Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
HIVI RAISI SAMIA HII TAARIFA HAJAIONA ILI AMTETEE MWANAMKE MWENZAKE?
 
"Neno askari ni General (jumla) kwa kuwa hata mgambo ni askari, hivyo hatuwezi kulifafanua zaidi kwa kuwa haikubainishwa wazi na tunaliacha hivyo" amesema kamanda huyo.
Duh,
Huu ni ubabaishaji wa hali ya juu sana.
Hawezi kufafanua kivipi wakati ako na watuhumiwa mkononi?
Huyu ni jipu amekosa mtumbuaji tu
 
Regardless kama aliyoyaongea yalikuwa ya kweli au uongo ila RPC Mallya hakutakiwa kuongea aliyoyaongea especially this time!

Hawa viongozi sijui kwann huwa wanatanguliza utemi na ubabe badala ya busara
Tanzania watu wanapenda kulindana hata kama ushenzi umefanyika vp

Ova
 
Rais Samia masaibu haya yaliyo mpata huyu bint, ambayo Sasa inaonekana Polisi wako wanaonesha wanataka kupindisha haki au sheria. Hiki kitakuwa ni kipimo chetu kwako, wewe ukiwa Rais wetu, Mzazi, na zaidi ya yote wewe ni muumini wa dini ya Kiislam. Mama, huyu bint alilawitiwa (Kwa mujibu wa video) na watu watano. Rais wetu sema neno kuhusu hili kwani Polisi wako wanamlinda 'Afande' mwezao. Ukikaa kimya sisi wananchi wa kawaida Sana hasira zetu tuta zielekeza kwenye sanduku la kura dhidi ya CCM na wewe.
 
Kilichobainika vijana hao hawakutumwa na askari, walikuwa kama walevi na wavuta bangi tu, lakini yule dada alikuwa kama anajiuza 'kahaba’.
Ukisoma hapo tuu hata kama ni mtoto wa wa miaka mitano atajua hawa jamaa ni waongo na kuna kitu wamekificha, tangu mwanzoni tuu walionekana kabisa wanatafuta namna ya kuyapaka mavi marashi ili yanukie bora hata wangekua wanatumia akili kwenye kudanganya sio wanaongea utoto ambao hata mwehu hawezi kukubali
 
Hii nchi haki ni changamoto video inaonyesha dhahiri kua binti kafanyiwa unyama ule kwa maelekezo ya mtu(afande)..inakuaje tena uchunguzi uonyeshe kua binti alikua kahaba na hao wadau ni walevi na wavuta bange...BORA ANGEKUEPO mwenda zake walau tungeupata ukweli mapema.
 
Back
Top Bottom