Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
Kama alikuwa anajiuza watueleze ni kiasi gani cha fedha binti huyo alikubali kwa ajili ya kubakwa na vijana wengi hivyo?

Aisee
 
Regardless kama aliyoyaongea yalikuwa ya kweli au uongo ila RPC Mallya hakutakiwa kuongea aliyoyaongea especially this time!

Hawa viongozi sijui kwann huwa wanatanguliza utemi na ubabe badala ya busara
Unafikir waliposema kazi ya upolisi ni kazi ya laaaana walikua na maaana gani
 
Kwa hyo kurasaa ndio ishafungwa Kwa namna hyo 🙆🙆
 
Yule dada akijichanganya kukubali alijiuza maana yake anajitia hatiani na yeye mwemyew. Kaingiliwa kinyume na kasambaza picha za ngono atakula kama miak 15 hivi. Asijichanganye
Hakuna namna yoyote ya kuthibitisha kuwa mtu anajiuza. Kuingiliwa kinyume na maumbile atasema haikuwa kwa ridhaa yake, na video hakusambaza yeye.
 
Yule binti kama victim anahitaji mwanasheria binafsi tena anayejiamini kweli, naona polisi wameamua kumuangushia jumba bovu.
 
Wamelindana Kwa sababu wa bakaji ni maafisa wa polisi.Nimeamini polisi wako juu ya sheria
 
Hakuna namna yoyote ya kuthibitisha kuwa mtu anajiuza. Kuingiliwa kinyume na maumbile atasema haikuwa kwa ridhaa yake, na video hakusambaza yeye.
Ah wapi.. kama alikuwa anajiuza kurekodiwa alitegemea video ikatumike wapi kama sio kuntangazia biashara? Kafanya matangazo ya biashara yake. Hil pia ni kosa kisheria... hawa madogo wasicheze kabisa na sheria mana ukweli uko dhahir. Anaambiwq aombe msamaha na kaomba! Atawez kuelezea msamaha ule wa nn?

Hapo ataingia kwenye kosa lingike kisheria kudanganya umma tena mahakamani.. ibara ya ngapi ile? BICHWA KOMWE -
 
Ndugu zangu Watanganyika,

Tusimalize maneno. Tujikumbushe hili suala la kubakwa lilitendeka mwezi April likaja kutrend mwezi August, kama kweli alibakwa kwanini muda huo hakufika police kushitaki. Mimi hili suala nishalitilia shaka hata kipindi habari zake zinaanza kutoka.

Huyu Binti hajabakwa ni kama alitaka mwenyewe. Wale vijana ni kama walimlipa ili kumpiga mande na kukubaliana kurecord hivo. Kujamiiana kikahaba lazima lugha chafu na kaubabe kapite, wale hawakuwa wanafanya sex kistaarabu.

Tujiulize maswali, yule Binti aliingiaje geto kwa wale vijana, na wale vijana wambake yule Binti Kwa sababu zipi na wanawake wamejaa mjini. Unaweza japo kuona muonekana wa yule Binti unaoneka sio wa Binti mwenye maadali mema.

Jeshi la police lina intelejensia kali, halishindwi kupata ushahidi mdogo kama huo, naamini police wanaona kama Binti alilidhia mwenyewe Sasa hapo alibakwaje?

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Theopista Mallya amesema jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam limekamilika.

Vijana hao wanaodaiwa kutumwa na afande, wanne kati ya sita wameshakamatwa ambao walipanga na kutekeleza uhalifu huo. Tukio hilo liliibua mijadala mikali maeneo mbalimbali, ikiwemo mitandaoni.

Ukamataji huo umewagusa pia watu wengine wanane, kati yao wakiwemo wanne waliokamatwa kwa kukiuka sheria na kusambaza picha mjongeo (video) za tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii, zilizoonyesha tukio hilo la ukatili.

Jana Jumapili, Agosti 18, 2024, RPC wa Dodoma, Theopista akizungumza juu ya kinachoendelea kuhusu watuhumiwa hao, alisema katika uchunguzi Jeshi la Polisi lilibaini vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.

“Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza ‘kahaba’.”
“Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo” alisema Kamanda huyo.

#KitengeUpdates

FB_IMG_1724050162503.jpg
 
Wakuu,

Naona tunaenda kufanyiwa maigizo tena na kuna mtu anataka kulindwa. Eti uchunguzi umebaini vijana wale hawakutumwa na 'afande na kwamba vijana wale walikuwa kama wavuta bangi tu na yule binti alikuwa kahaba!

Mpaka utambulisho wa moja wao umebainika halafu leo maneno yanageuzwa hivi!

Nilikuwa saluni majuzi hapa, si mnajua stori za saluni zinavyonoga sasa wakawa wanajadili suala hili, sasa kwenye stori wakawa wanasema kwamba mmoja ya wale vijana waliohusika kwenye kumbaka binti ni mtoto wa askari mwenye cheo kikubwa, sasa katika malipo vijana wengine walipunjwa mgao, ili kumkomoa jamaa kwakua baba ake ni askari ndio wakaamua liwalo na liwe, wakaachia kideo. Ni kweli au ni story tu za vijiweni kama nyingine, sijui!

Anyways, kwa mara nyingine naona sheria inaenda kupindishwa wenye nguvu wanaenda kushinda hata kama ni wanyama na makatili wanaostahili kufungwa milele

=====

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), imesema bado haijafikishiwa jalada la kesi ya vijana watano wanaotuhumiwa kutekeleza tukio la ubakaji na ulawiti wa binti anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha jongefu (video) kuhusu tukio hilo zilisambaa Jumapili ya Agosti 4, mwaka huu kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha vijana watano wakimbaka na kumwingilia msichana huyo kinyume cha maumbile.

