Polisi Wanatetewa Haki Zao Lakini Wanaenda Kumkamata Mtetezi Wao

Polisi Wanatetewa Haki Zao Lakini Wanaenda Kumkamata Mtetezi Wao

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Polisi uitwa Jeshi la kulinda watu na mali zao, lakini jeshi letu hili la polisi limekuwa ni jeshi la kulinda wanasiasa na familia zao. Hakuna watu nchi hii wanaogopa kupoteza kazi kama polisi na walimu, hususani polisi ndio kabisaa na wengi maisha yao ni Duni. Polisi ndio taaluma pekee inayoweza kuongozwa na mtu ambaye hana Fani ya Upolisi au ambaye hajapita mafunzo ya upolisi. Tuchukulie wakuu wa Wilaya wote Nchini, kwa ujumla uwa ndio viongozi wa Ulinzi na Usalama kwenye Wilaya husika, ,maana yake jeshi zima la polisi lililoko kwenye Wilaya yake liko chini yake na yeye ndio anayepanga hatua za kiusalama za wilaya.

Sasa ni wakuu wa Wilaya wangapi wenye mafunzo ya kijeshi au kipolisi mpaka wapewe dhamana ya ukuu wa ulinzi na usalama wa Wilaya. Tuchukulie Msanii Jokate Mwegelo ambaye ni alikuwa kwenye ushiriki wa Miss Tanzania, akaingia kwenye Mziki na Uigizaji kidogo badae akala shavu la Kisiasa na sasa ni Mkuu wa Wilaya. Inakuwaje mtu ambaye hana professional ya Ulinzi kuwa Mkuu wa Ulinzi na Usalama, jeshi la polisi likiwa chini yake. Mtu aliyeteuliwa Kisiasa anakuwaje mkuu wa jeshi la polisi.

Tanzania inavyuo vinavyotoa kozi za Uongozi, basi hizi idara ya Ukuu wa Wilaya zisiwe za kuchaguliwa ziwe za watu kuomba ajira, au watu wanaoteuliwa wawe wamesoma kozi za uongozi kama Public Administration au Leadership and Management, sio tu kuchukua kada wa chama fulani na kumuweka ambaye mwisho wa siku atafanya kazi kwa matakwa ya aliyemteua na si kufanya kazi kwa Professionalism kwa sababu yeye kateuliwa tu na Uongozi sio Taaluma yake.

Tukija kwenye sakata la kisiasa la kukamatwa kwa Lissu, ni wazi kabisa wanamdhimisha kiasa hili sera na falsafa zake zisiingie kwenye Akili za watu na wengi wanaoongoza jeshi la polisi kufanya ukamataji ni hao hao wanasiasa ambao hawajui hata Protocol, maadili na miiko ya upolisi. Wanaendeshwa kimiemuko, na polisi wengine wamewekwa au kuteuliwa kwa matakwa ya kisiasa tu kutumikia kiongozi aliyewaweka.

Hatukatai kuna polisi wengi wazuri na wanafanya kazi kwa weledi, ila kwa sababu ya polisi wengi wapo kimasirahi na si kitaalamu basi wanapelekea na wenzao kufanya kazi kama wao.

Unamkamataje mtu anayeitetea kesho yako? Anayetetea usawa wa haki na sheria? Anayepinga ufisadi?
 
Mbwa hata ukimrushia tonge la ugali atalila lakini hatakuwa na shukrani endapo ataamriwa na mwenye mbwa kamata mtu, atakamata bila kukumbuka kuwa mtu huyo alimrushia tonge akala na kushiba. Polisi hawana namna ya kukataa amri ya serikali yake. Polisi ni chombo cha serikali watakuambia wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria
 
Back
Top Bottom