mojamoja kwa mikono ili hatoke
 
Mwamposa aliwajibika kwa kuuwa watu uwanjani?
Swali lako halina Logic na Critical Thinking
Mwamposa aliitwa Polisi na Kwenda Kujieleza, kama Niffer

Kwahiyo Leo hii Raisi au Diamond platinum akipiga kampeni au Show Uwanja wa Mkapa Hapo watu wakakanyagana wakafa Utasema Aliwauwa Uwanjani?

Utathibitishaje aliwaua wakati hakumgusa hata Mtu kumuua!
 
Mkuu umesoma na kuelewa hiyo namba 2 inaeleza nini?
Hicho kifungu kinaeleza kwamba mtu akikusanya fedha za maafa ni lazima.aziwasilishe zote kwenye kamati ya maafa.
Wangetakiwa wasubiri huyo binti achangishe fedha na akishamaliza waone atazifanyeje. Kama zisingewasilishwa kwenye kamati ndio angekamatwa kwa kuvunja sheria.
Kuhusu kujua kiasi cha fedha alichokusanya na kilichowasilishwa kwenye kamati ya maafa kama ni sawa hiyo ni kazi ndogo sana kwa Financial Intelligency Unit ambao wapo wizara ya fedha .
Hii ishu Majliwa amekurupuka ingewezekana wangemtumia huyu binti positively angeweza kuwakusanyia hela nyingi sana kusaidia wahanga wa hilo janga la ghorofa
Ingewezekana Majaliwa badala ya kumtangaza vile negatively kama mtuhumiwa .
Angeagiza watu wake wa kitengo cha maafa wamuaproach positively wamuambie tumekuona mitandaoni umejitolea kukusanya fedha kwa ajili ya maafa ya kuanguka ghorofa kariakoo wangemshukuru kwa kuwasaidia kazi na wangempa maelekezo yafuatayo:-
1. Fedha za maafa zikikusanywa na mtu binafsi zinatakiwa ziwasilishww kwenye kamati ya maafa kwa mujibu wa sheria.
2. Wangemweleza pia michango anayokusanya inafatiliwa na serikali kupitia financial intelligence unit asijaribu . kuchakachua .
3. Wangempa support na promotion wangeweza kutangazia umma kwamba wanafahamu huyo binti anaendesha harambee ya kukusanya fedha za wahanga kwa niaba ya kamati.
(sheria inaruhusu kamati ya maafa kuomba msaada wa huduma mbalimbali)
4. Wangempa cheti cha pongezi na kutambua kazi aliyoifanya pamoja na kutangazia umma kiasi alichokusanya na kukiwasilisha kwenye kamati ya maafa

Hili suala lingechukuliwa hivi kwa mtazamo wangu huyo binti angeweza kuwakusanyia hao kamati ya maafa fedha nyingi sana.
Ila.lilivyochukuliwa limeleta picha ya hovyo ikiwemo kumuaibisha waziri mkuu mwenyewe pamoja na huyo binti .
Nampongeza huyo binti kwani anaonyesha anaujasiri pia anakubalika na watu wa kawaida.
Manake naamini Majaliwa michango aliohamasisha ya hili janga la kariakoo zitachangia taasisi tu za umma au binafsi tena zitafanya hivyo kwa kujipendekeza .
Huto binti waliomchangia ni kwa moyo wa dhati wa kujitolea kwa jinsi wanavyomwelewa na kumuamini na sio kujipendekeza.
Tutambue pia kushawishi watu wakuchangie fedha ni kazi ngumu sana na ukitaka kujua hayo angalia haya ma taasis ya charity yanapotaka kuajiri mtu anayeitwa fundriser hapa inahitajika zaidi soft skills ambazo serikalini hakuna serikali inajua hard skils tu kama za kukusanya kodi sijui kuuunda tasks force .kukamata mali, kufunga akaunti za watu, kutisha kufilisi,kupeleka mahakamani
Umeandika upumbavu mtupu
 
Hito ni kwako wewe na nidhamu yako ua uoga .
Kwangu mimi kusema ukweli sio utovu wa nidhamu
Sasa ukweli kwenye issue ya huyo binti na michango yake huyo.majaliwa karopoka na kakurupuka .
Huto binti hajafanya kosa lolote kwa mujibu wa sheria za nchi hii
Ukikutana na waziri mkuu uso kwa uso unaweza kumwambia kuwa aliropoka?
 
Hivi kwa akili yako kile kigorofa ingetumika nguvu ya haraka Kama kukamatwa kwa huyo dada watu wangekaa chini ya kifusi kwa siku 3?.
Sio kila kitu ni cha kufanya kwa haraka dude sasa useme yaje magreda yatoe kifusi ao waliokuwapo hai si wangekufa vizuri,kumbuka mule waliokwisha kufa tangia siku ya kwanza wapo wengi tu na waliopo hai ndo walikuwa wanatolewa taratibu lile zege plus nondo sasa unakuta layer mbili zimekutana na pipo zipo down zinaita
 
Watu hawajui kitu Ndugu Yangu.. Tanzania Tunapigana na Maadui Wengu Nyerere alisema Watatu.. Ujinga ,umasikini na Maradhi.

Ujinga unamfanya Jamaa anadhani Ghorofa likianguka basi Ukileta Magreda Mengi Unaokoa Hajui kuna Kuta Zikiguswa Vibaya Tu Zinawaangukia hata Walio hai
 
Back
Top Bottom