Pia soma: Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama

Katika video nyingine watuhumiwa hao wanasikika wakimhoji binti huyo na kumshurutisha amwombe radhi mtu aliyetajwa kwa jina la afande, naye alifanya hivyo.

Hata hivyo, katika taarifa aliyoitoa kwa umma Agosti 9, 2024, Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime alisema uchunguzi umewezesha kubaini tukio hilo lilifanyika Mei 2024 katika eneo la Swaswa jijini Dodoma.

Aliwataja vijana waliokamatwa kwa kosa la kumlawiti na kumbaka binti huyo ni Clinton Damas jina maarufu Nyundo, Praygod Mushi, Amini Lema na Nikson Jakson.

Misime alisema watuhumiwa hao walikamatwa mkoani Dodoma na Mkoa wa Pwani na Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili ambao walikuwa hawajapatikana mpaka wakati huo.

Mwananchi leo Jumapili Agosti 18, 2024 limezungumza na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Sylvester Mwakitalu kuhusiana na hatua iliyofikiwa katika uchunguzi wa sakata hilo na kipi kinaendelea.

Mwakitalu amesema jalada la tukio hilo bado halijamfikia mezani kwake kwa kuwa bado linaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi.

“Bado upelelezi unaendelea na likifika kwangu ni kukamilisha upelelezi tu, isipokuwa kwa sasa bado jeshi linaendelea na upelelezi,”amesema DPP Mwakitalu.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa uchunguzi wa tukio hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Ramadhan Kingai amesema aulizwe Kamanda wa Mkoa wa Dodoma na Msemaji wa Jeshi la Polisi watakuwa na majibu sahihi.

“Suala hilo mtafute Kamanda wa Polisi Dodoma au Msemaji wa Jeshi la Polisi watakueleza hatua za tukio hilo lilipofikia,”amesema Kingai

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Theopista Mallya amesema jalada la tuhuma hizo limekamilika na kwamba kesho Jumatatu Agosti 19, 2024 atafuatilia kama litapelekwa mahakamani.

Amesema katika uchunguzi, Jeshi la Polisi limebaini vijana hao waliotuhumiwa kwa madai ya kutumwa, walikiri kutoagizwa na askari kama ilivyoelezwa.

"Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza 'kahaba’.

"Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo" amesema kamanda huyo.

Hata hivyo, Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Polisi, Misime kutaka kujua kama watuhumiwa wengine wawili waliobakia kati ya sita wanaotuhumiwa hakupokea simu na alipotumiwa ujumbe kwa whatsapp aliousoma lakini hakujibu chochote.
Jeshi linatafuta njia ya kujisafisha inavosemekana wale vijana walikua maafande wengine kutoka jwtz wengine jkt walitumwa Na afande Wa kike Na Uyo Mume wa afande naye Ni mwanajeshi wote maafande...hiki kitendo kimelichafua Sana jeshi ndomana wanakanusha
 
Ah wapi.. kama alikuwa anajiuza kurekodiwa alitegemea video ikatumike wapi kama sio kuntangazia biashara? Kafanya matangazo ya biashara yake. Hil pia ni kosa kisheria... hawa madogo wasicheze kabisa na sheria mana ukweli uko dhahir. Anaambiwq aombe msamaha na kaomba! Atawez kuelezea msamaha ule wa nn?

Hapo ataingia kwenye kosa lingike kisheria kudanganya umma tena mahakamani.. ibara ya ngapi ile? BICHWA KOMWE -
Keyword "KAMA", hilo neno tayari limeshabeba walakini na sheria haitakiwi kuwa hivyo. Anything that can't be proven beyond reasonable doubt, has loopholes.
 
Ndugu zangu Watanganyika
Tusimalize maneno,
Tujikumbushe hili suala la kubakwa lilitendeka mwezi April likaja kutrend mwezi August, kama kweli alibakwa kwanini muda huo hakufika police kushitaki,
Me hili suala nishalitilia shaka hata kipindi habari zake zinaanza kutoka.

Huyu Binti hajabakwa ni kama alitaka mwenyewe,
Wale vijana ni kama walimlipa ili kumpiga mande na kukubaliana kurecord ivo
Kujamiiana kikahaba laZima lugha chafu na kaubabe kapite, wale hawakuwa wanafanya sex kistaarabu.

Tujiulize maswali,Yule Binti aliingiaje geto Kwa wale vijana, na wale vijana wambake yule Binti Kwa sababu zipi na wanawake wamejaa mjini,
Unaweza japo kuona muonekana wa yule Binti unaoneka sio wa Binti mwenye maadali mema.

Jeshi la police Lina intelejensia kali, halishindwi kupata ushahidi mdogo kama huo, naamini police wanaona kama Binti alilidhia mwenyewe Sasa hapo alibakwaje?
Hivi mkuu wewe waona ni jambo rahisi mwanamke abakwe aende mahakamani? Mabinti wengi tu wanabakwa hawaendi mahakamani kwa kuogopa aibu na kuwa judged na jamii kama wewe unavyofanya hapa. video inajieleza kabisa kuwa kile kitendo alikifanya bila ridhaa yake, video inajieleza kama walikuwa wakimpa adhabu.
 
Back
Top Bottom