Polisi waruhusu Mikutano ya hadhara.. Je, wamemgeuka Katambi?

Nakuona kabisa ukitikisa kichwa kiongozi wangu! yaaani sijui watu wamelewa pombe! huku ivi huko vile duuuu!
Nchi iliyokosa mifumo imara ya uongozi ( Transparency and responsibilities) ndio inakuwa na mambo haya
 
Kuna lililotekelezwa au muda Bado?
UTEKELEZAJI UNEANZA ILA UNAFANYIKA CHINI CHINI.

1. Nadhani ulimsikia Nchimbi akiongelea katiba Mpya na haki za Binadamu.

2. Nadhani umeona mikutano ya siasa kurudishwa.

3. Hautasikia Jinai kama Ugaidi, Uchochezi, uhaini kwasababu za Afcon na Commonwealth.

4. Soon watu wataanza kuachiwa na kila kitu kitaanza kwenda sawa..

NIMEKUWA NIKISISITIZA SANA MWISHO WA UBAYA NI AIBU.
 
Mambo mengine hayahitaji hata shule,wao kanyaga twende na watu wao kina Lukas mwashambwa na nduguye tlahtlah!
 
Yaani hao jamaa wanajiaibisha sana kwa kufanya mambo ya kukurupuka.

Unatangaza UGAIDI nchini halafu hapo hapo unataka watalii na pia unaandaa AFCON.

Ndiyo tatzo la jesh la polisi kujiingiza kwenye siasa.
Sasa sindio maana wamechanganyikiwa wameona watu wame wakalia kooni 😆😆😆

Wameshtuka kuwa propaganda Yao wameifanya kwenye wakati mbaya

Huku Afcon huku commonwealth, Wameona watanyang'anywa ushiriki wa Afcon so wameona wapige U-turn 🤣😆 hii Nchi in vituko

Kile kiwanja Cha Arusha watafugia mbuzi dadeki inapaswa watu wapush agenda vya kutosha kwamba Serikali yenyewe ndio ulisema kuwa Kuna ugaidi halafu tuone yajayo 😆
 

Pale mwenye mbwa akibweka kwa niaba ya mbwa wake tena kwa sauti ya ajabu mwisho humtuma huyo mbwa abweke kwa usahihi.

Matatizo yetu ni ya kutengenezwa.
 
Lakini Waziri wa mambo ya Ndani amesema hakuna Ugaidi,ingawa magaidi wapo.
 
Swali la kujiuliza, ni vipi mikutano inaruhusiwa katikati ya wimbi la magaidi? Polisi ambao ni wakamataji wa hayo makundi ya magaidi wanadai nchi imekuwa shwari sasa kuliko wakati wote!
 
Kuna maandishi yoyote au Tangazo la Taarifa kwa Umma? (Mm sijaliona).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…